Nampongeza mh.Said Juma Nkumba

Nampongeza mh.Said Juma Nkumba

Duh!! Nilidhan huyu bwana ameshakubalika kumbe bado.. Naomba me nitoe yale yalotokea mwaka 2000, manake uchaguzi huo ulinikuta huko... 1. Jamii ielewe kuwa Said ni mtoto wa Mzee Nkumba ambaye wakati huo ndo alikuwa M/kiti wa CCM mkoa wa Tabora wakati yeye (Said) akiwa mwl. wa primary. 2. Katika kura za maoni jina la Said lilipitishwa kwa mabavu hasa ukizingatia cheo cha babake. Kwa ufupi asingekuwa babake mwaka 2000 asingekuwa mbunge. 3. Kwenye kampeni za uchaguzi Said akitumia gari la chama huku Mzee Kasanga Tumbo (CUF) akitumia baiskeli na mara chache alikodi gari alimbwaga Said. Hata hivyo kwa nguvu za dola na mabomu walimtangaza Said kuwa mbunge wa Sikonge. 4. Baada ya kuwa mbunge ndo akaanza kurekebisha na kujenga nyumbani kwake... Kwa maana hiyo bac, nnao wacwac kama kweli 2005 alishinda kihalali.

2005 na 2010 alichakachua kura za maoni kwa kutumia nguvu ya baba yake na kumdhulumu ushindi mchumi mmoja anaitwa Joseph Kakunda. Kwa kifupi siku zote ushindi wake umekuwa wa kuchakachua.
 
siko hapa kwa ajili ya kujua nani ni nani....nipo hapa kusema kuile nilichokiona na kusikia...naipongeza hotuba yake na wala si kingine...mimi ni mchanga kwenye siasa
baada ya hotuba yake iliyokuvutia ungejaribu kuyafanyia kazi yale aliyoyaongelea then ukaja na hoja ikilichoiva, wanasiasa wachanga huwa hawa-copy na kupaste bali wanafanya uchambuzi wa kina na kutoa mtazamo wao. kwa namna hii siamini kama unaweza kukomaa kisiasa mi naona utadumaa.
 
Nimetoka juzi sikonge sasa huyu anayempongeza Nkumba sijui ana zungumza nin,Sikonge ni wiliaya ya mwisho kabisa kimaendeleo ktk mkoa wa Tbr,kutoka Tbr mjini mpaka Wilaya ya sikonge ukifiika kwa uchakavu wa barabara na ubovu wa barabar hiyo cha kwanza ukifika na kunywa dicloper kwa maumivu makali ya mwili,vijana wa sikonge hawana fursa za kielimu,chuo cha ufundi,miundo mbinu ya aji hakuna,huduma ya afya ni hafifu,ukitoka chabutwa kuelekea kitunda kuliko na mgodi wa dhahabu sasa hakuna umeme hakuna hata mawasiliano ya cm kiufupi wananchi wa sikonge wanahitaji kubadilisha muwakilishi hawana muwkilishi kabisa anayeweza kusimama kuwatetea na kuwapelekea mahitaji yao kwa serikali na muwakilishi huyo akayasimamia sas wameteseka vya kutosha wasikosee tena 2015.
 
kwa namna moja mimi ni mchanga kwenye siasa....ila nampongeza mbunge wangu wa sikonge kwa hotuba yake iliyofanyika wiki iliyopita.hotuba yake ilijikita sana katika suala la maendeleo. Na baada ya hotuba kila mwananchi alionekana kuvutiwa na hotuba ile. Hongera sana muheshimiwa said juma nkumba

ni nkumba huyu huyu amabye baba yake alikuwa kiongozi wa chama pale tabora? Nini kafanya cha kukustaabisha hata kama ni mchanga wa siasa? Me ni mkazi wa tabora pia but honestly sijawahi jivunia mbunge yeyote mkoani mwangu....wengi wamekuwa wachumia tumbo na wabinafsi wa hali ya juu. Zaidi wamekuwa viongozi wasio na vision....hivyo kupelekea mkoa wetu kuwa nyuma kimaendeleo licha ya wanachi kuendelea kuwachaugua viongozi wa ccm kwa miaka 50 sasa....

Hotuba yake imekupendeza nini wakati hata barabara kutoka tabora mjini mpaka sikonge ni vumbi miaka nenda rudi?

Hotuba yake inakupendeza nini wakati wananchi wa sikonge wengi wao wanakula mlo mmoja kwa siku.?

Inakpendeza nin hotuba hii wakati wakulima hawa wa tumbaku wameendelea kupata shida licha tumbaku kuwa ni zao linaloiingizia serikali pato kubwa?


Tusiwe wanafiki kiasi tunasahau shida za wanaishi kwa kuendekeza kuwasifia viongozi ambao wameshindwa kutuvusha kimaendeleo

 
Wewe ndhani huijui skonge hivi Nkumba ni wakusifia kwa lipi kama angekuja na jipya angeleta mkakati mpya wa kuipatia skonge maji wa maana hapo angeeleweka

ni kweli mkuu hiyo ni hoja ya maana.hivyo kitendo cha kutoa mikakati yake ndo kimenifanya nimpongeze japo inawezekana suala la maji hakusema...
 
Mimi huwa nasahau kabisa kama kuna wilaya inaitwa Sikonge, naona inaniwea vyepesi kutamka wilaya mpya kama Chato, Kakonko, Uvinza etc etc kuliko kutamka wilaya ya Sikonge wakati ni wilaya kongwe hata sijui nina shida gani wajameni
 
Mimi huwa nasahau kabisa kama kuna wilaya inaitwa Sikonge, naona inaniwea vyepesi kutamka wilaya mpya kama Chato, Kakonko, Uvinza etc etc kuliko kutamka wilaya ya Sikonge wakati ni wilaya kongwe hata sijui nina shida gani wajameni

labda ni nkumbaphobia
 
Back
Top Bottom