Nani alaumiwe, Mzee Mangula au Gazeti la Uhuru au wote au kinyume chake tuwapongeze?

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Kuhusu mahojiano yayaliyofanyika kati ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula na Gazeti la UHURU mimi najikita kwenye dhima ya Mahojiano hasa ya maoni Mzee Mangula kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na sababu sa Gazeti la uhuru kuuliza Mangula na ufafanuzi wangu.

Pengine Gazeti la uhuru bado halijaamua kunadi kazi za Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na kutafuta madhaifu kuliko mafanikio.

Pengine Gazeti la uhuru haliko pamoja na Mh. Rais na Mwenyekiti wa CCM kwa maana linaona udhaifu katika ujenzi wa bandari ya bagamoyo labda na mambo mengine.

Pengine Gazeti la uhuru limenusa kuwa Mzee Mangula hakubaliana na ujenzi wa bandari ya bagamoyo.

Kipimo cha maoni
Rais Samia amefufua mchakato wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Ni mchakato sio ujenzi, bado hakuna mikataba wala makubaliano ya moja kwa moja hivyo kwa namna moja Mzee Mangula yuko SAHIHI kusema "bagamoyo wanajenga gati" na sio bandari.

Utata unakuja ambapo Rais Samia alikaririwa kuwa Serikali yake inaona nia ya kufufua mchakato wa ujenzi wa bandari. Nazani kwa busara Mzee Mangula hakutakiwa kukanusha kuwa CCM au Serikali haina mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo sababu kuu umesikia Rais akisema sana.

Nadhani alitakiwa kusema serikali inaangalia mambo ya msingi yenye manufaa kwa wananchi katika ujenzi wa bandari hiyo. Hii ingekuwa kauli ya kiongozi tena Makamu Mwenyekiti wa CCM.

Nikiangalia uhalali wa kauli ya Mzee Mangula napata utata kutokana na rekodi za huko nyuma kwa kuwa hajawahi kupinga uanzishwaji wa miradi iliyofanywa na Marais waliopita mfano Rais Magufuli iliyokuwa nje ya ilani.

Sasa narudi kwenye gazeti je nia ya kuhoji ujenzi wa bandari ni kukusaidia chama na Mwenyekiti wake au kudhoofisha?, Kama matarajio yalikua kusaidia je katika kauli zote ni hii tuu ilipasewa kupewa kipaumbele.

Swali jingine je Gazeti la uhuru linamchongea Mzee Mangula kwa Rais Samia?

Majumuisho yananiambia ni kwa namba yoyote ile Gazeti la uhuru limefanya kosa la kiufundi hasa kutokupima athari za kuchapisha maoni hayo. Kimsingi Gazeti la uhuru limehusika kudhoofisha jina, sifa, imani na uungwaji mkono wa Rais Samia katika mipango yake.

Nimalizie kuwa bado Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM anayo haki ya kufanya jambo lolote jema kwa watanzania. Na cha zaidi Rais Samia anafanya kwa uwazi na kushirikiana wananchi kitu ambacho huko nyuma hatukukiona.

Nimalizie kwa swali
Je, maoni ya mzee Mangula ni mwisho kwa busara zake?
Je, Gazeti la uhuru wana jambo lao dhidi ya Mh. Rais?
Rais Samia
#KAZI IENDELEE
 
Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
486
1,000
Ndio hapo utajua kuwa kuna wazee, vichwa na wanajaribu kuonyesha kuwa wapo, hayupo peke yake huyo.

Pili, mama hakuna lolote zito alilofanya katika chama kuwa na ushawishi huko, huenda kikatiba akapata cheo lakini ndani ya chama akashindwa kuwa na ushawishi kubalance, ukiona kina Polepole wakiongea ujue nyuma yao wapo watu na wanaojiamini wana mizizi ndani ya chama.

Ndiposa watamshika shati kama wanatofautiana nae, hii inatokeaga kwa majirani zetu,
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Ndio hapo utajua kuwa kuna wazee, vichwa na wanajaribu kuonyesha kuwa wapo, hayupo peke yake huyo.
Pili, mama hakuna lolote zito alilofanya katika chama kuwa na ushawishi huko, huenda kikatiba akapata cheo lakini ndani ya chama akashindwa kuwa na ushawishi kubalance, ukiona kina Polepole wakiongea ujue nyuma yao wapo watu na wanaojiamini wana mizizi ndani ya chama,
Ndiposa watamshika shati kama wanatofautiana nae, hii inatokeaga kwa majirani zetu,
Unataka kumaanisha Mzee Mangula anaweza kumu overpower mwenyekiti wake?
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,341
2,000
Mbuzi wa Bwana heri shamba la bwana Heri, waache waendelee na mambo yao wala hakuna wakuwaingilia maana wana dola wana wasiojulikana wana mahakama na magereza pia , wafanye watakalo.Nchi ina mambo ya ajabu sana hii kilichokua haramu wakati wa jamaa sasa ni halali
 
Nov 23, 2021
94
150
Mzee Mangula hana chembe ya unafiki,bandari hiyo imegubikwa na sintofahamu,sasa ulitaka aunge mkono uharamia? Kisa ni CCM?,
CCM wanachama wake ni kwamba watasema kweli daima.

Sasa niolozeshee miradi yote aliyoifanya Magufuli ambayo haipo kwenye Ilani ili twende sawa.

Ninachofahamu Magufuli aliitekeleza ilani ya CCM kwa speed ya 5G.
 
wababayangu

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
325
500
Unataka kumaanisha Mzee Mangula anaweza kumu overpower mwenyekiti wake?
Mkuu pamoja na kwamba JPM ni marehemu lakini bado anao ushawishi mkubwa sana kwa wananchi zaidi ya mama. Hivyo hakuna ubishi kwamba mzee Mangula anayo nguvu kubwa sana ndani ya chama zaidi ya mama.

Huu ni ushawishi wa JPM unaoishi
1. Kauli ya kwamba mikataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni wa kinyonyaji. Hii kauli bado inaishi katika vichwa vya watanzania

2. Chanjo ya covid19 JPM hakukubaliana kabisa na chanjo hiyo. Nadhani unaona matokeo ya kukubalika kwa chanjo hiyo.

3. Uhuru wa machinga kupanga bidhaa zao mahali popote wapendapo. Hii haikuwa sahihi kabisa. Lakini mama alivyokubali wamachinga kuhamishwa, wananchi wanaona wanaonewa kwa sababu JPM amefariki.

4. Soma katika mitandao ikitokea katika hotuba ya mama akakosoa utendaji kazi wa JPM atatukanwa matusi yote unayoyajua
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Hata wewe umeandika kwa kumtetea zaidi Raisi. Mangura ndiye mwenye chama na nchi pia. Hivyo hazuiwi na mtu yeyote kutoa maoni yake. Mangura yuko sahihi 100%
Chama Cha CCM kinamilikiwa na Mangula
Kwaio mwenyekiti hana chake
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Mkuu pamoja na kwamba JPM ni marehemu lakini bado anao ushawishi mkubwa sana kwa wananchi zaidi ya mama. Hivyo hakuna ubishi kwamba mzee Mangula anayo nguvu kubwa sana ndani ya chama zaidi ya mama.

Huu ni ushawishi wa JPM unaoishi
1. Kauli ya kwamba mikataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni wa kinyonyaji. Hii kauli bado inaishi katika vichwa vya watanzania

2. Chanjo ya covid19 JPM hakukubaliana kabisa na chanjo hiyo. Nadhani unaona matokeo ya kukubalika kwa chanjo hiyo.

3. Uhuru wa machinga kupanga bidhaa zao mahali popote wapendapo. Hii haikuwa sahihi kabisa. Lakini mama alivyokubali wamachinga kuhamishwa, wananchi wanaona wanaonewa kwa sababu JPM amefariki.

4. Soma katika mitandao ikitokea katika hotuba ya mama akakosoa utendaji kazi wa JPM atatukanwa matusi yote unayoyajua
Mkataba wa Bagamoyo bado haujasainiwa zaidi Rais amefufua mchakato
 
Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,066
2,000
Uzito wa uzoefu na mizizi ndani ya chama ndio inayoleta ushawishi, hasa pale mnapokuwa sio kitu kimoja tena basi mwenye ushawishi zaidi ataonekana hata kwa chinichini bila kuvuruga hali ya hewa.
Nafasi ya Mzee Mangula inatolewa na nani?
 
RAISI AJAYE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,812
2,000
Ajenda ya mama kugombea uraisi 2025 ni ajenda ya zanzibar tena kwa msaada wa mwenyekiti wa ccm Bwana Shein!!!Sio ajenda ya Bara wala ya Deep state!!!Gazeti la uhuru linatuonyesha wazi kabisa Mwisho wa mama kuwa Raisi ni 2025!!Tusubiri!!!
 
Ametamka kuwa atagombea
 
50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
3,156
2,000
Mzee Mangula hana chembe ya unafiki,bandari hiyo imegubikwa na sintofahamu,sasa ulitaka aunge mkono uharamia?,kisa ni CCM?,
CCM wanachama wake ni kwamba watasema kweli daima.

Sasa niolozeshee miradi yote aliyoifanya Magufuli ambayo haipo kwenye Ilani ili twende sawa.
Ninachofahamu Magufuli aliitekeleza Ilani ya ccm kwa speed ya 5G,
NAKAZIA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom