Nani alaumiwe?

Satuuuu

JF-Expert Member
Dec 3, 2015
1,849
1,993
Imekua kawaida katika jamii ya sasa kukuta baadhi ya familia baadhi ya watoto wanajikuta katika makundi ambayo jamii inawetenga na kuwaona wamearibika au hawafai tena katika jamii. Kuna maswali mengi yakujiuliza pale idadi ya watu hawa inapo ongezeka katika kizazi cha sasa,Je ni malezi,Je ile tabia ya wanafamilia kurekebishana na kushauriana imetoweka ? Au elimu ya kujitambua na kujithamini haitolewi kwa vijana.
 
Hapo cha kwanza kabisa ni wazazi kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulea, kutoa matumizi nk kutokana na maisha kuwa magumu kwa sasa. Unakuta mzazi anaondoka asubuhi kwenda kutafuta riziki, akirudi anapitia kwenye kahawa, bar, mchepuko nk kurudi nyumbani saa 6 usiku watoto wote wamekwisha lala, sasa hapo watoto wakianza tabia mbaya siyo rahisi kugundua na kuchukua hatua.
 
Malezi ya mtoto yanategemea sana kupatikana katika mihimili mitatu 1.Mzazi 2.Dini 3.Serikali/Jamii kwa ujumla wake..
Sasa mihimili yote hiyo imekengeuka sana Mzazi hataki kumlea mtoto katika njia ile ipasayo mtoto wa 2yrs anapelekwa boarding..ili hali pale ndiyo mtoto anapaswa kuwa karibu na mzazi...Dini zetu nyingi zimepotoka sana watu wamekuwa wakiangalia maslahi binafsi hata mtoto akienda huko hakuna anachojifunza zaid ya somo la kutoa sadaka tu..Serikali kwa maana ya Mashulen huko ndiyo kumekuwa tatizo hakuna walimu wenye wito wa kuhakikisha watoto wanakuzwa katika maadili yapasayo..Mwalimu anasema achana na hao watoto ili mradi we unalipwa mshahara na Jamii vivyo hivyo hakuna mwenye tym na mtoto asiye wake..hata amkute mtoto anafanya makosa namwacha...So wote tunaingia kwenye lawama hizi..
 
Point nzuri sana, hayo yanatokana na kubadilika kwa Mfumo wa maisha & Watu wanaotuzunguka na vitu tunavyoviona kila siku. kwamfano Media, social netwoks na cares za wazazi kwa watoto zimekuwa tofauti sana na miaka ya nyuma.
 
Mtoto anakuwa chini uangalizi wa mzazi/mlezi pale anapokuwa under 18,akiharibikiwa chini ya hapo lawama zote ni za mzazi/mlezi lakini akianza kuharibika baada ya kuvuka umri huo hapo asilaumiwe mtu.
 
Back
Top Bottom