Namuonea huruma huyu binti

Boss hali hiyo hata mimi iliwahi kunipitia,kuna nyimbo inaitwa IF YOU LOVE ME LEAVE ME..watu tumeachana sio kwasababu hatupendi,sababu tumependa..huo ndio uanaume,.ila unachopaswa kufanya mwambie ukweli wote..
 
Najua lazima nitajuta na nishajiandaa kisaikolojia lakini iyo ni kwa upande wangu vipi kuhusu yeye mkuu, huoni kama nampotezea muda
Kwani yeye kasema unampotezea muda?? Kwann uanze kubashiri, kaa nae muambie hali halisi kama hauko vizuri kiuchumi, kama anaona hatoweza kuwa mvumilivu anaweza kubali wanaume wengine.

Laikin sio umuache kwa kuhisi wampotezea muda, usikute mwenyewe ana enjoy hiyo hali
 
Nipe namba yake
 
Mtaji, uzoefu kibiashara na changamoto ya kiafya( nina shida kidogo ya kusikia vizuri) vinanikwamisha kwenye suala la kujiajiri, ingawa nishafight mara kadhaa nikafeli
Kusikia vizuri sio tatizo na wewe. Kuna vifaa vingi vya kusaidia kusikia vizuri, unaagiza hata kwa 30,000 vipo safi kabisa unafanya biashara. Biashara inategemea na sehem unakoishi, angalia changamoto zilizopo then work on them. Usidanganywe na motivation speakers
 
Mkuu ilo tatizo ni jambo pana kidogo sio rahisi kama unavyofikiria. Mpaka nikaamua sasa nitulie nikubali ndo mtihani wangu hapa duniani ujue nishaenda mpaka hospital kubwa kama CCBRT. Kwa hali yangu niliambiwa nikitumia ivyo vifaa ndio naongeza ukubwa wa tatizo. Hata ivyo shida sio kusikia tu kuna changamoto ya mtaji pia ukizingatia sijatokea kwenye familia ya mboga saba
 
ila sisi wanaume bana,

tusipopendwa tunalalamika, tukipendwa tunaanza kujiogopa

hatujui tunachokitaka

jiamini mkuu, huyo amekupenda jinsi ulivyo, ukimuacha utakuja kujuta

kakupenda pamoja na kufulia kwako, kapenda boga na ua lake....
Hii ni shida binafsi ya mleta mada. Amepigwa njaa mpaka amekua na inferiority complex. Imefika hatua anaamini hastahili kua na mwanamke mzuri!

Sisi wengine tunajua tunachokitaka!
 
Uchumi na upendo ni vitu viwili tofauti, anaekupenda atakuvumilia labda kama wewe unajua ukizipata utamuacha ndio maana unamuonea huruma vinginevyo hiyo huruma yako haina maana yeyote.
 
Hii ni shida binafsi ya mleta mada. Amepigwa njaa mpaka amekua na inferiority complex. Imefika hatua anaamini hastahili kua na mwanamke mzuri!

Sisi wengine tunajua tunachokitaka!
Changamoto za kimaisha zinaonekana nyepesi sana kama haujakutana nazo au una uwezo wa kuzimudu kwa wakati husika. Hata ivyo shukrani sana kwa mchango wako mkuu
 
Nipe mm mkuu.
 
Ni vitu viwili tofauti lakini vinategemeana mkuu. Ili mahusiano yawe imara uchumi una nafasi yake pia
Una nafasi yake sikatai ila kama mwanamke anaelewa hali yako na anakupenda wewe unapaswa kupambana kujiinua kiuchumi hali ikimshinda na akitaka kukimbizana na muda ataamua yeye mwenyewe na hatokuonea huruma.
 
Nyota yako ya mafanikio ipo kwake
Nakushauri mwoe utaona mambo yako yatakavyofunguka

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…