Nampenda lakini simuelewi kwa tabia zake

Haya majina yenu mara nyingine yawe yanasadifu uwezo wenu wa kufikiri na kufanya maamuzi ingawa hakuna aliyesahihi, ila kuna maamuzi waweza yafanya sahihi kabisa. Badili jina kwanz halaf uendelee kuwepo
 
...wanawake wamejaa tele siku hizi..sioni sababu ya kuzinguana kwenye penzi....kama hamuelewani yanini kugandana?...maisha ya kiafrika haya kudanganyana...ishi kizungu..chukua time tafuta anaekufaa...
 
Dawa ya mwanamke anayetingisha kiberiti ni wewe kuuwasha tu. Wanawake wote hawa unaumiza kichwa na mmoja. Wanawake wanapenda wanaume confident. Akisema muachane mwambie poa halafu ignore her.
 
Tengua tu uteuzi hapo hamja jinsi mshachokana ukiona hvyo anza kujiondoa mdg mdg tu maana utateseka sana na atazidi kukunyanyasa zaidi
 
Huyo naona anatishia kujamba wakati ana tumbo la kuharisha, achana naye, huenda kuna tudume twingine tunammendea na kumpa kichwa. Mara nyingi wanawake wako tayari kupotezewa muda na walaji kuliko waoaji, na muda unapowaishia huanza kujuta, wanasahau Kuwa wazuri kila siku wanazaliwa na wengine kila siku wanapevuka.
 
Za asubuhi ndugu zangu..

Natumaini mmeamka salama.

Ndugu zangu, dhumuni la kuleta uzi huu hapa jamvini ni kuomba msaada
hali ya mahusiano yangu imefikia pabaya.

Na sijui nafanyaje mpenzi wangu huyu amekuwa ni mtu wa visirani visivyo isha na majibu machafu hata kwa kosa dogo nilijaribu kumuonya kwa miaka miwili sasa tuliyokuwa kwenye mahusiano lakini hajirekebishi.

Kama binadamu wengine kuna makosa madogo madogo kama kuchelewa kufika eneo fulanu kutokana na kubanwa na shughuli na vingine vingi. Ila ninachoshindwa kumwelewa huwa ananijibu hovyo alafu anakimbilia kuachana kuliko kawaida kosa dogo amekimbilia kuachana sio mtu wa kusamehe anabeba visasi mno ukumkosea leo anakumbushia na ya zamani nimemvumilia lakini sasa nachoka nimesha jaribu kuongea na mzazi wake dada zake waongee nae.

Ata pretend wiki moja yuko sawa lakini baada ya hapo anarudia tabia zake nikijichunguza mimi sina kosa sijawahi hata kumsaliti nimekuwa mwanifu kwake lakini yeye hataki kuelewa kiburu kimemjaa nimemsaidia mambo mengi kwenye maisha yake, haswa kutokana na hana kazi ya kueleweka lakini naona juhudi zangu hatambui.

Akitishia kuachana nikikubali kukaa kimya baada ya wiki ananitafuta anaomba msamaha ("huwa anadai kuwa anachanganyikiwa mpaka kufikia hiyo hali ya kuniacha alafu baadae ndio anashtukia kuwa amenikosea, anadai kuwa ananipenda").

Naombeni ushauri ndugu zangu, nifanyaje?
Nikifanya reference na ule uzi wako mwingine..

Uyo mwanamke ndio yule mama yako hamtaki?
 
Mahusiano mahusiano ni kitendawili. Kila mhusika ana jibu la tofauti.
 
achana nae ukatafute malaika ...tofauti na hapo nobody is PERFECT even YOU
 
Back
Top Bottom