OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,013
- 114,360
Napenda kumpongeza,kumtia moyo na kumuombea kwa Mungu Mh.Tundu Lissu Mbunge na Rais wa TLS
Ni dhahiri kwamba nchi ipo katika tahamaki ya hali ya juu kabisa. Kwa umri wangu mimi hii ni tahamaki kubwa kuliko zote nilizowahi kishuhudiwa. Mparanganyiko huu hasa unatokana na utawala kutokuambilika wala kupokea ushauri wa yeyote yule. Kwamba haupangiwi na mtu cha kufanya
Lakini Mungu hawezi kukunyima vyote,ametupatia Tundu Lissu. Huyu ni mwanasiasa na nwanasheria aliye mstari wa mbele kabisa kukemea utawala pale unapofanya fyongo.
Tundu Lissu kwa uwakili wake angeweza kukaa kimya tu kama kina Membe, Prof.Shivji na Prof.Mwandosya. Au akala buyu kama wakili Mkono akapiga pesa za uwakili,lakini anajitoa kwa ajili ya watanzania wote.
Ni wangapi wanaoweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya wengine wasio ndugu zao wa damu,ni wangapi wapo tayari kulala sero bila idadi kwa ajili ya kupigania ukombozi? Wapo watu wanatamani sana kusema lakini wanaishia kufumbafumba tu kwa hofu kubwa. Wengine ni wa kubwa kabisa tupo nao humu kwenye fake ID. Mungu wasamehe
Mtu huyu ni wa kumuombea kwa Mungu azidi kumuongezea na kumuepusha na maadui wa aina mbalimbali