nampenda lakini...

Mambo mengine wala hayaitaji ushauri wakati ukweli unaujua,au umezoea kudanganywa?Mtu kakwambia ana mtu wake,wat else do u want?kwahiyo unaomba ucku na mchana amuache alienae aje kwako!huko ni kuwa selfish,yani vizuri vyako,vibaya vya wenzako?Kama ulienae humpendi,ucmpotezee mda wake,mwambie mapema.
Sometimes tunakosa baraka za Mungu kwa mambo madogo madogo,ni sawa na kuomba Mungu akupe mke/mume wakati unatembea na mke/mume wa mtu.
Hicho kiatu cha penda penda kivue!
 
Tulia ndugu, haya mapenzi yakizungu yasikupotoshe! Uliwezaje kuwa na mtu usiyempenda kwa muda wote huo, alafu itakuwaje uendelee kupoteza muda kwa mtu mwingine ambae keshakwambia hawezi uza thamani ya penzi lao?? Think twice....
 
Dear Reina,
Pole sana kwa hali inayokukabili kusema ukweli 'you are stuck between a rock and a hard place'.Wakati mwingine moyo una hila ya kutaka visivyoweza kupatikana kwa urahisi au visivoweza kupatikana kabisa.Huyo kijana unayempenda amekuheshimu sana kwani angeweza kutumia mwanya huo na kukutumia vibaya,tafadhali na wewe mheshimu kwa kukaza moyo na kufanya uamuzi mgumu lakini wenye faida wa kuendelea na maisha bila kusubiri yasiyowezekana.Life is short make the most of it.Na kuhusu huyo anayekupenda lakini wewe haumpendi usijaribu kujilazimisha kumpenda utakuwa ni kama umekaa chini ya mti wa mwembe huku unasubiri chungwa lianguke.
 
nina mtu mwingine ananipenda sana lakini sina feelings zozote juu yake japokua ana nia ya kunioa. nifanyeje jamani??? naogopa kuolewa na nisiyempenda

nice conundrum.... gals never cease to amaze me!
 
mweleze ukweli usiyempenda awe huru kuwa na mweingine atakaye mpenda...kuhusu unayempenda ameshakueleza live bila chenga hakuna haja ya kuendelea kuharibu mahusiano ya watu wewe umeona muda unakwenda inawezekana sio kweli ni upofu/mapenzi uliyonayo kwa huyo mkaka tuli wakati wake ukifika utapata unayempenda na atakuoa. pole kwa kuumia moyo
 
Pole dear, penda akupendae, u dn love the guy then learn to love him ukishamzoea tu utashangaa mwenyewe ulikua wap mda wote huo kumshow some luv back.
 
Naona wengne hamjanipata vizuri. Sina uhusiano na huyo anaenipenda maana sitaki kumpotezea muda wake.
 
Aisay wanawake mnajua kupenda, yani ukisha penda....ndo huyo huyo poleni sana.

Mimi hata nikipenda vipi, atokeze mwinmgine mzuri na yeye napenda....Yani moyo wangu hauna ubaguzi, wanawake wote wazuri
nawapenda :biggrin:
mwenzangu wewe hupendi naona unatamani.kila mzuri unampenda!
 
Naona wengne hamjanipata vizuri. Sina uhusiano na huyo anaenipenda maana sitaki kumpotezea muda wake.
yah reina heshimu uamuz wake kwamba hawezi kumuacha mpenzi wake basi.
huyo wako jifunze tu kumpenda nina uhakika utampenda mwisho wa siku.
 
nimetokea kumpenda sana kijana mmoja hivi kiasi cha kutamani awe mume wangu! ana qualities zote ninazozitaka na ameshika dini pia. tatizo ni kwamba nimekuwa nikimpenda muda mrefu sana lakini kutokana na tamaduni nikashindwa kumweleza. nikapata tetesi kwamba ana mpenzi tayari lakini sikuamini maana alikua ana dalili za kunipenda pia. nilipomuuliza akaniambia ndio anaye mpenzi japokuwa ananipenda lakini hawezi kumuacha maana sio playboy.naumia sana kumpenda huyu kiumbe ambae sina uhakika kama atakuja awe wangu. sitamani mwanaume yeyote ila yeye tu. na yeye ananipenda pia lakini ndio hivyo ameshaingia kwenye relationship. nina mtu mwingine ananipenda sana lakini sina feelings zozote juu yake japokua ana nia ya kunioa. nifanyeje jamani??? naogopa kuolewa na nisiyempenda na pia naogopa kuendelea kumsubiri huyo ninaempenda maana sina uhakika kama atakuja kuwa wangu.
Pole shosti, shukuru mungu amekweleza ukweli na jaribu sana kumuepuka nakusudia ukaenae mbali ili iwe rahisi kumsahau,
kata mawasiliani nae na u focus na huyo ulokuanae kwani sio wote wanapata wanavyotaka wanapata walivyo jaaliwa kama akiwa rizki yako utampata hata huyo alokua atamuacha la kama huyo ulonae ndio uliandikiawa nae basi ndio atabaki kua huyo,zaidi muombe mungu akuonyeshe njia sahihi....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom