Nampenda na Kumtakia Heri Paul Makonda

Nampenda na Kumtakia Heri Paul Makonda

Ukiwa mzazi, hutampenda tu mwanao bali pia utamtakia heri. Hata mimi, sitaki mtu anipende tu, bali nimwone pia akinitakia heri.

NAMPENDA MAKONDA

Nampenda Makonda, namtakia heri.

Kwanza, nilimpongeza kwa ujasiri na nia yake njema aliyoionesha. Nilimwombea kwa Mungu, nikaahidi kuendelea kumwombea, nikamtaka naye awe na Mungu.

Kwa upendo mkubwa nilimtaka aanze upya kisha aendelee. Nilimtaka asiishie njiani ili aweke rekodi iliyotukuka.

NASISITIZA UPENDO
Nampenda Makonda na kumtakia heri ndiyo maana Nahitaji Makonda awe kiongozi mwenye kufanikiwa

Naipenda sana Tanzania yangu, nawapenda na kuwajali Watanzania wenzangu,
mimi ambaye nampenda Makonda bila unafiki. Nampenda kwa kumtakia heri.

Ndimi Luqman MALOTO
Rafiki wa kweli ni wakati wa dhiki, hivyo upendo wa kweli ni wakati wa shida, hivyo upendo ndio unaohitajika sana kwake katika kipindi hiki.

P.
 
Back
Top Bottom