Namshangaa Mh. Mbowe....!!

Namshangaa Mh. Mbowe....!!

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,298
Reaction score
38,438
Akihutubia wananchi wa Vunjo amesema Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC haiko huru kuanzia leo,baada ya baadhi ya watendaji kubadilishwa hivyo kuanzia sasa wananchi watambue Tume yao haiko huru.

Hivi kabla ya baadhi ya watendaji kubadilishwa Tume ilikuwa huru?

Ina maana miaka yote Tume ilikuwa huru Hadi leo watendaji walipobadilishwa ndio imekosa uhuru.?

Mh.Mbowe uache kutulaghai wananchi na kutuona hatuna uwezo wa kufikiri wala kuona kinachoendelea ndani ya siasa zetu.!

Wengi tunaelewa Tume haiko huru miaka yote , hivyo unaposema kuanzia leo, unawafanya wenye uelewa wazidi kukushangaa kwa misimamo na kauli zako zenye ukigeugeu.!
 
Anatafuta chaka la kufichia aibu zake baada ya kugaragazwa vibaya sana na Rais Magufuli
 
Kikwete asidhani atasalimika kwa kuitumia Tume!
Kila Mtanzania anafahamu kuwa CCM inaondoka sasa!
 
Amesema kweli, huyo mtu kafanya bvr mara anaondolewa ghafla kipindi hiki
 
Kikwete asidhani atasalimika kwa kuitumia Tume!
Kila Mtanzania anafahamu kuwa CCM inaondoka sasa!

Mbowe anaposema kuanzia leo Tume haiko huru, huko nyuma ilikuwa huru.?
 
Mheshimiwa Jaji mstaafu Lubuva tuthibitishie madai ya Ukawa kuwa tume yako ya uchaguzi imetawaliwa na maofisa wapya na askari jwtz waloteuliwa na Mh.Rais Kikwete.
Mzee Lubuva unapokaa kimya sisi wananchi tunayumbishwa na madai ya Ukawa na vyama vingine vya siasa ukizingatia kwamba wewe una utumishi uliotukuka,tuna imani na wewe.
 
Tume wakati wote imeundwa na raisi!
Kwanini Mbowe atake kuipangia tume nani awe mjumbe nani asiwe!
Ni tume ya taifa tu (NEC) iliyokosa Uhuru!
Yeye aseme ni tume ipi iliyomkata Slaa?
Je chadema iko huru?
Aache kujitia utakatifu asio kuwa nao!
 
Kishapagawa. chezea jembe wewe! wait watanyoooooookaaaaa...... tuuu... nawacheka kwa dhalau hahahahahahahahah.......
 
Tume wakati wote imeundwa na raisi!
Kwanini Mbowe atake kuipangia tume nani awe mjumbe nani asiwe!
Ni tume ya taifa tu (NEC) iliyokosa Uhuru!
Yeye aseme ni tume ipi iliyomkata Slaa?
Je chadema iko huru?

Aache kujitia utakatifu asio kuwa nao!
Nyani haoni kundule hata kama linaachia uharo ovyo majukwaani.
 
Alieanzisha uzi hajamwelewa mboye na hatakaa amwelewe!
Huyo kweli sijamwelewa hata kumsikia sijamsikia.

Mimi namwongelea Mbowe Mwenyekiti wa Chadema.!
 
Nyani haoni kundule hata kama linaachia uharo ovyo majukwaani.
Umejidhalilisha sana! Hata kama ni chuki hii yako imepita kiwango! LOWASSA ndiye Rais wako baada ya KIKWETE! Taka usitake!
 
Kimsingi Mbowe anapenda sana kulalamika, lakini akumbuke kwamba alisema wamemchukua Lowasa kwani ndo anajua wizi wa ccm, mbona tena anatapatapa?

Na wao wataangaika sana, kwani Mwl.Nyerere aliwahi kuwambia kwamba ni vema wakatafuta nafasi za kutumikia wananchi kwa maana ya serikali/mitaa, udiwani na ubunge alafu wakishaaminiwa wapewe nchi, walipuuza ushauri wa baba wa taifa, huwezi kuwa na wabunge 27 kati ya majimbo 266, alafu unataka Urais, ni aibu sana, wangetumia nguvu nyingi kwenye ubunge na udiwani maana yake tungepata hiyo tume huru na sheria nyingi zingekaa vizuri na ndo shida ya watz, wao wamekomaa na Urais wakati wagombea wao tena walio wengi hawana fedha za kufanyia kampeni, kila siku wimbo wao ni tume ya uchaguzi.

Kweli katika hali ya kawaida utawapatia nchi watu ambao kila kukicha ugombana kwenye nafasi za majimbo? hii nafasi ya Urais bado haiwafai kabisa.
 
Tume wakati wote imeundwa na raisi!
Kwanini Mbowe atake kuipangia tume nani awe mjumbe nani asiwe!
Ni tume ya taifa tu (NEC) iliyokosa Uhuru!
Yeye aseme ni tume ipi iliyomkata Slaa?
Je chadema iko huru?
Aache kujitia utakatifu asio kuwa nao!
Amekubali kuingia kwenye uchaguzi ambao Tume inaundwa na Rais, halafu anataka kumpangia Rais watendaji wa kuwaajiri, huyu Mbowe laghai sana.!
 
Back
Top Bottom