Namna ya kujua Supplier fake ununuapo Online kama Alibaba

Wakuu mimi ni miongoni mwa watu wanaonunua vitu online hasa Alibaba kwa bahati nzuri hadi leo hii sijawahi kukutana na kuibiwa.

Hili nalileta kwenu kwa muda huu nimeona kwenye magroup ya Whatsapp zikipita jumbe nyingi zikitahadharisha wizi uliopo huko China kwa manunuzi ya online.

Sasa kabla sijaibiwa naomba kujua mabombo muhimu ya kuzingatia ili kujua kuwa supplier ni Genuine au fake.

Karibuni wakuu.
Iwapo Kampuni ya China wanakupa akaunti ya kulipia mzigo ipo nje ya china Stuka achana nao mara moja.
 
Vp chief, amazon wao hawana shida? Maana ndio nimejisajili ila bado sijaanza kununua vitu, wako vyema na wao?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Unapofanya manunuzi kwenye mtandao siku zote unatakiwa uwe makini. Hakuna sehemu ambayo matapeli hawajaribu kulaghai watu. Cha maana ni kuhakikisha unafuta misingi na kanuni za usalama. Mara nyingi uzoefu ni silaha nzuri na vigumu mtu kukuambia moja kwa moja ukitakata kuepuka matapeli tumia kanuni A,B,C. Hii ni kwa sababu matapeli hujaribu kubadilisha njia za upigaji. Ni kama tunavyoishi tu huku mitaani na matapeli. Kama huna uzoefu na ndiyo unaanza tafuta mtu unayemuamini akuelekeze (bila kumpa detail zako za credit card etc).
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom