Nampenda lakini simuelewi. Ushauri pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nampenda lakini simuelewi. Ushauri pls

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwana Mpotevu, Oct 23, 2011.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Jamani naombeni ushauri wa dhati katika hili, ni jambo langu mwenyewe. Kuna mdada nampenda sana na nina mwaka mmoja tupo katika mapenzi. Mara kwa mara amekuwa akinishutumu kuwa eti bibi zangu wanamsumbua na nikimwambia anitajie huyo anayemsumbua amekuwa hasemi. Mimi najijua fika kuwa sina mwanamke mwingine ambaye niko committed naye wa kuweza kufikia hatua ya kumsumbua. Nimemvumilia najua labda ni mapenzi tu. Wiki mbili zilizopita alinipigia simu akiniuliza nimwambie kama kweli nampenda kwa dhati ili asijilaumu na maamuzi yake. Nikamwambia ni kweli nampenda kwa dhati. Akasema anashukuru kwa jibu langu maana kuna mtu anamsumbua. Nikamuuliza nani anamsumbua na kwa kipi anachomsumbua, hakuniambia na akazima simu na kupotea kama siku tatu nne bila kupatikana. Kwa sasa nimekaa kimya natafakari na sijui nimuelewe vipi. naomba mnisaidie kama ni mwanamke anayenifaa kweli au la. Nisaidieni tafadhali ukweli ni kwamba ninampenda sana ingawa nashindwa kumuelewa na bahati mbaya sana tuko mikoa tofauti kwa sasa
   
 2. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  ni PM namba yake nikulainishie mkuu,afta 3 days beliv me atakuwa kwnye mstari!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  She is probably playing mind games with you. My advice to you: just slow your roll.
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama unampenda na yeye anakupenda itakua sawa tu. Mtafute uongee nae. Hata mimi nimepata shaka hapo uliposema "Mimi najijua fika kuwa sina mwanamke mwingine ambaye niko committed naye wa kuweza kufikia hatua ya kumsumbua"

  Maana yake nini? una wengine ila haupo committed sana? kama ni hivo basi faham kwamba hao hao wanaweza kusumbua pia. Inawezekana ikawa ni rafiki zako, au hata ndugu zako ambao hawajafurahia penzi lenu. Kaa na mwenzio, hakikisha akakwambia ni kitu gani kinaendelea na try to identify who is behind all this. from there utaona itakua ni rahisi kuhepuka matatizo yenye kutokana na usumbufu huo
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  NN Thanx for ur advice, kwakweli sina raha maana nampenda sana nadhani hajjui how much I love her
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  RR ukweli ni kwamba uhusiano wangu na yeye wala haujulikani kwa ndugu zangu ila naamini ndugu zake wanaweza kuwa wanajua maana nimewahi kuongea na ndugu zake kadhaa. Niko mkoani naye yuko dar na tumekuwa tukikutana mara chache kwa kutembeleana. Hakuna hata rafiki yangu anayemjua sanaaaaa kwa sababu ya umbali lakini ukweli nampenda sana. nachanganyikiwa hasa aliposema kuna mtu anamsumbua so anataka kujua kama mie kweli nampenda au la. nikajiuliza maswali mengi bila majibu. sina mwanamke yoyote kwa sasa (mpenzi) to be frank ndo maana nashangaa sana anaposema eti bibi zangu wa zamani wanamsumbua ingaw ahanitajii akisema anafanya upelelezi kwanza
   
 7. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kuna moja kati ya haya mawili:
  1.Anakupima ili afahamu ni kwa kiwango gani unampenda.
  2.Anatafuta upenyo wa kukutema.
  Take care!
   
 8. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kaka uko kwenye mizan ya huyo Mdada,anapesema kuna mtu anamsumbua sana na hatak kujutia maamuzi yake ni kuwa kuna mtu anamkatalia kwa ajili yako though anampenda,na kukuchunia 4 foru days,hiyo ni alert tosha kichwan mwako kuwa kuna ka mchezo nyuma ya pazia,ushauri wa NN ni wa muhimu kuzingatia,be carefull, usilie lie kila ukiongea au ukiwa nae,be confident and show her that you love her though you can continue with your life without her, na log off....
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna mtu anamsumbua....ina maana nyingi sana
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Bosi unaweza ukafafanua pls maana hata mie hiyo kitu inanisumbua sana. nisaidie mawazo mkuu
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakushukuru sana kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi. Thanks again
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nielewavyo mimi kama mwanamke anasema kuna mtu anamsumbua halafu anakuwa haeleweki basi nachelea kusema atakuwa mwanaume ambaye anashindwa kumpa jibu sahihi kwa hofu yako lakini element zote za kumpenda zipo. Hiyo ya kuwa bibi zako ni kitu kidogo tu, anataka kucheza na saikolijia yako ili ajue kama una mademu wengine. Hivyo mchunguze huyo demu wako kuna mtu anampima kwenye mizani akikushinda tu utasikia puuuuuuu kama kama kishindo cha mabomu ya Gongo la Mboto kutahamaki huna chako, inabaki historia. Akihangaika akiona nako kimewaka atarudi kwako na kukuomba msamaha ili mrudiane, kwa kuwa ulikuwa bado unampenda unaweza kujikuta unafanya ndivyo sivyo. Tafakari chukua hatua.
   
 13. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #13
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Tatizo kujua if it is 1 or 2 or both
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mzee wa Rula inawezekana kabisa kweli huyu mdada anatuweka kwenye mizani maana nashindwa kabisa kuelewa pale anapodai eti kuna mtu anamsumbua halafu hasemi ni nani na badala yake anataka uhakika wa penzi langu kwake. Itabidi nadhani nimkalie kooni nijue moja na achague moja, kusuka ama kunyoa
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni uhakika upi anaoutafuta yeye wakati nyie ni wapenzi na bila ya shaka umeshamwambia utaishi nae. Kuna kitu hapo anakitafuta.
   
 16. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huyo anataka akuteme-sema hataki yeye kuwa source ya kuachana,anataka akuache then kesi akupe wewe kuwa ndo ulisababisha,
  atakuwa na mwingine huko aliko.
  hio ndio tatizo ya kuwa na distance relationship
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Fanya kitu kimoja Mkuu,mwambie kwa upole kabisa,"Sioni Faida ya kuwa katika mahusiano ambayo hayaoneshi futre yeyote zaid ya Quaral za kila siku, nimemua nikupe nafasi ya wewe kukaa na kufanya Maamuzi Sahihi,ukiwa Tayari utanijibu,kwa sasa nimeamua niwe apart na wewe mpaka hapo uakapoamua kueleweka", Some times its better to distant from people just to make them realize how important you are in their life, We mpe nafasi bwana ,kama ni wako atarudim if it was not meant for you then it will be much fine Kaka, acha kulia lia Boss.
   
 18. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #18
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Bramo nimekuelewa nadhani hiyo ndio njia inayoweza kusaidia kujua msimamo wake na kama kweli ananipima kwenye mzani basi afanye maamuzi ama mimi ama huyo mwingine. I think this is the right thing to do
   
 19. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #19
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  labda kama anataka kujua reaction gani nitakayoichukua kwa jinsi anavyoichezea akili yangu
   
 20. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #20
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Sasa nadhani sina namna zaidi ya kumwambia wazi aseme anachotaka na achague moja kama kuendelea nami au huko aliko kama ana mwingine basi aendelee nae nisijikute napoteza muda kwa kuchanganywa
   
Loading...