Kiukweli Botswana ni nchi nzuri sana,nakumbuka kuna bro mmoja alikuwa anasomaga chuo cha ushirika moshi,wakati anasoma akabahatika kumpata na kumtia mimba bint wa kibotswana,baada ya kumaliza bint akarudi kwao mchizi akawa anasota kitaa,basi baada ya mda bint akamfuata jamaa na kwenda nae botswana,jamaa kufika akapata kazi fasta baada ya kama miaka miwili akarudi kutembea bongo akiwa na gari yake mwenyewe,kuna story alinipa ya kuwa botswana ni nchi nzuri sana kwani inamaendeleo ukizingatia bado wazungu wapo nchini botswana mpaka leo,mi nakushauri nenda mambo ya kupata kazi utajua huko huko ila kazi zipoHabari za mwisho wa wiki waungwana?
Naomba anayejua namna ninavyoweza kufika Botswana kutokea Dar anisaidie maelekezo ila isiwe kwa ndege.
Nahitaji kwenda Botswana kujaribu nafasi nyingine ya maisha.
Pia naomba kujua inabidi niwe na documents gani ili niingie kwa njia halali.
Nimeamua hivi kwa sababu Botswana ni nchi ya ndoto yangu tangu nikiwa mdogo. Hivyo nimeona nikajaribu bahati yangu huko.
Nawasilisha