Namna ya kutibu mshituko wa moyo

Namna ya kutibu mshituko wa moyo

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
b7b155d280b296a2ac6f5eb7ea1fefb3_L.jpg

Mshituko wa moyo unahitaji kushughulikiwa haraka. Kama unamshuhudia mtu akipatwa na mshituko wa moyo unapaswa kuomba msaada haraka au kumfikisha kituo cha afya haraka iwezekanavyo. Kama mtu aliyepatwa na

mshituko wa moyo amepoteza fahamu, baada ya kuomba msaada kituo cha afya cha karibu, unapaswa kumfanyia CPR mara moja kama unajua kufanya hivyo. CPR ni kitendo ambacho husaidia kufikisha hewa ya oksijeni katika

ubongo. Kwanza hakikisha njia za hewa za mgonjwa ziko wazi, yaani hakikisha mdomoni na puani kwake hakuna kitu kinachozuia hewa kupita na msaidie kwa hewa kila baada ya kumkandamiza kifuani au (chest compress)

mara 30. Kama hujuia CPR pia unapaswa kuanza kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepoteza fahamu kutokana na mshituko wa moyo, kwani kufanya hivyo huenda kukaokoa maisha yake. Tutaelekeza hapa jinsi ya

kumkandamiza kifuani mgonjwa aliyepatwa na mshituko wa moyo na aliyepoteza fahamu. Weka kiganya cha mkono wako mmoja katika mfupa wa kifua (chestbone) katikati ya matiti na kiganya cha pili juu ya cha kwanza, na

kandamiza kwa kiasi cha inchi mbili au sentimeta 5 kuelekea chini. Eendelea kukandamiza na kuachia mara 30. Kama unajua namna ya kufanya CPR mfanyie mgonjwa na kama hujui endele kumkandamiza sehemu hiyo ya kifua hadi msaada utakapowasili au hadi mgonjwa atakapopata fahamu au kuonyesha dalili za kupumua.

MATIBABU.

​
Matibabu ya ugonjwa wa mshituko wa moyo hufanyika hospitali kwa njia tofauti kulingana na hali ya mgonjwa. Kila dakika inavyopita baada ya kutokea mshituko wa moyo, ndivyo tishu ya moyo inavyopoteza oksijeni na kuharibika au kufa. Njia kuu ya kuzuia moyo usiharibike ni kurejesha tena haraka mzunguko wa damu. Mgonjwa wa mshituko

wa moyo huweza kutibiwa kwa dawa au njia nyinginezo za tiba kwa kutegemea jinsi gani tishu ya moyo ilivyoharibika. Dawa tofauti zinazotumika kutibu mshituko wa moyo ni kama aspirin, dawa zinazoyeyusha damu ili

kuondoa damu iliyoganda ambazo huitwa kitaalamu kama clot buster, dawa aina ya heparin na nyinginezo ambazo hutofautiana kutokana na utendaji wake mwilini. Baadhi ya wakati athari za mshituko wa moyo huwa kubwa ambapo mgonjwa hutibiwa kwa njia inayoitwa Angioplasty. Hiyo siyo operesheni bali ni matibabu ya

kufungua mishipa ya damu iliyoziba au kudhoofika na kusabisha mshituko wa moyo. Mara nyingine wagonjwa wa heart attack hutibiwa kwa upasuaji unaoitwa bypass surgery.

Baada ya kujua namna ya kutibu mshituko wa moyo, sasa tuangalie ni jinsi gani tunaweza kujiepusha na ugonjwa huo wenye madhara makubwa kwa miili yetu.

Kwa wale ambao tayari wameshapatwa na ugonjwa huu pia wanashauriwa kuendelea kutumia dawa walizopewa hospitalini lakini pia kubadilisha mienendo ya maisha yao ili kuzuia kupatwa tena na mshituko wa moyo katika siku

zijazo. Kwa wale ambao mshituko wao wa moyo umesababishwa na magonjwa mengineyo waliyonayo kama matatizo mengine katika moyo au maradhi tofauti, wanatakiwa kutibiwa maradhi hayo. Lakini kwa ujumla tunaweza

kujiepusha kupatwa na ugonjwa huo kwa kutovuta sigara, kudhibiti hali nyinginezo kama shinikizo la damu, ongezeko la mafuta ya kolestroli mwilini na kisukari. Suala jingine linaloweza kuzuia kupatwa na shinikizo la damu

ni kuushughulisha mwili kila mara na kufanya mazoezi, kupata lishe bora, kupunguza uzito uliopindukia wa mwili na kupunguza ua kujiepusha na wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.

Kama ndio kwanza unafungulia redio yako mpenzi msikilizaji kilichopo hewani ni kipindi cha Ijue Afya Yako kinachowajia kupitia Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mada tunayozungumzia ni mshituko wa moyo. Kama wewe ni mvutaji wa sigara, tafadhali acha kuvuta sigara ili ujiepushe kupatwa na heart

attack na kama unaishi katika mazingira ambayo kuna mtu au watu wanaovuta sigara, basi washauri wenzako waache kuvuta sigara kwani sio tu tabia hiyo huathiri afya zao bali yako wewe pia. Vile vile matumizi ya tumbaku

yana taathira kama ya sigara kwenye moyo. Tunashauriwa kufanya mazoezi kwa uchache dakika 30 kwa wiki ili kujiepusha na ugonjwa wa moyo. Mazoezi hayo yanaweza kuwa ya aina yoyote hata kutembea kwa mguu. Hii ni katika hali ambayo, lishe ina nafasi muhimu katika kuwaepusha watu kuwa na unene wa kupindukia na hivyo kutokupata mshituko wa moyo.

Dakta Linda Van Horn mtaalamu wa lishe na mjumbe wa Kamati ya Lishe ya Jumuiya ya Moyo ya Marekani ambaye pia ni mhadhiri wa tiba ya kuzuia maradhi katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Northwestern huko Chicago anashauri kuwa, ili kujikinga na mshituko wa moyo tunapaswa kula vyakula vyenye ufumwele kwa wingi na

visivyokuwa na mafuta mengi ili kuimarisha afya ya mioyo yetu. Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yasiyo na madhara au unsaturated fats kama vile fati asidi za omega 3 na mafuta ya zaituni huweza kusaidia kupunguza

kiwango cha mafuta yenye madhara katika miili yetu, kuzuia damu kuganda na pia kufanya chembe za mafuta zisigande katika mishipa ya damu. Lishe iliyo na ufumwele ambayo mara nyingi hupatikana katika nafaka, baadhi

ya matunda na mboga, husaidia kupunguza kolestroli aina ya LDL ambayo ni hatari kwa miili yetu. Baadhi ya vyakula vyenye uwezo wa kuimarisha afya ya mioyo yetu ni samaki hasa aina ya sardine na salmon. Samaki hao wana kiwango kikubwa cha omega 3 pamoja na calcium na niacin ambazo ni virutubisho muhimu kwa afya zetu. Chakula kingine ni shayiri yenye ufumwele kwa wingi na pia huupatia mwili nguvu kwa haraka na kuzuia njaa kwa muda mrefu.

Wasikilizaji wapenzi utafiti umeonyesha kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo. Utafiti huo uliotolewa katika Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo

la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza kwamba kunywa kikombe kimoja cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30. Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa

kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake yanaweza kuwa kinyume. Utafiti mwingine umeonosha kuwa, kufanya mazoezi kwa muda mrefu hakuhusiana na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Huko nyuma kulikuwepo

tafiti zilizoonesha wasiwasi wa afya ya mishipa ya moyo kwa baadhi ya wanamichezo wa Olimpiki. Tafiti hizo zilisema kwamba, kupanuka kwa mioyo ya wanamichezo kunakoitwa kitaalamu "athlete's heart" huufanya moyo kuwa dhaifu sana na kushindwa kuvumilia mazoezi mazito. Lakini kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa kwenye

jarida la Marekani la Kitengo cha Magonjwa ya Moyo, mazoezi mazito hayana hatari kwa afya ya moyo. Kiwango cha damu inayosukumwa katika miili ya wanamichezo hakibadiliki wakati wa mazoezi. Mbali na kupanuka kidogo baadhi ya sehemu za moyo, misuli ya moyo hubakia sawa wakati wa mazoezi. Wanasayansi wamehitimisha

kwamba, mioyo ya wanamichezo ina afya nzuri na inaweza kuvumilia kirahisi mazoezi ya kiwango cha juu. Pia wamesema kwamba, baadhi ya dawa kama vile erythropoietin (EPO) zinazotumiwa na wanamichezo hao ili kuzipa nguvu chembe chembe nyekundu za damu, kunaufanya utendaji kazi wa moyo udhoofu, suala ambalo limekuwa likiwaathiri wanamichezo hao na wala sio mazoezi mazito ya mwili wanayoyafanya.

Naam wapenzi wasikilizaji, kabla hatujahitimisha kipindi chetu sio vibaya ukijua kuwa, moyo ulioko katika kifua cha mwanadamu hupiga mara 100,000 kwa siku, husukuma galoni mbili za damu kwa dakika, galoni 120 kwa saa na

hufanya hivyo kwa masaa 24 kwa siku, miezi na miaka yote mwanadamu anayoishi duniani. Mfumo wa mishipa ya damu ambayo

husafirisha damu katika mwili wa binadamu ina urefu wa maili 60,000. Ukubwa huo ni mara mbili zaidi ya mzunguko wa dunia!

Suala la kustaajabisha zaidi na unalopaswa kujua kuhusiana na kiungo hiki muhimu katika mwili wa binadamu ni kwamba moyo huanza kupiga katika mwili wa mtoto mchanga pale anapoumbwa tumboni, hata kabla ubongo haujaumbwa. Moyo huanza kupiga kabla hata ya mfumo wa fahamu wa kati kuumbwa! Kuna nadharia maarufu

kwamba mfumo wa kati wa fahamu (CNS) hudhibiti na kusimamia vitendo vyote vya mwanadamu kuanzia kwenye ubongo lakini utafiti umeonesha kwamba mfumo wa fahamu hauanzishi mapigo ya moyo. Kiuhakika mapigo ya

moyo huanza yenyewe na kuna wanaosema kuwa bado haijafahamika mapigo ya moyo huanzishwa na nini. Wataalamu wanasema kuwa moyo ni kituo cha ufahamu (consciousness) na wala sio ubongo kama wengi tunavyodhani. Daima tuzilinde afya zetu!
 
Asante mkuu MziziMkavu.... Hivi huo mshtuko wa moyo ndio kuzimia au??? Make kuna watu huwa wanazimia kwenye matukio hasa misiba au kwenye mikusanyiko yenye watu wengi. Je hao pia wanaweza kupatiwa huduma ya kwanza kama uliyoitaja hapo juu???
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu MZIZIMKAVU kwa kutupatia elimu nzuri sana mshituko wa moyo ni ugonjwa ambao nao unaojitokeza mara kwa mara , bila kuwa na elimu hii tunaweza kupoteza ndugu zetu hata kwa magonjwa ambayo yako ndani ya uwezo wetu wa kawaida tu. :yell:
 
Nilishafuzu hii kozi kitambo sana. Ahsante Mh. waziri ila tatizo linakuja unapokuwa mjini then mtu anaanguka mbele yako, utamsaidiaje? Maana humjuwi na kwa hali ya sasa ya kuwa karibia kila mtu ana ngoma utaanzaje kumpumulia hewa? Ni maoni yangu tu na yananisumbua kweli kwani mara nyingi nawaza hivyo.
 
Hivi usubi ni ugonjwa gani?
[h=1]UGONJWA WA USUBI UNGALI UKISAMBAA[/h]MATIBABU YAKE NI RAHISI LAKINI UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA
Nchi zaidi ya 35 zilizo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa usubi zimehimizwa kuongeza kasi ya kupambana na ugonjwa huo ili kuweza kuutokomeza.
Hii ni pamoja na kuweka mikakati mipya ya kuzuia, kutibu na kuwahamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambayo yanashambuliwa na ugonjwa huu wachukue tahadhari ikiwa ni pamoja na kumeza dawa za kuzuia ugonjwa huu na mapema.
Mkutano huu kwa upande mwingine ulionesha utashi mkubwa wa kisiasa kutokana na kuwa hata watawala na wanasiasa walihudhuria na kutoa ahadi za kuendeleza mapambano dhidi ya adui usubi.
Ndio maana mkutano huo ukawaleta kwa pamoja mabingwa kutoka sekta za afya kutoka nchi mbalimbali, zaidi ya mawaziri 20, wasomi na wanasiasa kutoka zaidi ya nchi 25 zilizo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania binafsi ndiye aliufungua mkutano huo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Desemba 2006, naye akianisha madhara ambayo tayari yamesababishwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watanzania.
Kwa mujibu wa takwimu za mabingwa wa afya kwenye mkutano huo tayari mataifa 35, yanasumbuliwa na ugonjwa huo.
Mataifa 28 kati ya hayo ni ya ki-Afrika. Jumla ya watu wanaougua ugonjwa huo kote ulimwenguni hivi sasa wamefikia milioni 18.
Ugonjwa huu hutokana na minyoo aina ya onchecerca volvulus na kusambazwa na inzi weusi majike wadogo-wadogo mithiri ya mbu wajulikanao kama simulium. Mbu hawa huzaliana kwa wingi kwenye maeneo yenye vijito au mito yenye maji yatiririkayo kwa kasi.
Wadudu hawa wana uwezo wa kuruka hadi umbali wa kilometa 400. Waziri wa Afya wa Tanzania na maendeleo ya Jamii Profesa David Mwakyusa anasema licha ya kuwa wadudu hawa wana umbo linaloshabiriana sana na la mbu lakini tabia zao ni tofauti kabisa.
"Kwa sababu wao wanapendelea kuzaa kwenye miamba ambapo kuna maji yanapita haraka.
Ambapo hawa mbu wanaoeneza malaria kama unavyojua wanatafuta maji ambayo yametuama kwa hiyo katika maeneo ambayo kuna mito ambayo ina maji ambayo yana kwenda haraka ndo unawapata". Anasema waziri na kuyataja maeneo ambayo wanapatikana wadudu hawa sakili kwa hapa Tanzania kuwa ni kwenye mikoa ya Tanga, na Morogoro.
Akizungumza na idhaa hii Waziri huyo alionya kuwa hali ya kusambaa ugonjwa huu inazidi kuwa kitisho na kuwa matokeo yake badhi ya watu wameanza kuhama maeneo yao hali anayodai inarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi Tanzania.
Waziri anadokeza kuwa licha ya tatizo hilo kuongezeka Tanzania halijafikia kiwango cha baadhi ya nchi za Afrika Magharibi.
"It is the disease of the pure" anasema waziri kwa lugha ya kiingereza akimaanisha kuwa ni ugonjwa wa watu maskini, na kuongeza. " kwa hiyo unaanza kuwa na uchumi ambao ni hafifu halafu ukiongeza na matatizo kama hayo ndio unazidi na kama nilivyo eleza kwenye hotuba yangu tunayajua maeneo ambayo watu walikuwa wanalima lakini kwa sababu mito waliyokuwa wanaitumia ina mbu wengi hao na wao wamegundua kuwa hiyo ndio inatuletea upofu basi wanahama".
Wataalamu katika mkutano huu wa Dar es salaam kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa kupambana na ugonjwa huu kwa ushirikiano wa nchi zote zilizo katika mapambano au jirani ili kwa pamoja waweke kuweka mikakati ya kutokomeza adui usubi.
Hii bila shaka inatokana na ukweli kuwa ikiwa nchi moja itafanya juhudi za peke yake hata nchi hiyo ikifanikiwa yanaweza yasiwe mafanikio ya kudumu kwani ugonjwa huo unaweza kuingizwa tena kutoka nchi nyingine.
Mfano kamili ni nchi ya Kenya ambayo inadai iliteketeza ugonwa huu taklibani miaka 50 iliyopita lakini hivi sasa ugonjwa huo unatishia kurudi nchini humo kutokana na ujiro wa wakimbizi.
Hivyo ndivyo Dr. David Sam alivyoiambia Deutsche Welle alipokuwa akielezea hali ya ugonjwa wa usubi nchni Kenya.
Hata hivyo Dk. Sam anasema juhudi zinazofanywa na nchi yake ni kuhakikisha ugonjwa huo hausambai tena kwa wananchi. " Tumejaribu kuzuia hao sisi sana kwa raiyaa lakini mahali refugee wako sio rahisi kusambaza huo ugonjwa".
Njia inayopendekezwa na wataalamu katika kudhibiti ugonjwa huu ni kuwapa watu wote walio kwenye maeneo wanapopatikana wadudu hawa dawa ya kutibu na kuzuia usubi.
Waziri Mwakyusa anasema hii ndiyo njia rahisi ya kupambana na hali hii hasa ikilinganishwa na ikiwa serikali ingeamua kumpima kila mtu ili wapatikane watu wenye vijidudu vya usubi na kasha wapewe dawa.
Na tena njia hii inafikiriwa kuwa bora kwani dawa hizi hazimdhuru mtu ambaye labda amezimeza wakati hana vijidudu vya usubi.
" Kwa hiyo tunachofanya katika maeneo ambayo tunajua kuna huo ugonjwa tunawapa dawa mara moja kila mwaka" anasema waziri Mwakyusa na kuongeza.
"katika kila mwaka kuna tarehe ambayo tumeweka. Tunajua wanakuja wote, wanapewa watu wote wadogo kwa wakubwa, tunarudi tena mwaka kesho kwa miaka mitatu mfululizo. Tegemeo lote ni kuwa tutakuwa tumemaliza baada ya kufanya hivyo".
Mkutano huu wa Dar es salaam Joint action forum, ni wa 12 kwa maana maana mikutano kama hii imekuwa ikifanyika na kupitisha maadhimio. Swaku ambalo mtu anaweza kujiuliza ni mafanikio gani ambayo yamefikiwa? Waandishi wa habari walimuuliza waziri Mwakyusa ambaye anajibu.
" Kwanza umoja wenyewe ni …..wa family moja wenye matatizo mamoja, tumekuja pamoja. programu hii ilianza Afrika magharibi na nchi zipataozo 11 tu.
Lakini kama ulivyosikia leo hii hapa tupo 36 kwa hiyo watu wakigundua na wenyewe wanajiunga tunabadilishana nao mawazo".
Binafsi nilimuuliza Waziri Mwandosya kuwa ikiwa inajulikana wazi kuwa wadudu hao ndio hueneza usubi kuna juhudi zozote za kujaribu kuteketeza nzi hao naye akajibu " Ndio na hapana. Huko tulipoanza mimi nikiwa bado mwanafunzi tulikuwa tunapiga spray ya dawa kwenye mito lakini unajua hiyo ni ngumu sana umetia dawa ya kutosha dawa inakwenda.
Kwa hiyo tukaona kwamba njia ambayo ni rahisi zaidi ni kuviua hivi vijidudu visiwepo kabisa.
Manake huyu mbu akikuuma hatapata kitu.
Tunaweza tukafanya lakini unaangalia kitu kinaitwa cost effectiveness unapotia hela kiasi hiki, unavuna kiasi gani kutumia mpango tofauti" anajibu waziri Mwandosya.
Wataalamu wanasema kuwa tangu mtu anapoumwa mbu mwenye vimelea vya ugonjwa huo hadi ugonjwa huo kujitokeza inachukua muda wa tangu mwaka mmoja hadi miwili.
Katika kongamano hilo aliletwa Bi Miriana Fernand. Mwanamama huyo alishambuliwa na ugonjwa huo kwa miaka mingi na kila mara alipobeba mamba ilitoka. Afya yake kwa ujumla ilizorota. Baada ya kupata matibabu hivi sasa amepona na tayari ana mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na nusu.
Mama huyu aliwaonyesha waandishi wa habari sehemu ya miguu yake. Ingali na madoa kama ya chui licha ya kuwa yeye anadai madoa hayo yamepungua baada ya kupatiwa tiba.
Dalili za ugonjwa huu hujitokeza kwa binadamu katika sura 3 tofauti.
Kwanza ni kwenye ngozi ambayo huwasha sana, hupata upele na ukurutu , huvimba na kuwa kama ya mtu mwenye ukoma, hukakamaa na kuwa ngumu , huchakaa na kulegea, ngozi huwa na madoa madoa kama chui, ngozi huota vinundu. Kwenye mwili na ubongo kwa wagonjwa wachache ukuaji wa mwili na ubongo huathirika na kusababisha kudumaa vile vile kifafa kinaweza kutokea.
Kwenye macho mazalia ya filarial hudhuru macho na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kuona na hatimaye kusababisha upofu.
Takwimu za shirila ka Afya Ulimwenguni zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 85 wapo kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo katika nchi 27 za bara la Africa na nchi 6 za bara la Amerika ya kati ya Kusini.
Watu milioni 18 wamekwishia kuabukizwa kati yao watu milioni 1 wana shida ya kuona, na zaidi ya laki 4 wana upofu.
Hapa nchini Tanzania watu milioni 4 wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu katika mikoa ya Ruvuma, wilaya zote, Morogoro; wilaya zote, iringa ; wilaya ya Ludewa na maeneo mengie yatachunguzwa. Tanga; wilaya za Korogwe, Lushoto na Muheza Mbeya ; wilaya za Rungwe na Kyela.
Mpango wa kudhibiti ugonjwa huo nchini Tanzania ujulikanao kama National Onchocerciasis Controal Programme NOCP ulizinduliwa rasmi mwaka 1998 na unaendeshwa na wizara ya Afya chini ya Idara ya kinga.
Muundo wa NOCP unaenda sambamba na muundo wa mabadiliko ya sekta ya afya Health Sector Reform katika ngazi ya Taifa kuna kamati maalumu ya kudhibiti ugonjwa wa usubi, National Onchecerciasis Task Force NOTF ambayo majuku mu yake makubwa ni kufuatilia utendaji wa kazi zote zinazohusu udhibiti wa ugonjwa wa usubi nchini.
Dawa ambayo inatumika kutibu ugonjwa huu na iliyopigiwa sana upatu ni ile iitwayo mectizan ambayo hupewa mtu mara moja kwa mwaka kwa kipindi kisichopungua miaka 15 mfululizo.
Mwisho.@Bujibuji
 
Back
Top Bottom