Namuanzaje mamamkwe-mrejesho

Mshukuru Mungu kakuonyesha udhaifu wa huyo mwanamke mapema na ukishamjua mbwa hakupi taabu!
 
Bado hakuna kitu cha kuprove hapo.
Suppose mama hakutaka ujue, unafikiri angesema nilimwambia 'Ester' achukue pesa kwenye account yako?

Kwanini hukumpa live mchumba wako kitu ulichoongea na mamamkwe, ingekuwa ngumu kutunga uongo wa haraka2.

Maybe, ni yeye alichukua hiyo pesa na akatumia kwa kitu ambacho wewe hukipendi au ulimkataza; so akaamua kusema uongo ili apunguze ugomvi, such a big deal!

Kaka mimi nafikiri, umuache tu huyo dada hakufai kabisa! Yaani katumia laki tano zako bila ruhusa wala maelezo ya maana! Si mwaminifu halafu ni mwizi na si ajabu ametumia kuhonga wanaume. Yaani ningekuwa mimi ningemuacha long time!
 
Kwanza pongezi kwa kutupa feedback. Hapo kweli pagumu kaka, jaribu kuvumilia kidogo labda ukirudi bongo utapata jua ukweli wa mambo sembuse mwanamama alitumia pesa kwa sababu za msingi kabisa thou sio vyema kwamba hakukuweka wazi. Ukijua A-Z ndo uamuzi ufanyike.
 
Bado hakuna kitu cha kuprove hapo.
Suppose mama hakutaka ujue, unafikiri angesema nilimwambia 'Ester' achukue pesa kwenye account yako?

Kwanini hukumpa live mchumba wako kitu ulichoongea na mamamkwe, ingekuwa ngumu kutunga uongo wa haraka2.

Maybe, ni yeye alichukua hiyo pesa na akatumia kwa kitu ambacho wewe hukipendi au ulimkataza; so akaamua kusema uongo ili apunguze ugomvi, such a big deal!

Kaka mimi nafikiri, umuache tu huyo dada hakufai kabisa! Yaani katumia laki tano zako bila ruhusa wala maelezo ya maana! Si mwaminifu halafu ni mwizi na si ajabu ametumia kuhonga wanaume. Yaani ningekuwa mimi ningemuacha long time!

Dadaangu Kaunga kumbuka kwanza niko mbali na yeye ndiye mwenye account yangu kwa sasa. Kwa hiyo kitendo chochote kitakachopelekea yeye kujua kwamba ninaujua ukweli kinaweza kunigharimu sana. Nimeona bora yeye aendelee kudhani mimi sijui wakati ambapo natafuta namna nzuri ya kurudisha kila kitu mikononi mwangu. Kama kweli itakuwa mamamkwe ndiye alizikopa na kaogopa kusema bado kwangu mimi sio jambo baya pia!

Kumpiga chini au kutompiga yatakuwa ni maamuzi ya mwisho baada ya kurudi home na kuweka kila kitu wazi!..(hilo jina la 'esther' umenikumbusha mbali kidogo)..otherwise pamoja sana!
 
Mkuu umefanya vizuri kuongea na mama yake. Binafsi kitu ninachoona hapa ni kuwa huyo bidada hafai kwa vigezo vya uaminifu, umemuamini kwa kiasi kikubwa sana, alishindwa nini kukuambia hata kama ingekuwa kweli kuwa ni mama yake amezitaka?! Mbona wachumba huambizana hata mambo ya ndani sana ya familia zao? Usidanganyike, hata ingekuwa elfu hamsini bado ni hela yako na angetakiwa kukushirikisha, hapa siyo suala la u-malaika bana hivi uaminifu unaanzia wapi? Watu tumetofautiana sana, binafsi mtu wa aina hiyo ni kutafuta namna ya kuipata ATM card yako halafu unaachana naye kistaarabu tu.
 
Sasa Bw. Snowball ninachokushauri ni kwamba hili sio tatizo la kukufanya usitishe uchumba. Ni kweli mtu wa karibu kiasi hicho kukuzunguka inauma sana. Lakini ni mambo yanayotokea hata kwenye ndoa. Isitoshe huwezi jua huenda mkeo mtarajiwa alifanya hivyo kwa kurubuniwa na mama yake. Huenda alitoa hizo hela kinyume kabisa na dhamiri yake, labda alishindwa kumkatalia mama yake mzazi. Hayo yote unapaswa kuyafikiria kabla hujafanya maamuzi. Binafsi sioni sababu ya kutosha kufikiria upya uhusiano wako na mchumba wako. Jiulize, je angekuwa mke tayari, kwa hili tu ningeanza mchakato wa kutafuta talaka?
 
WanaMMU heshima mbele.

Ni siku kadhaa hivi nilitupia uzi wenye kwenda kwa jina 'Namuanzaje mamamkwe'?. Kwa kweli naomba nishukuru kwa Mawaidha, Ushauri, Maonyo pamoja na Michango yote kiujumla. Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kufuata ushauri wa kupiga simu ili niongee na mamamkwe kuhusu issue iliyokuwa inanitatiza. (Kwa wale ambao watakuwa hawafahamu nini kinaendelea wanaweza kujikumbusha HAPA ). Kilichonileta tena ni kuleta 'feedback' kulingana na mlivyonishauri. Kiukweli niliamua kuwasilaina na mamamkwe na mazungumzo yetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Snowball: Hallow mama shikamoo!
Mamamkwe: Marhaba mwanangu..za siku..za huko?
Snowball: Nzuri tu mama..halaf pole na matatizo ya kazini kwenu mama..
Mamamkwe: (kama akastuka)..Ahsante mwanangu..si unajua tena mambo ya kazini..
Snowball: Sasa mama nilikuwa naomba majina yako kamili ili nikutumie japo kiasi kweye western union(nikafix ili kuona ukweli).
Mamamkwe: hapana baba..yale mbona yaliisha..hayakuwa makubwa..isitoshe kama ningehitaji pesa mbona ningekuambia mwanangu..yameisha baba!!
Snowball: (Nikashtuka)..Kweli mama??
Mamamkwe: Kweli mwanangu
(Nikajibaraguza na mengineyo kisha nikakata simu).

Kwa kuhofia labda mama kajivunga ili kuua soo..nikatulia kidogo ili kuona kama watawasiliana na binti yake na kwa vyovyote nikajua atanipigia. Hamadi baada ya kama lisaa hivi mchumbaangu akanipigia na kikubwa akaniambia mama alimuambia kuwa nimempigia simu na yeye mchumbaangu akaniuliza kama nilimulizia kuhusu pesa (inaonekana mamamkwe hakumgusia hii kitu) na mimi nikamdanganya kuwa sijamgusia chochote zaidi ya kumsalimia. Eti mchumbaangu akanipongeza kwa kutomuuliza mamamkwe habari za pesa zaidi akinisihi kuwa tumuache tu mama atazirejesha!!!Sikusema chochote zaidi tukaagana na nikakata simu.

Jamani huyu ndiye mchumbaangu ambaye Mungu kama atapenda baadaye mwaka huu eti tutafunga ndoa!!!..Kwa kweli tangu hapo nimeanza kuwaza vitu vingine tofauti!!!..Na pia nimeamini 'pesa mwanaharamu'.
Ahsanteni kwa waliochangia ule uzi....kwa kweli i am fed up!!..Ni laki tano tu but it has given me a lesson!!!!

If this is the way you approach life, then call yourself A BIG LOSER!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom