kiroba
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 324
- 114
Nikiwa kama mtanzania mwenye kuipenda nchi yangu tukufu Tanzania, napenda kutoa maoni yangu kuhusu huyu kijana aliyeshujaa anayepaswa kuungwa mkono kwa hali na mali. Kwa maoni yangu Mh Lema anapaswa kuwa kama hivi
1. Ikumbukwe ni vigumu sana kupata vijana wenye ujasiri kama Mh Lema. Hivyo kwa kuwa Mh Lema ameonyesha uthubutu wake basi sidhani kama akipewa kazi ya kuzunguka nchi nzima kuanzisha vuguvugu la ukombozi itakuwa ni kosa. Mh Lema kwa sasa hadhi yake ni ubunge wa nchi nzima na wala si Arusha tu. CDM mulione hili kwani kumtumia Mh Lema kwa jimbo la Arusha tu ni kuwanyima haki watanzania ya kupatiwa elimu ya ukombozi na huyu jasiri.
2. Kwa kuwa Mh Lema ameamua kujitoa kwa kuitetea nchi yake basi vijana hawana budi kumuunga mkono kwa hali na mali. Mimi nadhani kwa kumtumia Mh Lema kuzunguka nchi nzima na kusambaza M4C na vuguvugu la ukombozi basi tutakuwa tumewafaidisha watanzania wote na si wana wa Arusha tu.
3. Viongozi wakuu wa CDM wamchukulie Mh Lema kama ni kijana aliyejitoa muhanga kuikomboa nchi yake. Hivyo apewe ushirikiano wa kutosha wa hali na mali. Pia wamtie moyo kwa kazi anayokwenda kuifanya kwa kuwa ni kazi ngumu sana na yenyekuhitaji uvumilivu wa hali ya juu.
4. Mungu muongoze huyu kijana jasiri ili aweze kuandika historia ya ukombozi wa tanzania yetu. Vijana wote wawe nyuma ya huyu shujaa na wampe ushirikiano wa kutosha. Ni kweli Mh Lema ameanza na mungu na inshaalah atamaliza na mungu!
Saa ya ukombozi ni sasa, vijana amkeni!