Namna ya kufanya maamuzi magumu

Namna ya kufanya maamuzi magumu

Dinero

Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
39
Reaction score
52
Watu wengi tumekuwa wagumu sana kufanya maamuzi magumu.Hii inatokana labda na uwoga kwamba nikifanya hili jambo baadaye litaniletea matatiazo au madhara ambayo hayafai kurekebika tena.

Lakini si kweli kwamba ukifanya maamuzi ya jambo fulani lazima yatokee matokeo mabaya.Kwa kuona watu wanapata shida sana kufanya maamuzi leo hii nimekushirikisha njia saba ambazo zitakusaidia kufanya maamuzi yoyote yale.

1.Kuwa na dira ya maisha

Dira ya maisha ni msingi na nukuu nzuri kwa kila maamuzi unayofanya.Kwenye ndoto zako unayaonaje maisha kuhusu kazi,mahusiano,mambo ya kifedha,maisha ya kila siku(namna ya kuishi)n.k.Kitu gani hasa kinaonyesha dira yako.Andika/Orodhesha vitu vyote vinavyoonyesha dira yako.Pitia tena dira yako mara mbili,uamuzi ukikujia unaweza kutumia dira hii kama silaha yako.Ukitoka nje sana ya dira utaumia na utajuta. Fanya tathmini kwenye chaguo lako ukiongozwa na dira iliyopo.

2.Tathmini faida na hasara

Wakati unafanya maamuzi zingatia matokeo chanya au hasi yanaweza kutokea.Orodhesha faida na hasara kwenye kila mbadala halafu linganisha na pointi zako ulizoorodhesha awali.Je madhara ni mengi kuliko faida?unaweza kuishi na hayo matokeo hasi?utafanya nini kurekebisha hiyo hali?

3.Washirikishe rafiki zako

Kabla hujafanya maamuzi yoyote yale kwenye maisha yako ebu tafuta marafiki wawili au watatu unaowaamini sana na uwashirikishe.Waeleze dira ya maisha yako,waoneshe orodha ya faida na hasara alafu waulize kuhusu mtazamo wao.Kama kuna mmojawapo amepitia hali kama ya kwako basi atakuwa mwalimu mzuri sana na utapata ushauri mbalimbali kutoka kwao.

4. Tafuta nguvu kubwa zaidi

Nenda sehemu iliyotulia, pumua kwa nguvu, fumba macho yako,sali au fanya MEDITATION ni uamuzi wako utakachotaka wewe na omba mwongozo.Huwezi amini lakini baada ya muda mfupi utajiwa na busara na akili yako itafunguka mpaka utashangaa.Tumia muda huo kutafakari kuhusu uamuzi unaotaka kufanya.Wazo likija chukua kalamu na karatasi andika haraka hisia zako baada ya tafakari.Subiri siku kadhaa utapata jibu bila kutarajia.

5.Tumia njia ya kurusha shilingi

Njia hii kwa namna fulani naipenda pindi nikiwa na mambo mengi kichwani na sijui cha kufanya.Chukua shilingi upande wa kichwa nuia maamuzi fulani unayotaka kuyachukua na upande mwingine wa shilingi yani mkia nuia maamuzi mengine.Rusha shilingi hewani kabla haijatua kuwa makini na upande gani utakuwa juu.Kama una maamuzi zaidi tumia njia hii itakusaidia sana.Hii ndio njia rahisi ambayo hata moyo wako unakusukuma kufanya.

6.Fanya utafiti wa kutosha

Kabla hujafanya maamuzi yoyote yale fanya kwanza utafiti wa kina ili usije ukajutia baadaye.Ongea na watu ambao wana uzoefu na jambo ambalo unataka kufanyia maamuzi.Kama haitoshi angalia njia mbadala zake zitakuwaje.Kama unataka kazi fulani basi tafuta mtu kwenye ile ofisi kuhusu hiyo kazi mpya unayotaka kuifanya.Kama unataka kuvunja mahusiano na mpenzi wako basi fanya utafiti madhara yake.

7.Usiangalie nyuma

Kama umemaliza kazi, umeheshimu maono yako,umepitia faida na hasara,umepata ushauri na nafsi yako imeridhika basi huna budi kufanya maamuzi sasa na usiangalie nyuma.Kwenye maisha yetu ya kila siku tunapitia misukosuko mingi sana ambayo mtu inabidi utulize akili kufanyia maamuzi kwani maamuzi mabaya yanaweza kuharibu hata vizazi vijavyo.

Ukitumia njia hizi na kuweza kufanya maamuzi kwenye maisha basi itaonyesha namna gani umekua kiakili kwani kufanya maamuzi si jambo rahisi kama linavyotamkika vinywani mwetu.
 
Hii makala ina uhusiiano wowote na mheshimiwa mzee wa mamuzi magumu aliyerudisha fomu ya kugombea kuingia Big Brother White House pale Magogoni?
 
Back
Top Bottom