2. Don't move too fast/act desperate.
....nk Mpe nafasi ya kukusoma je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.
18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.
Mama Ashrat.
....mnh, huyu kaka BAK wa leo ndiye kweli?
'Hatua za awali+"kila mmoja" karidhika+idara zote= kuambiana ukweli!
.....mjumuisho huo nautazama kwa jicho la kupendana "blindly" and irresponsibly.
Anyway, labda na tahadhari zangu sababu najua athari na faida nilizonipata thru past and present relationship.
Ahsante sana Kaka Mbu,
Hata mie michango yangu umesimama katika hizo nguzo. Labda ni kutojua kujieleza vizuri.
Sijui King'asti, BAK et al wanastumia nguzo zipi?
Mie sifanyi kazi ya kuuza data pasipo sababu ya msingi!!
Babu DC!!
Moskwito, unasahau kwenye uhondo wa ngoma haingii peke yake na wewe unamtangulia. Cha kupatia broken heart? Yaani na mie nimeshakolea ndo nasema ama jamaa anagundua anasepa? Yaani wakati tu marafiki tu mi nakuambia yoote ujue kama utasuka ama kunyoa. Sihitaji kukutega manake ndo utakuja kuninyanyasia penzi likichuja. Dingi anavuta mibhange, so ukija kunisema mi nakucheka ww! Lol
Dark City, kuhusu kijana aliyedhaniwa muarabu, mbona mie mpenzi namchukulia kama rafiki? Mtu mnayeweza kupiga michapo, umbea na udaku na ukakaa mioyoni mwenu! Mi nikitaka kumsengenya hata mama yake mzazi nataka nimsengenye kwake ili yasirudi kwa mama nikasutwa. Kama ni mie ningemsimulia tena nikicheka amuone babangu anavyoweza kuwa katuni. Mwenza atakayenihukumu kwa sababu ya alichofanya babangu ama mamangu kwa kweli hanifai. Nimepitia vitu mbalimbali and I learned from them. Tena ningependa mwenza aniambie 'mupenzi, you are repeating your mom's mistake. Hukupenda alivyofanya a b c d, but haina tofauti na unachofanya sasa'. Mbona atakuwa kanisaidia sana na kunifungua macho? I love open relations kiukweli! Give me all ur dirties!
Kuhusu issue ya uchawi, I guess ningesema tu kiukweli! Ili aelewe kwa nini nakaa mbali na baba yangu. Kuna mtoto wa binamu yangu alikataliwa kumuoa binti fulani kwa sababu ya background ya familia yake. Mdingi akaiongelea siku moja about kuchagua familia bora. Aisee, sikumkopesha! Nilimuambia huku kwetu mbona kuna 1 2 3? Hata sie hatufai basi eeh! Ilibidi awe mpole. Yule mpwa wangu hakumuoa yule binti, na Mungu sio King'asti dada wa watu is happily married. Mpwa kaishia kutundika mimba mwanamke asiempenda, presha ya familia yetu 'takatifu' kaishia kumuoa. Kamtesaaa na sasa kamtelekeza kwa wazazi wake kaenda 'kupumzika' marekani. Na ana visa ya mwaka, sijui kama kuna kurudi tena hapo!
.....kwangu mie, wangu kafaulu yote na sasa yumo katika 'final exam' ya haya mawili....
Labda niongezee neno la akiba.....mara nyingi kwenye hatua hizi za mwisho kuna kina dada/mama ambao huamua "kuubeba" ujauzito kama '-guarantee-' ya kumkamata vizuri (assurance) huyo mwanaume (asijemkimbia) ambayo kwa tafsiri yangu hilo pia linaangukia kwenye category ya kumkamata 'pembe' huyo mwanaume.
Mnalizungumziaje hili? (....Kumradhi wazee wa 'msiikurubie zinaa,' na wahamasishaji wa nyota ya kijani)
........Si lazima ugonjwa Babu, hata kukinga ni sababu ya msingi pia!
Hahhahaahha nimedandia tren kwa mbele hata sijui mwaongeleani hapa...ngoja nisome
Karibu sana dada MwanajamiiOne,
Hii ni sub-item ya mada nzuri sana ya Mama Ashrati (which I have to acknowledge kwamba nimeipenda sana na ina mambo mengi mazuri kwetu sote, men and women). Kwa hapa, tunaongelea kama kuna haja ya ku-filter mambo ya kumwambia mpenzi wako au la (yale yanayohusu familia zenu na hata ukoo mzima).
Kuna wanaosema kuwa ni safe kumueleza kila kitu kuhusu familia yako (mfano, kama baba ni/alikuwa jambazi, shoga etc; au mama alikuwa mchawi, kahaba, mmbeya na mengine mengi). Pia tupo (Mie na Mbu) ambao tunasema kuwa haina haja kuanza kuanika familia yako. Ila tukaweka angalizo kwamba unaweza kusema baadhi ya mambo ambayo unadhani huko mbele yanaweza kuingia kwenye equation ya maisha yenu.
Binafsi naamini kuwa, kuna baadhi ya mambo ambayo hata GF/mchumba akigundua hawezi kuniuliza. I can't imagine my GF aniulize eti nimweleze jinsi mama yangu alivyokuwa kahaba/changudoa....!!! Nadhani nitapoteza appetite naye toka siku hiyo!!
Babu DC!!
I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona sio vibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba Ashrat sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila tumedumu na bado tunaendelea na safari.
Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.
1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k
2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.
3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.
4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.
5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.
6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.
7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.
8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.
9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.
10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe.
11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.
12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi yako.
13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.
14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.
15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.
16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.
17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.
18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.
Mama Ashrat.
Ahsante sana ingawa hilo la mwisho nahisi linafaa kuambatana na kila unachofanya.
Soulmate hili la kina mama 'kuamua' kubeba mimba ndipo hasa wengi wetu tunapokosea. Wanawake wengi huwa tunaitumia hii silaha kama silaha ya kukumaliza kabisa kumbe ndo tunajimaliza. Kubeba mimba si 'uamuzi' wa mmoja, tena mwanamke pekee ni maamuzi ya pamoja na ambayo hujenga zaidi kuliko yakiamuliwa na mmoja. Ingawa pia sometimes kuna kujisahau kati ya wapenzi ambao sasa wameshaanza kujifeel 'confortable' to each other, ambapo utakuta hata kama walikuwa wanatumia kinga basi zinawekwa kando na hakuna wa kumwuliza mwenzie la vipi mbona??
Pili ukimya nao unachangia ni vema kama mnaanza kuwa pamoja na hamtuimii kinga basi kuwekane wazi kuwa hamna mpango wa watoto hivi karibuni kuliko kukaa kimya ukiassume kuwa mwenzangu ana 'ukubwa' wa kutosha kuelewa kuwa hatujaoana so hatutakiwi kuleta viumbe duniani kwanza.
Lakini la tatu na kubwa zaidi ni kuwa WOTE wawili mchukue tahadhari! Mkaka jua mzunguko wa mpenzio, kuwa makini katika utumiaji kinga kila mara, ukimwachia mdada peke yake kama ndo anazo hizo evil minds za kukushika pembe basi utakuwa umempa funguo mwenyewe!
Ehee kumbe. Nadhani msimamo wako wewe na Mbu na wengineo wenye mtazamo huo uko sahihi. Kuna mambo mengine ni bora yaendelee kukaa huko huko kwenye makabati na ikitokea yakaingilia utaratibu wenu wa maisha utayatolea maelezo yafaayo wakati huo,
Kuna tatizo la wivu ambao hata makahaba wanao. Yaani unakuta mwanamke ni mpelelezi kuliko hata polisi
Na wanawake wengi mnadhani kumchimbachimba mwanaume ndo kuhakikisha anakupenda.
Wanasahau Mungu akipewa nafasi na wao kuwa na mienendo mizuri ya uamifu ni kipimo tosha mwanaume mwenyewe kujisema kuhusu anavyokufikiria. NB: Uaminifu sio pamoja nakutoa ngono haraka
...Babu DC mie naomba kuuliza hapo kwenye bold...ni wakati gani muafaka wa kuongea mambo yanayohusu familia zenu? hasa kama kuna dosari/tuhuma dhidi ya wale waliomo ndani ya familia?
Hata mie sielewi mkuu,
Uanze kusema kuwa, unajua sweetie, baba yangu ni mchawi, kaurithi uchawi kwa bibi yake mzaa mama. Na mama yangu ni mwizi namba moja pale mtaani....Halafu, dada yetu mkubwa ni changudoa.....
Huyo GF/BF naamini atakuona kama nati fulani za kichwa zimelegea!!
BAK,
Haina tija kueleza negatives za familia yako, labda kama kuna sababu ya msingi au zitaingia katika equation ya maisha yenu huko mbele ya safari.
Na umri wangu huu, kuna mambo kibao ya familia yetu ambayo sijawahi kumweleza Bibi DC na wala sitamwambia. Naamini hata yeye akija kuyajua hataniuliza kwa sababu yajaadhiri ndoa yetu kwa namna yoyote ile.
Babu DC!!
Babu DC kuna mambo mengine kwenye familia unaogopa hata kuyaweka hadharani kwa yale hayaathiri mahusiano yenu bora kuwa kimya imenikumbusha story ya dada mmoja alibakwa na baba yake mzazi akiwa mdogo alikuwa na akili za kutambua alichofanyiwa huwa najiuliza ataeleza hiyo story chungu kwa BF wangapi mpaka kujaolewa? nafikiri mengine yatajulikana safari inavyoondelea utapata maneno ya kueleza pindi muda wake ukifika