Wanajukwaa nawasalimu. Napenda kufahamu kwa waliokwenda nanenane morogoro kukoje??? Maana nami nataka nijongee huko jumapili nishinde pamoja na jumatatu
Hivi haya maonesho ya nanenane ..kuna kituo chochote hapa maeneo ya Dar au Pwani?
Subili serikali ikihamia Dodoma tutahamisha yale ya Dodoma tutaleta Dar es Salaam
Kwa sasa sabasaba inawatosha
Hardman, dar hakuna ndio maana Yale ya morogoro alikwenda PM, RC's wa dar, pwani na tanga
Mkuu Leo najiandaa nipande basi pale ubungo ni fike huko kuongeza maarifaNane nane Morogoro ipo vizuri mimi nilipata bahati yakwenda kwakweli nimejifunza mengi sana na nimekutana na wakulima na wafugaji mbalimbali pia makampuni ya mbegu na madawa.
Pia nilikutana na watu wa kampuni ya A to Z nimekuta wanaproduct yao AgroZ Net ambayo ni chandarua maalum kama green house ina ukubwa wa 30 X 5.5mt inauzwa kwa 250,000/= . kwasisi ambao tulikuwa hatuna uwezo wa green house hii ni mkombozi wetu.
Jambo la pili ni haya maonyesho yamegawanyika katika kanda kwa kanda ya mashariki kuna mikoa ya Pwani, D.S.M na Morogoro yanafanyika Moerogoro, kanda ya Kusini yamefanyika kwa pamoja Lindi na Mtwara. Kanda ya Kati yanafanyika Dodoma nk.
Ukipata nafasi nenda ndugu.
Du karibu sana huku mambo mazuri uwanja umefurika kwa kweli pako vizuri japo mwanzo kulukuwa kumepoa ila siku hz mbili pamechangamka sanaWanajukwaa nawasalimu. Napenda kufahamu kwa waliokwenda nanenane morogoro kukoje??? Maana nami nataka nijongee huko jumapili nishinde pamoja na jumatatu
mkuu hawa ATO Z wanapatikana wapi nimependa idea ya hicho chandaruaNane nane Morogoro ipo vizuri mimi nilipata bahati yakwenda kwakweli nimejifunza mengi sana na nimekutana na wakulima na wafugaji mbalimbali pia makampuni ya mbegu na madawa.
Pia nilikutana na watu wa kampuni ya A to Z nimekuta wanaproduct yao AgroZ Net ambayo ni chandarua maalum kama green house ina ukubwa wa 30 X 5.5mt inauzwa kwa 250,000/= . kwasisi ambao tulikuwa hatuna uwezo wa green house hii ni mkombozi wetu.
Jambo la pili ni haya maonyesho yamegawanyika katika kanda kwa kanda ya mashariki kuna mikoa ya Pwani, D.S.M na Morogoro yanafanyika Moerogoro, kanda ya Kusini yamefanyika kwa pamoja Lindi na Mtwara. Kanda ya Kati yanafanyika Dodoma nk.
Ukipata nafasi nenda ndugu.
nimelima heka 2 so nahitaji kuuzia shambani bt sijui pa kuanzia.Unauza mwenyewe mtaani mkuu..
Ni aina gani na una uzaje?nimelima heka 2 so nahitaji kuuzia shambani bt sijui pa kuanzia.