Nani aijuaye kesho?

Nani aijuaye kesho?

Two dimension array

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,592
Reaction score
2,381
Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.

Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.

*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo. Rais wa zamani wa Zimbabwe *Robert Mugabe aliwahi kusema "heshimu kila mtu kama unavyoheshimu taulo lako. Kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio leo, kesho unaweza kuitumia kufutia uso."*

Hakuna chochote kwenye maisha yetu kinachodumu milele. Pia kumbuka hakuna tunu ya kujali wengine inayopotea bure. Jukumu la msingi la uhai tuliopewa na Mungu ni kusaidia wengine. Kwahiyo kama MUNGU amekujalia uwezo wa kifedha, au madaraka vitumie kusaidia wengine.

Na kama huwezi kuwasaidia basi usitumie cheo chako, pesa zako au madaraka yako kuwaumiza. Mahatma Ghandi aliwahi kusema kama huwezi kuwasaidia wengine basi angalau usiwaumize (If you cant help them, atleast do not hurt them).
 
Hakika anayejua ya kesho ni Mungu, amini usiamini kiumbe wake ni wiki ya tatu sasa sina ata shilingi Mungu ananilisha kama ndege wa porini ila naishi bila kujua kesho itakuwaje.

Ila nina matumaini makubwa haya nayo yatapita tu, sijaomba msaada wowote kwa ndugu. HAKIKA MUNGU ANAWEZA AISEI.
 
NAMKUMBUKA MAMA MWENYE NYUMBA ILE YAKWANZA NAANZA KUJITEGEMEA...NILIISHIWA NIKAUZA KILA KITU ILI NIPATE MTAJI....NIKAKOSA KOD NA AKASHINDWA HATA KUNIPA MAHAL PAKUWEKA UBAV....NIKAONGEA NA MSHIKAJ CHUMBA CHA JIRAN AKAKUBAL NILALE KWAKE MANA ALIKUWA SINGLE...BAADA YA MAMA MWENYE NYUMBA KUGUNDUA NAKAA NA MSHIKAJ AKATAKA KUMPA NOTS SO NIKAONA NISIMKWAZE JAMAA JAPO ALIKUBAL KIROHO SAF....NIKASEPA NAULI YAKURUD MOSHI SINA NA PAKULALA SINA NA SINA RAFIKI MANA NILIKUWA MWANAFUNZI.....NKAWA NALALA MSIKITIN MPAKA CHANEL ZILIPOSOMA.....NOW MWANAYE ANATAKA SHAVU NIMPE PIKIPIK AZUNGUSHE (MKATABA).......ILA NAMSHUKURU MAMA MWENYE NYUMBA MANA NINGEENDELEA KUBWETEKA NA CHANEL PENGINE ZINGEGEUKA.....ALHAMDULILLAH KWEL USIMDHARAU MTU COZ HUIJUI KESHO YAKE
 
sasa kabila alikosaje nauli?
Wakati familia ya baba Joseph ilipohamia Dar es Salaam Tanzania, Joseph Kabila alipelekwa kujiunga na shule ya msingi na ya sekondari katika Daressalaamna Mbeya. Na inasemekana wakati ule alitumua jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu za usalama.
Sasa jibu la swali lako ni, tukio hilo la kushushiwa porini huko Mkoani Iringa.... Lilimtokea wakati alipokua akisafiri kati ya Dar na Mbeya.
 
Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.

Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.

*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo. Rais wa zamani wa Zimbabwe *Robert Mugabe aliwahi kusema "heshimu kila mtu kama unavyoheshimu taulo lako. Kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio leo, kesho unaweza kuitumia kufutia uso."*

Hakuna chochote kwenye maisha yetu kinachodumu milele. Pia kumbuka hakuna tunu ya kujali wengine inayopotea bure. Jukumu la msingi la uhai tuliopewa na Mungu ni kusaidia wengine. Kwahiyo kama MUNGU amekujalia uwezo wa kifedha, au madaraka vitumie kusaidia wengine.

Na kama huwezi kuwasaidia basi usitumie cheo chako, pesa zako au madaraka yako kuwaumiza. Mahatma Ghandi aliwahi kusema kama huwezi kuwasaidia wengine basi angalau usiwaumize (If you cant help them, atleast do not hurt them).
Kwel kbsa
 
Mnataka kusema wote humu hamuijui kesho?au mnatania

KESHO NI JUMANNE !!!!

anaeweza kupinga
IMG_20180814_004347_022.jpg
 
Usimdharau mtu yeyote asilani na wala usitumie cheo chako vibaya
Nalog off
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom