Namna ya kumkamata mwanaume!!

Hujakosea jina unaonesha ni Asharat wa ukweli.
 
Nimekukubali. Problem yetu ni desperado! Nna dadangu akiambiwa na mkaka ntakutoa jioni, anaulizia pa kupata gauni la harusi!
Kila la kheri mama

aah hiyo kali halafu hapo aliposema mwingine anapigiwa tu simu na wanaume hata wasiojulikana ndo nimekubali
 



on point mama ashrat..hasa iyo ya 14,kina nakusalimia,waharibif sana..
 

fazaa

Kuna mengi dini isiyoruhusu ila at some point tunajikuta tunafanya kwasababu tunaona tunatakiwa/hitaji kufanya hivyo. Ndio maana kukawa na kutubu, tunakosa kila siku na tunatubu na kuachana na hayo makosa. Hata wewe inawezekana hukushiriki/bado hujashiriki nje ya ndoa ila haina maana huna makosa mengine, pia usisahau kuwa kwa Mungu hamna mizani.

Tukirudi kwenye kuheshimu na kuogopa.
Kwanza kumuogopa mtu sio kumheshimu. Naweza nikakuogopa wewe kwasababu hii au ile ila nisikuheshimu, hiyo inaiywa nidhamu ya woga maana hutoona kwamba sikuheshimu. Pili, kumwogopa mwanaume/mwanamke wako kutakunyima uhuru/wepesi wa kuwa karibu nae kimawasiliano na hata kihisia kwasababu unamwogopa.Ndio maana wapo watu wapo kwenye ndoa miaka na miaka ila hata siku moja hamna anaeweza mkalisha mwenzie chini akamweleza hisia zake au akamkosoa kiutu uzima. Matokeo yake ndo hao wahusika kwenda kutafuta unafuu sehemu nyingine.
 
Last edited by a moderator:

Heshima ndio itakayozuia hayo yasitokee.
Ukishamheshimu mtu (heshima ya kweli na sio ya kushinikizwa) utamtii automatically. Kila kitu kitaenda kwa maelewano.

charmingirl, nafurahi kusikia hivyo mwaya.

BAK na UmkhontoweSizwe
Asanteni sana kwa nyongeza zenu, kila mlilosema linaongeza mambo muhimu sana.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
BAK umeongea kitu muhimu sana. Sio ex tu ama watoto, kuna issue ya wanafamilia wakorofi pia. Hii tabia (hasa ya wadada) ya kujifanya unatokea familia takatifu is really disgusting. Hata kama babako mchawi muambie mwenzio, ajue u don't side with mambo yake. Ili hata huko mbele ya safari akikusakama nao umuambie the loss is his asiwacheke ndugu zako manake nao ni sehemu yenu.
Asante rafiki.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK


...Nilishawahi kuweka mfano hai hapa wa rafiki yangu mpenzi ambaye baada ya kumpata kimwana na kutoamini bahati yake kwamba kimwana yule alikuwa hana mtu ikabidi amuweke kiti moto kuulizia mahusiano yake ya nyuma na kwanini mahusiano yake ya mwisho yalivunjika. Kimwana akawa muwazi kuelezea kila kitu bila kuficha chochote, na jamaa akafuatilia ili kuhakikisha aliyoambiwa yalikuwa kweli na akathibitisha kwamba ni ukweli mtupu. Binti naye akataka kujua mahusiano ya nyuma ya mwenzie basi njemba haikuwa na hiana ikaelezea kila kitu. Mapenzi yakapamba moto sasa ni mume na mke.

Vaislay
 
Last edited by a moderator:

Ahsante sana King'asti kwa mchango wako muhimu.
 
Last edited by a moderator:
point,,,,hakika na kweli
 
dah, shule mwanana sana hii... si mbaya siku nyingine ukishuka kwenye jukwaa la kule chini kabisa kutugawia dondoo zinazohusiana na department ile pia...
 
Mke mwema hutoka kwa Bwana; kwa akili zetu si rahisi kumtambua mke mwema

unamtaka mke mwema atokaye kwa mungu,sawa,wewe ni mwema,,,,,,,,,yaan mungu amtoe mtu wake mwema ampe haramia,,,,,,,,jaman,jamii imeharibika na wanawake hao gibiligibili ni zao lake,,,,,zaa kusanya watoto lea somesha,,,kuoa tunaolea mazoea tu,,,ila moto,,tunakufa kwa presha tunawaacha wanadunda,,,wanafurahi hao hasa umeacha vimali,,kaburi lako atajengea hata kwa marumaru na kuwasha mishumaa kumbe ukiwa hai alikuuuumiza,,,,achana nao:yo:
 
Hii sredi imetulia sana kwa wadada, ubarikiwe mama.
Ufafanuzi : Lawyer nikisema sredi imetulia basi ujue ina hazi ya kimataifa
 
Aisay mimi na wewe tuko tofoutii sana wewe unadhani mke kumuogopa mme ni sababu ya vipigo anavyo pewa.

Mwanaume anaye piga mwanamke naye ni mwanaume...hao sio wanaume, hao ni walevi, vichaa, yani sijui niseme nini...Yani wewe unadhani wanaume wote ni walevi au vichaa au hawajui mwanamke katokea wapi?

Ndo naona mawazo yako na mimi yako tofouti sana, wewe unaona wanao piga wake zao ni wanaume :A S shade:
 
mama asharat ni noumeeer...umegusa 95% ya mambo aliyokua ananifanyia wife wakati tukiwa wachumba,tena umesahau.....hard working pia ni mpango mzima,leo hii ni mme na mke na mtoto mmoja....
 
Yeap kuna kutubu mengi tu lakini sio ya kuoa mwanamke umeisha sex naye, afu unaendelea naye eti ni wife wako...wakati kwa mungu wewe kila ukisex na huyo mme wako/mke wako ambaye mliona bada ya sex ni dhambi tu, sababu mungu hatambui ndoa yenu.

Mtu ana tubu harudii makosa yake tena...sa we unategemea kutubu lini? ikiwa mme uliye naye umefanya naye sex kabla ya ndoa...sijui niseme nini hapo...Hivi kuna toba hapo.

Mtu anatubu kama vile ka sex nje ya ndo afu haendelee na makosa tena ukiolewa na mtu ume sex naye ina mana hujatubu bado , sasa wewe sijui niseme nini sijui lini unategemea kutubu afu hapo hapo unashangilia wengine watoe matunda ili waolewe hahaha...kweli kuna vichekesho duniani...najua wengi mtanichukia sababu mmo katika huo mfumo...lakini huo ni ukweli, mtake msitake ndoa zenu hazikubaliwi na mungu :A S shade:
 
dah, shule mwanana sana hii... si mbaya siku nyingine ukishuka kwenye jukwaa la kule chini kabisa kutugawia dondoo zinazohusiana na department ile pia...

Hahaha, hiyo mpaka niombe ruhusa kwa baba mwenye nyumba.
 

...Niliyoyaandika hapa ni maneno ambayo nimeyasikia kwa akina mama ambao wanapata vipigo ndani ya ndoa zao wengine ni ndugu wa karibu kabisa kwamba wanawaogopa waume zao kutokana na vipigo na wanapokuwa hawapo nyumbani wanajiona wako huru zaidi lakini waume wakirudi tu basi uoga huwajaa kwa kujua kosa dogo linaweza kusababisha kipigo.

Kutofautiana hakuna tatizo lolote au vinginevyo tungekuwa tunakubaliana kila kitu basi hili jamvi lingekuwa halina mvuto kabisa. Bado msimamo wangu ni ule ule kwamba hakuna sababu yoyote ya mke kumuogopa mumewe bali anatakiwa kumuheshimu. Ukiona mke anamuogopa mumewe basi ujue kuna walakini wa namna moja au nyingine.
 
Hii sredi imetulia sana kwa wadada, ubarikiwe mama.
Ufafanuzi : Lawyer nikisema sredi imetulia basi ujue ina hazi ya kimataifa

Hahaha asante klorokwini au lawyer kama unavyoitwa/jiita.

fazaa
Wewe ndio msemaji wa Mungu? Hayo unayoongea umeyapata wapi? Kama ni maoni yako tu basi yabaki kama yalivyo, ila kama una uhakika kwamba Mungu ndivyo anavyofanya kazi naomba vilelezo vya uhakika.

majany
Hilo nalo linahusika kwakweli.Mwanamke kujituma na sio kubweteka.
 
Last edited by a moderator:
Nimekubali point nyingi hasa za wale wanaotaka kuolewa; ila kwa wenye ndoa maisha ni more complicated na wengi tu wenye heshima kwa waume zao ndoa zao ziko ndivyo sivyo. Na huwezi sema kuwa mumeo achiti ni siri ya moyo wake; ila ni vizuri ku think positive na kujipa moyo.

Inategemea na mume ulo nae; wengine hata walambwe hawakamatiki. Hence it takes two.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…