Jinsi binti wa kichina alivyomuua mama mkwe wake

Princess21

JF-Expert Member
Oct 15, 2015
272
266
Miaka kadhaa huko Uchina, Binti aitwaye Li-Li aliolewa na akaenda kuishi kwao mumewe na mama wa mumewe.

Ndani ya muda mfupi Li-Li alijikuta hana maelewano kabisa na mama Mkwe wake. Tabia zao zilikuwa tofauti kabisa, walipishana kauli kila mara na Li-Li alichukizwa sana na tabia nyingi za mama mkwe wake. Mbaya zaidi, mama-mkwe alimlaumu na kumsema vibaya Li-Li mara zote.

Kadri ya siku na wiki zilivyopita, Li-Li na mamamkwe wake walizidi kubishana na kugombana. Kilichofanya hali kuwa ngumu sana ni mila kuwa Li-Li alitakiwa kumnyenyekea na kutimiza kila alichohitaji.Ugomvi na kukosekana amani ndani ya nyumba vilimsababishia mfadhaiko na kumyima amani mume wa Li-Li kwani aliwapenda wrote.Baada ya kushindwa kumvumilia mama Mkwe wake ambaye alinung'unika kila mara na kutaka kuwa ndiye anayefanya maamuzi yote ndani ya nyumba, Li-Li aliamua kwenda kwa rafiki wa baba yake,Huang, ambaye alikuwa anauza Dawa za mitishamba.

Alimuelezea hali ilivyo na akamuomba kama anaweza kumpa Dawa yenye sumu ili aweze kutatua tatizo mara moja na lisijirudie tena.Huang, alifikiria kwa muda na mwishowe akamwambia, "Li-Li, nitakusaidia kutatua tatizo lako. Lakini lazima unisikilize na utekeleze masharti nitakayokuambia"Li-Li akasema, "Ndiyo, Huang, nitafanya chochote utakachoniambia'. Huang akazunguka nyuma ya chumba na akarejea dakika chache baadae akiwa na kifurushi cha mitishamba.

Akamwambia Li-Li, "Huwezi kutumia sumu itakayo muua haraka mama mkwe wako kwa maana itasababisha watu wakuhise kuwa wewe ndiyo umemuua.Hivyo nakupa sumu itakayojengeka mwilini mwake taratibu na kumuua baada ya muda mrefu. Sharti ni kuwa kila siku muandalie chakula kitamu anachokipenda na changanya kiasi kidogo cha Dawa hii.

Ili kuhakikisha hakuna anayekuhisi atakapokufa, lazima uwe makini na kuwa naye karibu na kuwa rafiki yake kuanzia sasa. Usibishane wala kugombana naye, kila anachoomba mtekeleze na mjali na kumthamini kama malkia. Li-Li alfurahi sana maana sasa alijua tatizo lake limekwisha.

Alimshukuru Huang na akaenda mbio nyumbani na kuanza mkakati wake wa kumuua mama mkwe wake.Wiki na miezi ilipita na kila siku Li-Li alimpikia mama Mkwe wake chakula maalumu anachokipenda.

Alikumbuka masharti ya Huang kuwa aepuke kugombana naye au kumsema vibaya, hivyo akajifunza kuzuia hasira zake, akatii maagizo na kumjali mama mkwe wake kama mama yake wa kumzaa.

Baada ya miezi sita, maisha ndani ya nyumba yalibadilika sana.Li-Li alikuwa amemudu kudhibiti hasira zake kiasi kwamba hakuna siku aliyokasirika wala kujisikia vibaya. Hakuwa amegombana na mama mkwe wake kwa miezi 6 maana mama Mkwe wake sasa alionekana mpole, mwenye moyo safi na rahisi kuelewana naye.

Tabia ya manunguniko na lawama za mama Mkwe kwa Li-Li pia ziliisha, na mama huyu alianza kumpenda Li-Li kama mwanaye wa kumzaa. Mama huyu alianza kuwaeleza ndugu na marafiki zake jinsi ambavyo Li-Li ni mkamwana bora ambaye siyo rahisi kupata mkamwana kama huyu.Li-Li na mamamkwe wake wakaanza kuishi kama Binti na mama yake halisi wa kumzaa.
Mume Wa Li-Li alijawa na furaha kuona kinachoendelea.

Siku moja Li-Li akarudi kwa Huang kuomba msaada wake tena. Akasema, "Huang,tafadhali naomba unisaidie sumu isimuue mama yangu. Amebadilika sana na sasa ni mama mzuri sana, nampenda kama mama yangu wa kunizaa. Sitaki afe kwa sababu kwamba nimempa sumu"
Huang alitabasamu na kutikisa kichwa.

Akasema, "Li-Li, usihofu chochote. Dawa niliyokupa haikuwa sumu. Ilikuwa ni vitamini za kuboresha Afya.Sumu pekee ya kuharibu uhusiano wenu ilikuwa ndani ya fikra zako kwa jinsi uliyokuwa unamtendea mama Mkwe wako vibaya, lakini sasa sumu hiyo imesafishwa kwa upendo mkubwa uliomwonyesha mama huyu"

CHA KUJIFUNZA:

Umewahi kufikiria kwamba jinsi unavyowatendea wenzako ndivyo hivyo hivyo wanavyokutendea? Ukiwasengenya watakusengenya pia, ukiwasema vibaya watakusema vibaya pia, ukiwachukia wanakuchukia pia.Pana Msemo wa Kichina unasema, "MTU yeyote anayewapenda wengine, naye atapendwa pia" Mungu anaweza kuwa anatenda katika maisha ya wengine kwa kukutumia wewe.Tuma ujumbe huu kwa wengine na usambaze nguvu ya upendo katika maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom