Nani alaumiwe?Anko?,au demu?Naitaji ushauri

Pole ndugu! Kwa hali ya kawaida si rahisi mwanaume akulie vyako halafu yeye ndo aje kukwambia. Uncle kama kafanya ivo ujue kakudharau sana na anataka kumgeuza demu wake so anakuvuruga umpige chini waendelee kwa raha zao. Cha msingi nawe tafuta mdogo wake au ndugu wake karibu upige halafu nawe ukamwambie

mdogo mtu ni mamdogo, sasa ndugu,dah!!.. Alisemalo mtu ndilo aliwazalo na kulitenda. Ko we huwa unapiga mashine mdogo wa mama yako?
 
Anko kazaliwa1980
Mimi nimezaliwa 1984
DEmu kazaliwa 1991

mtu mzima namna hii unashindwa hatua za kuchukua? Mi nilidhani ni vile vitoto vilivyoshuka verse necta! Mkuu umeniangusha sana japokuwa mapenzi hayana formula. Unatufanya tuliozaliwa 80s fikra zetu zionekane fupi.
 
Nina msichana wangu fulani ametembea na anko wangu tena amemwambia iwe siri sasa anko kaniambia,je nimlaumu nani?.

Tatizo mbona silioni. Wewe unatembea na wanawake wagapi barabarani naye halalamiki. Halafu huyo ni msichana tu sio mchumba, rafiki wa kike nk. Huo ni wivu wa kijinga: kulionea wivu poozeo. Jilaumu mwenyewe kwa kupenda mapoozeo.

Bazazi ni Bazazi!
 
we usimlaumu mtu we mwache anza mbele watoto wa tisin ndo zao hzo lol...pole
 
Wote wanamakosa lakini kua muungwana wala usilipize mdharau tuu huyo Uncle wako, na huyo mwanamke malizana nae pia.
 
Kwani mmeoana?

Hakuna wa kulaumiwa, wewe umerithi uzinzi kwa anko wako na machezo yako yalikuwa hafifu, binti kaamuwa aonje kwa anko, kanogewa.

Wote nyie wazinifu hamna mwenye afadhali, si wewe, si anko, si binti.

:biggrin1:
 
Nina msichana wangu fulani ametembea na anko wangu tena amemwambia iwe siri sasa anko kaniambia,je nimlaumu nani?.

HUYO SIO MSICHANA WAKO, NI MSICHANA WA WOTE (MALAYA). Msichana anaye jiheshimu hachangani mabwana. MULIKA MWIZI KABLA HUJA AMBUKIZWA VVU.
 
Nina msichana wangu fulani ametembea na anko wangu tena amemwambia iwe siri sasa anko kaniambia,je nimlaumu nani?.

Wote wana makosa na wanapaswa kulaumiwa. Anko wako anapaswa kulaumiwa kwa kutembea na mpenzi wako huku akijua kuwa nyie mu wapenzi na huyo mpenzi wako pia naye anapaswa kulaumiwa kwanza kwa kumkubali anko wako wakati akijua kuwa wewe na anko wako ni ndugu lakini pia ili hali akijua kuwa nyie bado ni wapenzi. Kitendo cha kishetani, cha laana ambacho kinastahili adhabu kali.

Badala ya kuumia unapaswa kumshukuru Mungu kwa kukuonyesha tabia ya huyo msichana wako kabla hata hamjafunga ndoa huweiz jua pengine yangaeweza kuja kutokea makubwa zaidi hapo baadae ambayo yangeuvunja moyo wako. Mfano: hivi ungejisikiaje kama ungekuja kuambiwa kuwa huyo mpenzi ambaye kwa wakati huo ni mke wako ametembea na baba yako, kaka yako, mdogo wako, au pengine hata mtoto wako mwenyewe?

Kuna dosari ndogo ndogo katika tabia ya mtu ambazo zinaweza kuvumilika na kurekebishika lakini ukishaona tabia za ajabu ajabu kama hizo ujue hiyo ni taa nyekundu unawashiwa na unapaswa ukimbie mapema sana.

Ndoa si swala la kufanyiwa mzaha au majaribio. Once decide to do it, there is no turning back. Think about it kaka na uamue mapema before its too late.
 
Back
Top Bottom