Namshauri kocha Amunike ajiuzulu, asisubiri kufukuzwa

shirima Mathias

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
451
1,320
Tetesi zimeshaanza kuzagaa, na hivyo ccm kujiondolea aibu ni kutafuta pa kujificha, ilani imekwamishwa na AMUNIKE. Kujiuzulu ni heshma kuliko kufukuzwa. Ni hayo tu. Munisamehe
 
Kujiuzuli ni kuvunja mkataba wako mwenyewe,kufukuzwa ni kuvunjiwa mkataba,mkataba wako ukivunjwa malipo hufuata.Ukocha siyo siasa kwamba ukijiuzulu unajipatia heshima,ndio maana wakasema coaches are hired to be fired.
 
pengine mkataba wake na TFF unasema akijiuzulu atakuwa kajifukuzisha kazi mwenyewe so no mshiko ila TFF wakimfukuza wao ndio watakuwa wamevunja mkataba hivyo watalazimika kumlipa jamaa mshiko wa nguvu.

Nadhani huwa unaona hata makocha wa vilabu Ulaya kama kina Mournyo huwa wanakomaa hadi wawe sacked wapate mshiko wa nguvu kuliko kujiuzulu
 
jaman kocha hana kosa, safar yoyote huanza na single steps, haikua rizki tu, ni kocha uyo uyo katuingiza kwenye mashindano ambayo ni miaka mingi tukiyashiriki, asiekubali kushindwa si mshindani kwani kocha ndo aliwafanya wapaishe mipira juu ya gori? What if isinhepaa ikaingia kocha uyo uyo mngesema anastaili pongezi. Tumecheza na wazoefu, na timu zenye ranks, ni afadhar tumepata hata tuition next time tutasogea mbele zaidi..

Aya click apa upate vocha zako https://jamiiforums.com/r56SdaG1UX
 
Ushauri wangu mdogo tu !! Tulete Kocha au msaidizi kutoka hukohuko tulipo fungwa ..ili atupe mbinu zao!!
 
Kwanza wamuite bashite kwenye kikao chao cha neki, wamuulize sababu ya sisiemu stars kufungwa, wakati yeye alishawaahidi timu itatekeleza ilani ya sisiemu kwa mafanikio makubwa.. Ufuatao ndo mahojiano kati ya neki na bashite;

neki stone: wewe uliahidi sisiemu stars itatekeleza ilani vizuri kwa kuifunga harambee stars, na haikuwa hivyo, kwanini..?

bashite: mheshimiwa, mkuu wa polisi kamana sio alikataa kutoa polisi wake kuandamana na mie hadi misri, peke yangu ningewezaje bila ya wao..?

neki stone: weee kamanda sio, kwanini ulikataa wito wa kutoa vijana wa kuandamana na mwanangu misri..? nakulipa mshahara wa kazi gani..?

kamanda sio: mkuu mie niliomba kibali kwa tume ya uchaguzi wakasema niwasiliane na jecha.. mkuu jecha niliwasiliana nae akaniahidi angerudi kwangu.. wakati nasubiri ndio nikasikia hivyo tena, timu yetu ya sisiemu stars imefungwa.. mkuu imeniuma sana na kuna watu wanafurahia, ila watanikoma hawa mkuu, niachie mie mkuu..

bashite: mheshimiwa kwa ruksa yako naomba nianzane na yule wakili wa kike mwenye kimbelembele yule, amekudhalilisha wewe na mie na timu yetu nzima ya sisiemu stars..

neki stone: fanya upendavyo lakini sipendi kuona mabaki, maana umevurunda sana hapa kati..

😜😜
 
Ushauri wangu mdogo tu !! Tulete Kocha au msaidizi kutoka hukohuko tulipo fungwa ..ili atupe mbinu zao!!
Mpira ni zaidi ya mbinu za kocha, mpira huanza na kipaji. vipaji hutofautiana kuna vipaji vya viwango,WATANZANIA wengi tunadhani mpira ni wa kujifunza kama kuwafundisha wanajeshi ilimradi una akili timamu na afya njema.Wengine wanasema tuwekeze kwenye soka la vijana kwa kuanzisha football academy nyingi,shida ni kuwa je kuna vipaji vya kiwango cha akademi halisi au tutaishia kuwa na vitu kama akademi.Tunalazimisha kuwa taifa lenye mafanikio ya kisoka,kwa hisia kama waganga wa kienyeji.Mpira ni mchezo wenye pesa sana ingekuwa ni kujifunza tu bila vipaji leo hii waarabu na nchi nyingi za ulaya zingekuwa na watu wengi sana kwenye mchezo wa soka.Vipaji ndio vinafanya Brazil,Ujerumani na Italy kuchukua kombe la dunia mara kadhaa kuliko nchi nyingine nyingi.
 
Jecha alisharekebisha mambo,
IMG-20190703-WA0001.jpg

Wanatekeleza Ilani, Kocha anaviwango vya Kimataifa si vyakutekeleza Ilani.
 
Binafsi ninamsifu sana kocha huyu kwa kazi nzuri. Tulipoishina Uganda 3 bila mpaka tukambeba kocha juu juu si alikuwa ni huyuhuyu Amonike! Leo tumtake ajiuzulu kwa sababu tu Samata na Msuva hawakufunga magoli, goalkeeper wetu alishindwa kutaka mikwaju mikali kwa sababu mabeki wetu hawakuwa makini?

Hivi unaweza kumleta Gadiola tanzania akaifanya Taifa Stars ichukue ubingwa wa Afcon?

Tunajua tulipoangukia lakini je, ni wapi tulipojikwaa? Kwa hali ilivyo taifa Stars haiwezi kushinda hata afcon ijayo lakini maandalizi yakifanyika vizuri kuanzia sasa afcon ijayo tutafika walau 16 bora.

Amonike amefanya kazi kubwa na nzuri ni vema akaendelea kuwapo badala ya kumleta mwingine aanze moja kutuzoea. Hata hivyo, kama tukiamua kumuondoa Amonike haitakuwa sababu hatukufanya vizuri kwenye afcon bali kwa sababu tunadhania kuwa kocha mwingine atafaa zaidi au tumemchoka tu huyu kocha na hayo yatakuwa ni maamuzi ya hovyo japo tutayakubali tu!
 
jaman kocha hana kosa, safar yoyote huanza na single steps, haikua rizki tu, ni kocha uyo uyo katuingiza kwenye mashindano ambayo ni miaka mingi tukiyashiriki, asiekubali kushindwa si mshindani kwani kocha ndo aliwafanya wapaishe mipira juu ya gori? What if isinhepaa ikaingia kocha uyo uyo mngesema anastaili pongezi. Tumecheza na wazoefu, na timu zenye ranks, ni afadhar tumepata hata tuition next time tutasogea mbele zaidi..

Aya click apa upate vocha zako https://jamiiforums.com/r56SdaG1UX
Kujifariji ujinga...madagascar first attempt na wameingia hatua ya 16 bora. Fatizo ni moja tuu...hatujui mpira na hatutatika kufanya sacrifices ambazo mafanikio ya mpira yanahitaji.
 
Kwani kijiuzulu ni jambo la sifa au heshima, wenzetu sio wakukata tamaa kama sisi wabongo....mpira ni jambo la taratibu kufika kileleni
 
Una maana tupate, msenegali, mualgeria au mkenya, maana hao ndo waliotufunga? Au una maana tupate mmisri!
Ahssante... Tupate Kocha Mwaraabu ..Maana miaka mingi tumekuwa wateja wao tukikatizwa na kuzidiwa Maarifa na umahiri ktk Soccer (mpira lhisha yake Lazima ufunzwe) Siri ipo kwao....
 
Mpira ni zaidi ya mbinu za kocha, mpira huanza na kipaji. vipaji hutofautiana kuna vipaji vya viwango,WATANZANIA wengi tunadhani mpira ni wa kujifunza kama kuwafundisha wanajeshi ilimradi una akili timamu na afya njema.Wengine wanasema tuwekeze kwenye soka la vijana kwa kuanzisha football academy nyingi,shida ni kuwa je kuna vipaji vya kiwango cha akademi halisi au tutaishia kuwa na vitu kama akademi.Tunalazimisha kuwa taifa lenye mafanikio ya kisoka,kwa hisia kama waganga wa kienyeji.Mpira ni mchezo wenye pesa sana ingekuwa ni kujifunza tu bila vipaji leo hii waarabu na nchi nyingi za ulaya zingekuwa na watu wengi sana kwenye mchezo wa soka.Vipaji ndio vinafanya Brazil,Ujerumani na Italy kuchukua kombe la dunia mara kadhaa kuliko nchi nyingine nyingi.
Well said!! Naamini vijana wapo !! Facilities hazipo!!
 
Tetesi zimeshaanza kuzagaa, na hivyo ccm kujiondolea aibu ni kutafuta pa kujificha, ilani imekwamishwa na AMUNIKE. Kujiuzulu ni heshma kuliko kufukuzwa. Ni hayo tu. Munisamehe
Timu apewe Bashite awe kocha mkuu. Msaidizi wake awe Slowslow. Hapo tutachukua wedikapu asubuhi tu.
 
Back
Top Bottom