Mtasema yote lakini mnapo apa mbele ya mchungaji kuwa mpo tayari kuishi maisha yote ktk dhida na raha!
wengi wanadhani shida labda ni kulala na njaa tu au wakati wa ugonjwa.
huyo dada arudi kwa mume wake apigane ndio maisha hayo! mngejua mama zetu walivumilia mangapi msingekimbia ndoa zenu.
Ukitafakari maana ya ndoa mtajua si kitu cha kukimbilia maana unabeba yote si lelemama!
Binti rudi kwako pigana mtoto wa kike unamuachia mumeo machangu!
Usipotoshe ndugu sababu moja kubwa ya kuvunjika kwa ndoa ya kikristo ni ngono nje ya ndoa. Hili ni kwa mujibu wa Sir Jesus Christ mwenyewe. Hii dhana kuwa wanandoa, hasa kina mama, lazima wavumilie tu wenzi wao wanapokuwa mafuska nje ya ndoa imekaa kibinadamu zaidi haina msingi kwenye ukristo.