Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,863
- 3,190
Kuhusu mahojiano yayaliyofanyika kati ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula na Gazeti la UHURU mimi najikita kwenye dhima ya Mahojiano hasa ya maoni Mzee Mangula kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na sababu sa Gazeti la uhuru kuuliza Mangula na ufafanuzi wangu.
Pengine Gazeti la uhuru bado halijaamua kunadi kazi za Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na kutafuta madhaifu kuliko mafanikio.
Pengine Gazeti la uhuru haliko pamoja na Mh. Rais na Mwenyekiti wa CCM kwa maana linaona udhaifu katika ujenzi wa bandari ya bagamoyo labda na mambo mengine.
Pengine Gazeti la uhuru limenusa kuwa Mzee Mangula hakubaliana na ujenzi wa bandari ya bagamoyo.
Kipimo cha maoni
Rais Samia amefufua mchakato wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Ni mchakato sio ujenzi, bado hakuna mikataba wala makubaliano ya moja kwa moja hivyo kwa namna moja Mzee Mangula yuko SAHIHI kusema "bagamoyo wanajenga gati" na sio bandari.
Utata unakuja ambapo Rais Samia alikaririwa kuwa Serikali yake inaona nia ya kufufua mchakato wa ujenzi wa bandari. Nazani kwa busara Mzee Mangula hakutakiwa kukanusha kuwa CCM au Serikali haina mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo sababu kuu umesikia Rais akisema sana.
Nadhani alitakiwa kusema serikali inaangalia mambo ya msingi yenye manufaa kwa wananchi katika ujenzi wa bandari hiyo. Hii ingekuwa kauli ya kiongozi tena Makamu Mwenyekiti wa CCM.
Nikiangalia uhalali wa kauli ya Mzee Mangula napata utata kutokana na rekodi za huko nyuma kwa kuwa hajawahi kupinga uanzishwaji wa miradi iliyofanywa na Marais waliopita mfano Rais Magufuli iliyokuwa nje ya ilani.
Sasa narudi kwenye gazeti je nia ya kuhoji ujenzi wa bandari ni kukusaidia chama na Mwenyekiti wake au kudhoofisha?, Kama matarajio yalikua kusaidia je katika kauli zote ni hii tuu ilipasewa kupewa kipaumbele.
Swali jingine je Gazeti la uhuru linamchongea Mzee Mangula kwa Rais Samia?
Majumuisho yananiambia ni kwa namba yoyote ile Gazeti la uhuru limefanya kosa la kiufundi hasa kutokupima athari za kuchapisha maoni hayo. Kimsingi Gazeti la uhuru limehusika kudhoofisha jina, sifa, imani na uungwaji mkono wa Rais Samia katika mipango yake.
Nimalizie kuwa bado Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM anayo haki ya kufanya jambo lolote jema kwa watanzania. Na cha zaidi Rais Samia anafanya kwa uwazi na kushirikiana wananchi kitu ambacho huko nyuma hatukukiona.
Nimalizie kwa swali
Je, maoni ya mzee Mangula ni mwisho kwa busara zake?
Je, Gazeti la uhuru wana jambo lao dhidi ya Mh. Rais?
Rais Samia
#KAZI IENDELEE