Nampenda lakini sina maisha

Nampenda lakini sina maisha

nsharighe

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
1,458
Reaction score
2,245
Wakuu Habari za muda huu, niende moja kwa moja kwenye mada.

Hii inanihusu Mimi mwenyewe na hapa Nawaza na kuwazua na sipati jibu sahihi, Nachanganyikiwa.

Mimi Ni kijana mwenye miaka 26, Elimu yangu Ni kidato Cha Sita na pia nilisoma Certificate in Clearing and Forwarding, Naishi Dar kwa Wazazi Ila nakaa chumba Cha nje Cha Peke angu,

Kwa muda Sasa nilikua nikitamani kuwa na familia, Yani mke na mtoto, ukizingatia rafiki zangu karibu wengi Wana maisha Yao na familia zao, niliwahi kuajiriwa lakini kwa Sasa Sina Kazi ya uhakika nadandia tu mishe yeyote itakayokuja mbele yangu.

Sasa Kuna huyu binti, mtoto wa Kanda ya ziwa, mzuri, binti mdogo miaka 20(Asomi) alikua akifanya Kazi za usaidizi za ndani, Muuni nikamuelewa nikaanzisha mahusiano nae, baada ya miezi kadhaa mwajiri wake akayumba Kiuchumi na kumuachisha Kazi.

Binti Hana ndugu mjini, kwao Ni mbali na maisha ya kwao pia wanamuangalia yeye ndio mwokozi wao, Kimsingi binti ananipenda na Mimi pia Nampenda na ndio msichana ninaetamani kuishi nae na kutengeneza familia.

Tatizo linakuja hapa, Mimi Jobless, kula kwa kengele japo sio kila siku kwasababu nikiwa na mishe zangu napenda kujitegemea kuliko kusumbua home, huyu mtoto wa watu nataka kumsaidia, nataka asiwe mbali na Mimi kusudi Mambo yangu yaki tiki niishi nae.

Kwa Sasa nimemuombea hifadhi kwa Dada yangu japo ya siku kadhaa na tayari Nina siku tano tu mbele za kujua hatma yake.

Nawaza nifanye Nini?? Nimtafutie nauli arudi kwao?? Nikae nae kibishi, atakula Nini? Ana mahitaji mtoto wa kike na Mimi Ni hohe have?? Naomba ushauri wakuu.
Natanguliza Shukrani.
 
Wakuu Habari za muda huu, Niende moja kwa moja kwenye mada.

Hii inanihusu Mimi mwenyewe na hapa Nawaza na kuwazua na sipati jibu sahihi, Nachanganyikiwa.

Mimi Ni kijana mwenye miaka 26, Elimu yangu Ni kidato Cha Sita na pia nilisoma Certificate in Clearing and Forwarding, Naishi Dar kwa Wazazi Ila nakaa chumba Cha nje Cha Peke angu,

Kwa muda Sasa nilikua nikitamani kuwa na familia, Yani mke na mtoto, ukizingatia rafiki zangu karibu wengi Wana maisha Yao na familia zao, niliwahi kuajiriwa lakini kwa Sasa Sina Kazi ya uhakika nadandia tu mishe yeyote itakayokuja mbele yangu.

Sasa Kuna huyu binti, mtoto wa Kanda ya ziwa, mzuri, binti mdogo miaka 20(Asomi) alikua akifanya Kazi za usaidizi za ndani, Muuni nikamuelewa nikaanzisha mahusiano nae, baada ya miezi kadhaa mwajiri wake akayumba Kiuchumi na kumuachisha Kazi,

Binti Hana ndugu mjini, kwao Ni mbali na maisha ya kwao pia wanamuangalia yeye ndio mwokozi wao, Kimsingi binti ananipenda na Mimi pia Nampenda na ndio msichana ninaetamani kuishi nae na kutengeneza familia.

Tatizo linakuja hapa, Mimi Jobless, kula kwa kengele japo sio kila siku kwasababu nikiwa na mishe zangu napenda kujitegemea kuliko kusumbua home, huyu mtoto wa watu nataka kumsaidia, nataka asiwe mbali na Mimi kusudi Mambo yangu yaki tiki niishi nae,

Kwa Sasa nimemuombea hifadhi kwa Dada yangu japo ya siku kadhaa na tayari Nina siku tano tu mbele za kujua hatma yake.

Nawaza nifanye Nini?? Nimtafutie nauli arudi kwao?? Nikae nae kibishi, atakula Nini? Ana mahitaji mtoto wa kike na Mimi Ni hohe have?? Naomba ushauri wakuu.
Natanguliza Shukrani.
Ww mchukue ukae nae, Alf utaona akil itakavyochanganua nn cha kufnyaje, mbn utaona mishe nyng tu ktaan
Kila la kheri
 
Ataitoa wapi sasa ikiwa ye mwenyewe ni jobless
wanaume wengi wa dar huwa wanakosa sababu ya kupata maendeleo kwa kukosa wa kuwapush,

akikaa siku 2 na mtoto wa watu ndani atapata tu akili ya kwenda kutafuta.

sinza kuna watu wanaishi chumba na seble mpka 500k kwa mwezi na hawana kazi maalum lakin wanapambana na kusurvive tena kwa issue za halali kabisa

maisha ni kutoka na kujichanganya ukijifungia ndani na yenyewe yanakufunga
 
Wazi kabisa mkuu
 
Mtaftie nauli arudi kwao ndo kitu pekee utachomsadia kwa Sasa

Unakula kwa shkamoo usiongeze changamoto nyumbani

Jambo ilo likutie nguvu uanze MWAKA kwa kasi

Mungu akubariki
Ahsante kwa Ushauri Ndugu yangu
 
Ww mchukue ukae nae, Alf utaona akil itakavyochanganua nn cha kufnyaje, mbn utaona mishe nyng tu ktaan
Kila la kheri
Shukrani Mkuu, Lakini kabla ya uwepo wake kaka nimesambaza San CV mpaka nazikuta kwenye vifungashio vya vitumbua,

Ingekua kijijini ningetumia Mafunzo ya JKT kuanzisha kilimo Cha mboga mboga
 
wanaume wengi wa dar huwa wanakosa sababu ya kupata maendeleo kwa kukosa wa kuwapush,

akikaa siku 2 na mtoto wa watu ndani atapata tu akili ya kwenda kutafuta.

sinza kuna watu wanaishi chumba na seble mpka 500k kwa mwezi na hawana kazi maalum lakin wanapambana na kusurvive tena kwa issue za halali kabisa

maisha ni kutoka na kujichanganya ukijifungia ndani na yenyewe yanakufunga
Brother, upo sahihi binafsi nakosa wa kuni push nipate hata temporary mishe wakati najiweka sawa.
 
Unaposema huna maisha kwani umekufa ? ...Pambana kijana ambao hawana maisha wapo futi sita chini
Sahihi mkuu, Acha nipambane.. lakini kwa wakati huu nifanye Nini mkuu? Nimtafute nauli au nikomae nae tu?
 
Shukrani Mkuu, Lakini kabla ya uwepo wake kaka nimesambaza San CV mpaka nazikuta kwenye vifungashio vya vitumbua,

Ingekua kijijini ningetumia Mafunzo ya JKT kuanzisha kilimo Cha mboga mboga
Wengne wanakuwa km baraka ila kmbka wengne km laana kwhyo kaz kwako mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom