Nani aijuaye kesho?

Nani aijuaye kesho?

kweli.....

maisha yana siri kubwa ....
inafikia wakati mtu unakata tamaa.... maana kila unavyojitahidi wapi ...na hapo inakuwa huna saidizi yoyote....nikikumbuka.....wakati mwengine hutoka machozi!
na wanakuja kukuvuta Toka kule bondeni ni watu ambao hukuwaza wala kufikiri na huwajui!
Bado namkumbuka mtu aliyenipa nauli ... na aliyenisaidia nikatoroka......
Mungu awape baraka huko waliko..maana siwajui tena ingawa nilijaribu kuwatafuta lkn sikufanikiwa.... sina maisha mazuri ila sio mabaya kama ningelibaki kule walikonisaidia kutoka!
Nimepata somo kubwa maishani! na najitahidi kusaidia pale ninapo weza.
 
Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.

Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.

*Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho*. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo. Rais wa zamani wa Zimbabwe *Robert Mugabe aliwahi kusema "heshimu kila mtu kama unavyoheshimu taulo lako. Kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio leo, kesho unaweza kuitumia kufutia uso."*

Hakuna chochote kwenye maisha yetu kinachodumu milele. Pia kumbuka hakuna tunu ya kujali wengine inayopotea bure. Jukumu la msingi la uhai tuliopewa na Mungu ni kusaidia wengine. Kwahiyo kama MUNGU amekujalia uwezo wa kifedha, au madaraka vitumie kusaidia wengine.

Na kama huwezi kuwasaidia basi usitumie cheo chako, pesa zako au madaraka yako kuwaumiza. Mahatma Ghandi aliwahi kusema kama huwezi kuwasaidia wengine basi angalau usiwaumize (If you cant help them, atleast do not hurt them).
Huo ni ukweli wa maisha ya kila binadamu! Binadamu yeyote anayejitambua na aliye na akili timamu anapaswa kutambua ukweli huo.

Kila kitu juu ya uso wa dunia hubadilika kulingana na muda!!! Hakuna kitu chochote kinachosalia vile vile siku zote.
 
Hakika anayejua ya kesho ni Mungu, amini usiamini kiumbe wake ni wiki ya tatu sasa sina ata shilingi Mungu ananilisha kama ndege wa porini ila naishi bila kujua kesho itakuwaje.

Ila nina matumaini makubwa haya nayo yatapita tu, sijaomba msaada wowote kwa ndugu. HAKIKA MUNGU ANAWEZA AISEI.
Data unapata wapi mkuu..
 
Haya maneno ni ya hekima sana. Unapopanda juu usiwasahau waliopo chini, kwani siku utakapoporomoka utawakuta wapo hapo kukupokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom