Northern Lights
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 412
- 367
Nenda Mlandizi....kuelekea bagamoyo..au nenda chalinze uelekeo SGR ubena hadi ngerengere utapata mashamba bei safii.....Habari JF
Nimeamua kufanya maandalizi ya kustaafu kabla ya muda na kuachana na hizi kazi za ofisini ndani ya miaka 5 ijayo. Hatua ya kwanza nimeona ni kununua shamba walau ekari 10 kwa ajili ya makazi pamoja na ufugaji(70%) na kilimo(30%).
Nitahamia shambani kabisa na kujenga nyumba huko kwa hiyo ardhi inabidi isiwe zaidi ya km 10 kutoka barabarani.
shida inakuja kwenye kupata shamba lisilo na migogoro, au kuuziwa shamba la mtu/serikali, na pia kuepuka madalali wenye njaa kali.
Ni njia zipi naweza kutumia ili kupata shamba zuri na kwa bei nzuri hasa kwenye maeneo ya kibaha, mkuranga, bagamoyo, mikese, dumila, mlandizi, na maeneo ambayo si zaidi ya masaa 5 kuja DSM.
Asanteni kwa ushauri
Asante sana.Fanya utafiti mzuri kwa kutafuta watu wa karibu wa hayo maeneo wakupe infor ya kutosha, mkoa wa pwani utoe kwenye orodha ya kupata shamba, mipango miji inaonesha hayo maeneo ni viwanja vilivyo changamka miaka michache ijayo...hivyo huwenda msamiati wa bei nafuu usifanye kazi sn hapo. Kila la heri mkuu kwa kuwaza juu zaidi juu ya mstakabari wa uzee. Wajuzi watakuja zaidi kukupa muongozo
Asante kwa ushauri, una uenyeji wa maeneo haya na bei zimekaaje kama hutajaliNenda Mlandizi....kuelekea bagamoyo..au nenda chalinze uelekeo SGR ubena hadi ngerengere utapata mashamba bei safii.....
Hapana sina...ila nenda utapata madalalo watakuonyesha kote.....acre from laki 3 kwenda juu....nasikia bagamoyo kumechangamka acre 3mil above....sbb bandariAsante kwa ushauri, una uenyeji wa maeneo haya na bei zimekaaje kama hutajali
Asante mkuu kwa mchango wakoNenda Chalinze. kuna kijiji kinaitwa Tukamisasa.Unaweza pita Ubenazomozi au Lugoba. Ni kama 12km na barabara inapitika mwaka mzima maana iko chini ya TANROADS.Bei ni laki 3 mpaka 5.Niliona kijiji kinaweka tangazo la shamba kuuzwa kwa muda wa kama wiki 3 ili kama kuna utata mtu ajitokeze