Namna ya kurusha ndege....

Namna ya kurusha ndege....

Vawulence

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
1,944
Reaction score
2,145
Jamaa flani Msafishaji wa Ndege
aliokota kitabu kimeandika; 'JINSI YA KUPELEKA NDEGE' wakati anasafisha ndege moja.

Akafungua ukurasa wa kwanza akasoma, "Ukitaka ndege iwake bofya kitufe chekundu."
...Akabofya
ndege ikawaka.

Akafungua ukurasa wa pili, akasoma tena, "Ukitaka ndege
ianze kutembea bofya kitufe cha Blu."
...akabofya
ndege ikaanza kusonga.

Akafungua ukurasa wa tatu akasoma, "Ukitaka ndege ipae boyfa kitufe cha manjano."
...akabofya ndege ikapaa.

Jamaa akacheka na kusema, "Hahaha, pumbav, kumbe kupeleka ndege rahisi hivi! Hawa marubani huturingia bure!"

Baada ya kukaa angani kwa muda akaamua atue...akafungu-a ukurasa wa nne ili asome jinsi ya kutua akapata kumeandikwa , 'KWA MAELEZO YA KUFANYA NDEGE ITUE, TEMBELEA CHUO
CHETU UFANYE COURSE YA MIAKA 5.'
 
E e e kumbe kitabu kilikuwa trial version si angekuja Jf angeelekezwa wapi apate full cracked hahaha
Sent from My Ujala using Jamiiforums
 
haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa uwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiii lanyee kafwa
 
Hapo ni kusubiri mafuta yaishe ndege yenyewe ingeanza kushuka bila hata yy kuhudhuria hiyo kozi, na ndoto yake ingetimia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom