Nani alaumiwe, ni CHADEMA au CCM?

Nani alaumiwe, ni CHADEMA au CCM?

Rose Mayemba

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2012
Posts
721
Reaction score
1,017
Tangu Tanzania iingie kwenye ushindani mkubwa katika siasa hasa kwa vyama hivi viwili( CHADEMA & CCM), watanzania wengi wasio na hatia wamepoteza uhai wao na wengine kupoteza viungo vyao( tukiacha wakati wa CUF na NCCR mageuzi).

Nawakumbuka akina Dr ulimboka, Daudi Mwangosi, Said kubenea, mauaji ya Arusha( tarehe 5/01/2011 na yale yaliyotokea hivi karibuni). Serikali yetu tukufu iliunda tume kufuatilia vitendo hivyo vya kinyama na kikatili ili baadae ije na majibu ya kuwaridhisha watanzania, si hivyo tu bali tujue muafaka wa wahusika wa vitendo hivyo viovu(nasikitika mpaka leo hakuna kunachoendelea)

Kinachonishangaza ni kwamba serikali yetu kupitia chama chake imesema inawafahamu wahusika wa matukio hayo yote na imewatangaza hadharani wahujumu hao wa maisha ya watu lakini hakuna hatua zozote za makusudi zinazochukuliwa juu yao. CHADEMA ni watuhumiwa namba moja wa mauaji na ukatili huu unaoendelea dhidi ya watu hawa.

Kwanini inatumia pesa nyingi kuunda tume kuchunguza matukio haya ilihali wahusika wanawafahamu? . Ama kwanini haijawakamata wanaodai CDM ndo wahusika ili wakasaidie kutoa ushahidi mahakamani? Je huku si kushindwa kuongoza kwa watawala?. Na mbona haijawahi kuleta majibu ya tume hizo tangu zimeanza kuundwa zaidi ya kuwahadaa watanzania?

Kwanini tusiamini kama matukio haya yanafanywa na wao wenyewe huku wakiisingizia chadema?. tumechoka kufungwa macho huku watanzania tuwekwe wazi tujue.

Kama serikali yetu ambayo ndiyo yenye dhamana ya kulinda haki za binadamu imekalia kimya unyama huu nani alaumiwe?.Ni waliofanya vitendo hivyo au wale waliowaacha huru ili waendelee kuyafanya haya?

TUMECHOKA KUONA DAMU ZA NDUGU ZETU ZIKIMWAGIKA...WATANZANIA TUNATAKA AMANI
 
Hili swali mbona liko wazi sana?

Bila ya CHADEMA kuleta tabia yao ya maandamano, kukaidi maagizo ya vyombo vya dola na ugaidi sidhani kama raia wa Tanzania wangeuawa na polisi.

Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na sio matakwa ya CHADEMA!
 
Inaendeshwa kwa kauli za Pinda.... PIGA TU
 
Hamy D
najua chadema ni watuhumiwa no moja, swali langu ni kwamba serikali mbona imekaa kimya huku inatambua chadema wanakiuka sheria ya haki za binadamu? hebu sema kitu juu ya ukimya wa serikali

acha ushamba wewe kwani Chadema ikifanya mkutano wake bila kuingiliwa na polisi mauaji yatatokea wapi?? Au unamaanisha Chadema wakiandamana watu wanakufa automatically??? Nieleweshe hapo
 
Hamy D
najua chadema ni watuhumiwa no moja, swali langu ni kwamba serikali mbona imekaa kimya huku inatambua chadema wanakiuka sheria ya haki za binadamu? hebu sema kitu juu ya ukimya wa serikali

Dada yangu,

Naweza nikasema ukimya wa serikali ni kwa lengo jema tu!

Kwa maana gani; unajua hapa nchini chanzo kikubwa cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi (ukiachilia mbali shinikizo la US kwa hayati mwl Nyerere) ni kupanua wigo wa demokrasia.

Katika azma hiyo ya kupanua wigo wa demokrasia, sio vyema kufuta vyama vya siasa hata kama vinafanya vitendo nilivyo orodhesha hapo awali.

Bali njia pekee ni kuvilea vyama hivyo vinavyo fanya huo uovu kwa lengo la kuviimarisha zaidi ili viweze kufanya siasa zilizo komaa na za kistaarabu.

Aidha, kwa wale wote watakao bainika kufanya vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi hasa katika uharibifu wa makusudi wa amani na utulivu, hao watachukuliwa hatua kali za kisheria, hapa nadhani umeona jinsi Lwakatare na Kileo wanavyo kabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
 
serikali inajua mhusika kuwa yenyewe ndio mhusika,fikiria kama ingekuwa ni Chadema ndio wanahusika wangekaa kimya,mfano mdogo Dr Ulimboka alisema Ighondu anahusika kumteka na kumtesa inatakiwa ashtakiwe kwa ugaidi lakini kimya, mbona hawachukulii hatua,je ingekuwa ni mtu wa chadema ja angeachiwa?imetengenezwa video feki ya Lwakatare tena mhusika hajasema kama Lwakatare ana nia hiyo lakini kupitia ushahidi wa uongo wa video ya mtandaoni alikamatwa na kushtakiwa,kuna kesi huko tabora shahidi ambaye ni askari amekiri mahakamani kuwa Mwigulu Nchemba alikodisha watu waliofanya mauaji lakini hadi lkeo hajakamatwa.
​TAFAKARI NDUGU KWA UMAKINI UTAPATA JIBU!!!!!
 
jamani naomba mwenye mkataba wa ajira ya vijana wa Lumumba autupie humu ndani ili nione kilichopo ndani ya huo mkataba,
 
lwakatare hana kosa la ugaidi hamy, mahakama ilikwisha kufutulia mbali madai hayo..pia kwanini iache eti kisa kudumisha demokrasia? huoni kama wanatuaminisha wananchi kama wao ndo wahusika wa matukio haya?
Dada yangu,

Naweza nikasema ukimya wa serikali ni kwa lengo jema tu!

Kwa maana gani; unajua hapa nchini chanzo kikubwa cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi (ukiachilia mbali shinikizo la US kwa hayati mwl Nyerere) ni kupanua wigo wa demokrasia.

Katika azma hiyo ya kupanua wigo wa demokrasia, sio vyema kufuta vyama vya siasa hata kama vinafanya vitendo nilivyo orodhesha hapo awali.

Bali njia pekee ni kuvilea vyama hivyo vinavyo fanya huo uovu kwa lengo la kuviimarisha zaidi ili viweze kufanya siasa zilizo komaa na za kistaarabu.

Aidha, kwa wale wote watakao bainika kufanya vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi hasa katika uharibifu wa makusudi wa amani na utulivu, hao watachukuliwa hatua kali za kisheria, hapa nadhani umeona jinsi Lwakatare na Kileo wanavyo kabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
 
Dada yangu,

Naweza nikasema ukimya wa serikali ni kwa lengo jema tu!

Kwa maana gani; unajua hapa nchini chanzo kikubwa cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi (ukiachilia mbali shinikizo la US kwa hayati mwl Nyerere) ni kupanua wigo wa demokrasia.

Katika azma hiyo ya kupanua wigo wa demokrasia, sio vyema kufuta vyama vya siasa hata kama vinafanya vitendo nilivyo orodhesha hapo awali.

Bali njia pekee ni kuvilea vyama hivyo vinavyo fanya huo uovu kwa lengo la kuviimarisha zaidi ili viweze kufanya siasa zilizo komaa na za kistaarabu.

Aidha, kwa wale wote watakao bainika kufanya vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi hasa katika uharibifu wa makusudi wa amani na utulivu, hao watachukuliwa hatua kali za kisheria, hapa nadhani umeona jinsi Lwakatare na Kileo wanavyo kabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
we mjinga sana, nia njema kwa watuwanaovunja sheria? maana ya serikali ni nini haswa? Na huyu msajili wa vyama vya siasa anafanya kazi gani kukifuta hiki chama au yeye hajui wajibu wake kwa vyama vinavyopelekea uvunjifu wa amani? Hili swali ulilopewa hata mwenyekiti wako wa chama angelikwepa kama sio kulitolea majibu mepesi kama yako
 
Hamy D
najua chadema ni watuhumiwa no moja, swali langu ni kwamba serikali mbona imekaa kimya huku inatambua chadema wanakiuka sheria ya haki za binadamu? hebu sema kitu juu ya ukimya wa serikali

Madam naomba kwanza hapo kwenye red urekebishe kauli hivi cdm wanamiliki majeshi au wanamiriki siraha ,pia ni shetani tu awezaye kuamini kuwa chadema inaua watu tena ...eti wale wanaukiunga mkono kwa 100%. Huu ni ushetani na laana iliyopitiliza. Mtuhumiwa namba moja ni mwigulu.
 
Hili swali mbona liko wazi sana?

Bila ya CHADEMA kuleta tabia yao ya maandamano, kukaidi maagizo ya vyombo vya dola na ugaidi sidhani kama raia wa Tanzania wangeuawa na polisi.

Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na sio matakwa ya CHADEMA!

Utawala wa sheria upi huo na sheria zipi hizo......na matakwa ya CHADEMA ni yapi hayo?....Kwani maandano au "kuandamana" ni tatizo linaloweza kusababisha watu wafe? Kivipi hebu jaribu kutetea kidogo hoja yako labda waungwana watakuelewa?

Unanikumbusha siku wabunge wa CCM wanapiga kura ya kupitisha bajeti ya serikali yao "sikivu" ya kuua na kutesa raia wake ya mwaka wa fedha 2013/2014 wiki juzi kwa kuitwa majina, pale ambapo kila lilipoitwa jina la mbunge wa CDM wabunge wa CCM walilazimika kuimba wimbo usio na korasi wa....maandamano!!........maandamano!!.....maandamano!!....ilikuwa mithili ya misukule ya pori la "Gamboshi" kwani ni wazi hawa wanaamini kitu wasichokijua.Na hii ikiwa hivi ni wazi utatenda jambo usilolijua na kujikuta kituko!!....This is what is happenning now among CCM members and their allies who are enjoying the sweetness of strong built corrupt system!!...Laiti pale pangekuwa na spika ambaye si mchumia mtumbo akawauliza swali wabunge hawa wa CCM wana maana gani kuimba wimbo huo,hakuna ambaye angetoa jibu la kingia kwenye vichwa vyenye akili kubwa.... zaidi ya mipasho!!

Imefikia wakati viongozi na wana CCM na wapambe wao wamekuwa kama mataahira hivi!!!..... It's absolutely undeniable that you also belong to them,if not give us honest answers for the questions in red above!!
 
Dada yangu,

Naweza nikasema ukimya wa serikali ni kwa lengo jema tu!

Kwa maana gani; unajua hapa nchini chanzo kikubwa cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi (ukiachilia mbali shinikizo la US kwa hayati mwl Nyerere) ni kupanua wigo wa demokrasia.

Katika azma hiyo ya kupanua wigo wa demokrasia, sio vyema kufuta vyama vya siasa hata kama vinafanya vitendo nilivyo orodhesha hapo awali.

Bali njia pekee ni kuvilea vyama hivyo vinavyo fanya huo uovu kwa lengo la kuviimarisha zaidi ili viweze kufanya siasa zilizo komaa na za kistaarabu.

Aidha, kwa wale wote watakao bainika kufanya vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi hasa katika uharibifu wa makusudi wa amani na utulivu, hao watachukuliwa hatua kali za kisheria, hapa nadhani umeona jinsi Lwakatare na Kileo wanavyo kabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Eti waachwe hata wanakiuka haki za binadam??? Wakati mwingine unanivunjaga mbavu sana kwa post zako za ki comedy comedy kwenye mhimu yanayogusa maisha ya mtanzania!!!! Punguza njaaa ndugu
 
Dada yangu,

Naweza nikasema ukimya wa serikali ni kwa lengo jema tu!

Kwa maana gani; unajua hapa nchini chanzo kikubwa cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi (ukiachilia mbali shinikizo la US kwa hayati mwl Nyerere) ni kupanua wigo wa demokrasia.

Katika azma hiyo ya kupanua wigo wa demokrasia, sio vyema kufuta vyama vya siasa hata kama vinafanya vitendo nilivyo orodhesha hapo awali.

Bali njia pekee ni kuvilea vyama hivyo vinavyo fanya huo uovu kwa lengo la kuviimarisha zaidi ili viweze kufanya siasa zilizo komaa na za kistaarabu.

Aidha, kwa wale wote watakao bainika kufanya vitendo vya kuhatarisha usalama wa nchi hasa katika uharibifu wa makusudi wa amani na utulivu, hao watachukuliwa hatua kali za kisheria, hapa nadhani umeona jinsi Lwakatare na Kileo wanavyo kabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Eti waachwe hata wanakiuka haki za binadam??? Wakati mwingine unanivunjaga mbavu sana kwa post zako za ki comedy comedy kwenye maswala mhimu yanayogusa maisha ya mtanzania!!!! Punguza njaaa ndugu
 
Hili swali mbona liko wazi sana?

Bila ya CHADEMA kuleta tabia yao ya maandamano, kukaidi maagizo ya vyombo vya dola na ugaidi sidhani kama raia wa Tanzania wangeuawa na polisi.

Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na sio matakwa ya CHADEMA!
Katika matukio yote kwani kaua? Sio Chadema wala CCM bali serikali! Ndiyo yenye dhamana ya kuwahakikishia raia usalama wao na malizao! Kama isingekuwa Polisi kutumiwa kisiasa na CCM haya yote yasingetokea! Wa kulaumiwa ni serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom