sakapal
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,804
- 1,424
Nimekaa nae sana,mpaka wazazi wake wamekaa nae na kuuliza tatizo ni nini hasemi tatizo,nimemuomba anisamehe kama mimi ndo tatizo anambie nijirekebishe wapi anatulia siku mbili ananimbembeleza asubuhi jioni tukio lingine kubwa zaidi linatokea. nakumbuka kuna siku mpaka mamake kalia mbele yangu akimsihi mwanae abadilike.
Kunavitu huwa watu wengi siku hizi hatuviangalii au hatuvijali tena kama babu zetu au mababu zetu zamani. Jaribu kuchunguza kwenye ukoo wao inawezekana kuliwahi tokea mtu aliyewahi kuwa na tabia kama zake kwenye ukoo wao huko nyuma au watoto wa shangazi zake au watoto wa mama wadogo au wakubwa yaani angalia ukoo wote kama unaweza. Maana vitu hivi ambavyo saa ingine vinatokea kwa tabia za kurithi ambazo zinaweza jitokeza baada ya mtu kufika umri fulani au baada ya wakati fulani na hili mtu anajikuta tuu anafanya bila kujijua na inaweza kuwa hata yeye hapendi anajikuta tuu. Ukishagundua kitu ni rahisi kujua nini cha kufanya hasa maombi maana mambo ya mizimu ya ukoo inataka nguvu za rohoni kukabiliana nazo. Pia upande wa pili mambo ya ushirikina yapo, si watu wote walifurahia ndoa yenu either wanawake wengine walitaka waolewe nae hivyo baada ya kuona kawatolea nje basi wakamtupia kijini cha mahaba ili tu wamuahribie na hili hawezi jicontrol ila kwa maombi tuu tena ufungu mshipi haswaa au yaweza kuwa kuna mkaka alikupenda wewe na alitaka akuoe ila kwa kuwa umemkubali huyo mumeo na kuolewa nae hakutaka kukudhuru wewe kamdhuru huyo jamaa ili umuone kuwa hafai tena na wewe umeachika inaweza kuwa ni goal yake moja na ukiwa kwenye hali ya maisha mapya nje ya ndoa baada ya kuheal angalia watu watakaojitikeza kukufariji na kutaka kuanza mahusiano na wewe, lazima atajitokeza hapa ili kuziba nafasi na kuachive goal yake ya kukupata jaribu kuwa makini maana duniani kuna vitimbwi na vituko, kunabinadamu wako radhi wafanye lolote wawezalo wapate wanachokitaka watu wa namna hii waogope sana ni hatari.
Pole kwa yaliyokukuta na funga mshipi wa maombi na sala kila kukicha na kukikuchwa bila kuchopka wala kukata tamaa.