Nampongeza mh.Said Juma Nkumba

Nampongeza mh.Said Juma Nkumba

mayuni

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
404
Reaction score
32
Kwa namna moja mimi ni mchanga kwenye siasa....ila nampongeza mbunge wangu wa Sikonge kwa hotuba yake iliyofanyika wiki iliyopita.hotuba yake ilijikita sana katika suala la maendeleo. Na baada ya hotuba kila mwananchi alionekana kuvutiwa na hotuba ile. Hongera sana muheshimiwa Said Juma Nkumba
 
Nini ? unaamini wote tupo Sikonge
weka hapaa alisema nini tujadili acha ubinafsi.
 
kwa namna moja mm ni mchanga kwenye siasa....ila nampongeza mbunge wangu wa sikonge kwa hotuba yake iliyofanyika wiki iliyopita.hotuba yake ilijikita sana katika suala la maendeleo.na baada ya hotuba kila mwananchi alionekana kuvutiwa na hotuba ile.hongera sana muheshimiwa Said Juma Nkumba
ngoja aje sikonge atufafanulie -- nyie wengine hamuaminiki kabisa.
 
kwa namna moja mm ni mchanga kwenye siasa....ila nampongeza mbunge wangu wa sikonge kwa hotuba yake iliyofanyika wiki iliyopita.hotuba yake ilijikita sana katika suala la maendeleo.na baada ya hotuba kila mwananchi alionekana kuvutiwa na hotuba ile.hongera sana muheshimiwa Said Juma Nkumba

Hivi Said Juma Nkumba ni huyu "Sharp Shooter wa Bunge?" Kama ndiye nakubalina na wewe kijana ni SMART, hana makuu.
 
Nini ? unaamini wote tupo Sikonge
weka hapaa alisema nini tujadili acha ubinafsi.

alisema kwamba imefikia wakati wakazi wasikonge tuache malumbano ya kisiasa na kuangalia maendeleo ya sikonge...nikajaribu kukaa na vijana wengi na kugundua kuwa kauli hiyo imewavutia na kuumunga mkono mh.Nkumba Said..
 
Katika watu nisiotaka hata kukutana nao ni pamoja huyu jamaa eti mwakilishi wa watu jimbo la Sikonge, hata sijui kazi zake kila siku ni nini?

wasting time to discuss about this eti member of parliament!!! -- watu wa sikonge hawana mwakilishi serikalini, kama unabisha fanya utafiti.

Hakuna kinachoendelea wilayani sikonge si kilimo cha tumbaku, uvuvi, uvunaji asali nk - vijana, kina mama, wazee wote wa wilaya hii wamechoka vibaya mno; mbunge hana mkakati wowote kunyenyua uchumi wa watu wa wake, yaani hata kuishawishi serikali kuwekeza hata viwanda vidogo vidogo hakuna, bulding capacity kwa vijana kujikwamua ki-uchumi hakuna aisee!!

Kama kweli tunataka kuendelea lazima 2015 tuchague mwakilishi atayetufikishia matatizo yetu, as of now Sikonge ipo nje ya ramani ya tanzania. Anayebisha atembelee vijiji hivi Sikonge yenyewe, Chabutwa, ipole, usunga, imalampaka, mibono na viunga vyake akajionee mwenyewe ninachokisema.
 
Kwa namna moja mimi ni mchanga kwenye siasa....ila nampongeza mbunge wangu wa Sikonge kwa hotuba yake iliyofanyika wiki iliyopita.hotuba yake ilijikita sana katika suala la maendeleo. Na baada ya hotuba kila mwananchi alionekana kuvutiwa na hotuba ile. Hongera sana muheshimiwa Said Juma Nkumba

ww ni muongo sana kwani binafsi sikuwepo hapo mkutanoni ila kupitia waliokuwepo na habari za mtaani ni kwamba Nkumba alikosa kabisa watu na hata walioudhuria ni wanachama wa CCM tu.
 
ndiyo huyo ninaemzungumzia he is acceptable man in Sikonge

Dunia ya leo ukisema uongo ujue hautafika mbali ..mie nimekaa hapa sikonge toka 2010 na nilishuhudia kila kitu pale mpaka jinsi alivyoshindwa na kulazimika kununua ubunge toka kwa aliyekuwa ameshinda(CUF)

kwa ufupi tu watu hawampendi na wala hana hata mtizamo mwema toka kwa watu make ni mtu wa kufunga vioo muda wote na si wa kujichanganya na watu

mkihitaji mengi semeni niwaletee niko tayari.
 
ww ni muongo sana kwani binafsi sikuwepo hapo mkutanoni ila kupitia waliokuwepo na habari za mtaani ni kwamba Nkumba alikosa kabisa watu na hata walioudhuria ni wanachama wa CCM tu.

Kwani hao si watu?
 
Katika watu nisiotaka hata kukutana nao ni pamoja huyu jamaa eti mwakilishi wa watu jimbo la Sikonge, hata sijui kazi zake kila siku ni nini?

wasting time to discuss about this eti member of parliament!!! -- watu wa sikonge hawana mwakilishi serikalini, kama unabisha fanya utafiti.

Hakuna kinachoendelea wilayani sikonge si kilimo cha tumbaku, uvuvi, uvunaji asali nk - vijana, kina mama, wazee wote wa wilaya hii wamechoka vibaya mno; mbunge hana mkakati wowote kunyenyua uchumi wa watu wa wake, yaani hata kuishawishi serikali kuwekeza hata viwanda vidogo vidogo hakuna, bulding capacity kwa vijana kujikwamua ki-uchumi hakuna aisee!!

Kama kweli tunataka kuendelea lazima 2015 tuchague mwakilishi atayetufikishia matatizo yetu, as of now Sikonge ipo nje ya ramani ya tanzania. Anayebisha atembelee vijiji hivi Sikonge yenyewe, Chabutwa, ipole, usunga, imalampaka, mibono na viunga vyake akajionee mwenyewe ninachokisema.

siko hapa kwa ajili ya kujua nani ni nani....nipo hapa kusema kuile nilichokiona na kusikia...naipongeza hotuba yake na wala si kingine...mimi ni mchanga kwenye siasa
 
Dunia ya leo ukisema uongo ujue hautafika mbali ..mie nimekaa hapa sikonge toka 2010 na nilishuhudia kila kitu pale mpaka jinsi alivyoshindwa na kulazimika kununua ubunge toka kwa aliyekuwa ameshinda(CUF)

kwa ufupi tu watu hawampendi na wala hana hata mtizamo mwema toka kwa watu make ni mtu wa kufunga vioo muda wote na si wa kujichanganya na watu

mkihitaji mengi semeni niwaletee niko tayari.

inawezekana ikawa kweli kwa namna ya wewe unavyomjua..ila mimi naipongeza hotuba yake..mimi kama kijana wa Sikonge...mimi mengine siyajui lbda kama ndo unanielewesha...
 
ww ni muongo sana kwani binafsi sikuwepo hapo mkutanoni ila kupitia waliokuwepo na habari za mtaani ni kwamba Nkumba alikosa kabisa watu na hata walioudhuria ni wanachama wa CCM tu.

idadi ya watu haifanyi mtu kutokusema ukweli...hat hao wanachama ni wakzi wa Sikonge na sio wa USA..hata wao pia ni wanamaendeleo...
 
Nkumba ni moja kati ya wanasiasa bugus sana...kilichokuwa kikimuinua ni baba yake kuwa m/kiti ccm mkoa,huyu mzee alikuwa mzee wa fitina na juju za kufa mtu..kila mgombea ilikuwa ni lazima ampelekee mlungula kijijini kwake la sivyo jina lako linakatwa...wanasikonge tunalia sana hatuna mbunge jamani.
 
Wewe ndhani huijui skonge hivi Nkumba ni wakusifia kwa lipi kama angekuja na jipya angeleta mkakati mpya wa kuipatia skonge maji wa maana hapo angeeleweka
 
Dunia ya leo ukisema uongo ujue hautafika mbali ..mie nimekaa hapa sikonge toka 2010 na nilishuhudia kila kitu pale mpaka jinsi alivyoshindwa na kulazimika kununua ubunge toka kwa aliyekuwa ameshinda(CUF)

kwa ufupi tu watu hawampendi na wala hana hata mtizamo mwema toka kwa watu make ni mtu wa kufunga vioo muda wote na si wa kujichanganya na watu

mkihitaji mengi semeni niwaletee niko tayari.

Duh!! Nilidhan huyu bwana ameshakubalika kumbe bado.. Naomba me nitoe yale yalotokea mwaka 2000, manake uchaguzi huo ulinikuta huko... 1. Jamii ielewe kuwa Said ni mtoto wa Mzee Nkumba ambaye wakati huo ndo alikuwa M/kiti wa CCM mkoa wa Tabora wakati yeye (Said) akiwa mwl. wa primary. 2. Katika kura za maoni jina la Said lilipitishwa kwa mabavu hasa ukizingatia cheo cha babake. Kwa ufupi asingekuwa babake mwaka 2000 asingekuwa mbunge. 3. Kwenye kampeni za uchaguzi Said akitumia gari la chama huku Mzee Kasanga Tumbo (CUF) akitumia baiskeli na mara chache alikodi gari alimbwaga Said. Hata hivyo kwa nguvu za dola na mabomu walimtangaza Said kuwa mbunge wa Sikonge. 4. Baada ya kuwa mbunge ndo akaanza kurekebisha na kujenga nyumbani kwake... Kwa maana hiyo bac, nnao wacwac kama kweli 2005 alishinda kihalali.
 
Back
Top Bottom