Ni shauri zuri Mkuu. Kwa mama mkwe namna hii dawa si kuondoka, kwani mke akiondoka atakuwa amemrahisishia kazi ya kutimiza malengo yake. Hata mumewe akirudi, mama mkwe atabakia hapo na mume hana kauli kwa mama yake. La kufanya hapo ni kumfanyia maisha ayaone magumu, awe yeye wa kuondoka. Wala si kwa njia ya kumtukana bali kusimama naye kimo kimoja, akimwaga mboga anamwaga ugali.Kwa haraka na kutumia maelezo yako..huyu mama ana mapepo yanamsumbua... na kijana wake amekosa sifa za kuitwa Baba wa nyumba..hivyo usimtegemee kama ataweza kutatua hizo issues...
Kikubwa ujue wewe ndiye mwenye mji..inabidi umuheshimu mama lakini siyo kwa nidhamu ya woga..Kupeana ukweli, kwa lugha ya heshima ni njia sahihi..
Lakini kabla ya yote lazima umwonyeshe mama kuwa hata wewe unao wazazi..kama wazazi wako wako hai waite waje (kwa gharama yeyote) na itakuwa vizuri ukaongea yote "black and white" mbele ya wazazi wako na huyo mama..bila kuogopa what is next... Najua wazazi wako hawatavumilia lugha mbaya kama huyo mama ataanza..na hivyo itakusidia wewe kukaa kimya na remote control kikao..
All in all, lazima ufanye kitu ASAP... binafsi sikushauri kukimbia nyumba kwa sababu ya mtu mmoja mwenye mapepo yanayomsumbua..Wewe hapo ni kwako na mama ni mgeni..Apewe heshima zake lakini sio kwa woga.. kama vidonge apewe..anywe, apone mapepo!
FL1...uko sahihi kabisa hii pia inaweza kuwa njia sahihi, nyie wawili tu, sababu kama kukiwa na mtu wa tatu, kwa aiubu ataleta ubishi na hatakubali kukusikiliza. Mtafutie siku , wawili tu. Unaweza kumfuata chumbani ukafunga mlango na kumwambia akueleze tatizo ni nini, Openly mwambie umechoka na mambo yake, anakukera, na kuwa hapo ni kwako hautaondoka. Jamaa mekuzimia na yeye hana jinsi ya kuibadilisha hiyo.....in short mpe Mkwara wa nguvu lakini uliojaa facts tupu!
Mimi ni mwanafunzi so siijui ndoa sasa ushauri wangu usijaribu kukimbia nyumba yako hata siku 1, piga mkwara mzito, then mtupie vilago vyake nje heri lawama kuliko fedhea.
Una visa wewe!!
<br />Saa nyingine hata nyie wake zetu mna matatizo bana, hivyo mi sikuamini 100% kwamba mama mkwe ndo mbaya. Jitoe kwanza boriti jichoni mwako.