Namna ya kuondoa hacking ya simu

Namna ya kuondoa hacking ya simu

Ctr

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
505
Reaction score
228
Nimekuwa muhanga kwa muda mrefu kwa tatizo hili, kuna mtu anaingilia mawasiliano yangu ya simu hasa call za simu, messeji na whatsap na facebook,nimehangaika kwa muda mrefu sana nimejaribu kubadilisha simu lakini tatizo liko palepale, nimejaribu kubadilisha line ya simu tatizo liko palepale, nimejitahidi sana lakini nimekuwa sina namna
 
Pia tengeneza nywira imara na achana na kufuata viunganishi usivyo husika navyo email mpya na nywira strong Itakusaidia
 
Kama unatumia smart4ne angalia kwenye list ya apps zako ambayo huielewi remove it, additionaly epuka kufungua ma links and other attachements usizo zielewa
 
Nashukuru kwa michango yenu ila kiukweli nishafanya hard reseting nikabadilisha nywira lakini wapi bado amezidi kuingilia mawasiliano, kibaya zaidi mtu huyo anaexpose mambo yangu ya kifamilia
Pole sana unatumia simu gani
 
Mchawi ni mtu wako wa karibu ambaye ana access na simu yako.... tunza simu yako kama korodani yani haishiki mtu tofauti na wewe....usifungue link yoyote kwa muda ....tumia app popular tu kama whatsapp n.k
 
Pole sana...

Badilisha email yako...

Alafu jaribu kuchepusha majina yako kidogo ili isiwe rahisi kwa huyo anayekudukua kukuotea...

Cc: mahondaw
 
Mchawi ni mtu wako wa karibu ambaye ana access na simu yako.... tunza simu yako kama korodani yani haishiki mtu tofauti na wewe....usifungue link yoyote kwa muda ....tumia app popular tu kama whatsapp n.k
Aisee nitauchukua ushauri wako mkuu
 
Fanya ukaguzi mzima wa simu yako...hakikisha unatumia email yako na si vinginevyo.....halafu ingia setting kisha angalia kama device administrator imesetiwa find my device ukikuta nyingine option ondoa tiki...kisha kagua accessibility kama kuna service ambayo ipo stored halafu imepigwa tiki iondoe haraka...ukisha fanya haya ma 2 ie device admn and accsesibilty nenda kwenye option y apps kisha kagua apps ambazo huzielewi nyingi huwa na jina l security make sure una zi unstall...hapo utakuwa umeisafisha simu yako ila kama huyo anaye kufatilia anatumia njia ya telbox app nivigumu kumzuia lbda ubadili number na asiifahamu
 
Back
Top Bottom