Namna ya kuchapisha kitabu bila gharama na kuongeza mauzo.

ngosh

Member
Dec 18, 2014
48
40
Jee wewe ni mtunzi wa hadithi, vitabu vya riwaya, tamthiliya au vitabu vya taaluma, na umekuwa hufadiki na kipaji chako cha uandishi? Jee umeandaa kitabu chako lakini umeshindwa kukichapisha kwa kuwa huna pesa? Sasa shusha pumzi ufumbuzi wa tatizo lako umepatikana, unaweza kuchapisha kitabu chako bila gharama yoyote na kuuza kitabu chako kwa wingi kwa muda mfupi. Kama unataka kufaidi matunda yako ya uandishi endelea kusoma makala hii.
Kwa wale wasio ni fahamu ngoja nijitambulishe mimi ni Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri, Ni Mshauri wa biashara na Mkurugenzi wa kampuni ya CPM Business Consultants. Nimefanikiwa kuuza nakala 5,000 za kitabu changu mwenyewe bila msaada wa mchapishaji au msambazaji yeyote wa vitabu. Kazi hii haikuwa rahisi nimeifanya kwa miaka 9 tangu mwaka 2008 hadi sasa ninavyoandika makala hii. Tatizo letu hapa Tanzania, waandishi wa vitabu wanakwama kwa sababu ya mfumo mbovu wa uuzaji vitabu na kukosekana uaminifu kwa wachapishaji na wasambazaji (Publishers) ambapo mwandishi akimkabidhi mswada Publisher kuna uwezekano mkubwa wa kudhulumiwa kazi yake. Hivyo mwandishi au mtunzi anaamua kuuza mwenyewe kitabu kimoja kimoja au kwa jumla kwenye maduka ya vitabu.Tatizo la mfumo huu unamfanya mtunzi ashindwe kufaidi matunda ya utunzi wake kwa sababu mapato ya vitabu yanaingia kidogo kidogo. Suala lingine linalokwamisha waandishi ni gharama za uchapishaji ambapo watunzi wengi hasa vijana wanashindwa kuchapisha vitabu kwa sababu wanashindwa kumudu gharama za uchapishaji.
Napenda kuwapa habari njema waandishi wa vitabu, sasa hivi hali imebadilika kutokana na mabadiliko ya teknolojia baada ya ujio wa mtandao wa internet ambapo unaweza kuandaa kitabu chako na kukiuza kwa mfumo wa soft copy ambapo kinajulikana kama (e book) hivyo huna haja ya kutafuta mchapishaji na kumlipa kwa hiyo hakuna gharama yoyote ya uchapaji. Faida nyingine ni kwamba internet inatumiwa na watu wengi, mfano sasa hivi nusu ya watu wote duniani wanatumia mtandao wa internet tena kwenye simu zao za mkononi, na watu bilioni 1.5 wanatumia mtandao wa facebook. Hivyo ukitumia mtandao wa internet kufanya biashara ya kuuza vitabu unaweza kuuza vitabu vingi sana kwa muda mfupi. Mfano nimeshuhudia mtu mmoja ninayemfahamu hapa Tanzania ambaye ametumia mfumo huu akiuza vitabu 3,500 kwa muda wa wiki 3. Hata hivyo usifikiri ni kazi rashisi kufanya hivyo kama huna mfumo (Platform) ya kufanyia kazi hiyo ambapo unatakiwa ku upload kitabu chako na uwe na mfumo wa kupokea malipo ambapo mtu akinunua kitabu anadownload mara moja.
Kama wewe ni mtunzi wa vitabu naomba tuwasilianekwa simu namba 0755394701 ili nikusaidie kutatua tatizo la kuuza vitabu vyako. hata kama una kipaji cha uandishi lakini huna pesa ninazo mbinu za kutunga na kuuza kitabu ambapo nitakupa mafunzo na ushauri bila gharama yoyote au kwa gharama kidogo tu.
Mwandishi wa makala hii Bwana Charles Nazi ni Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kupata ushauri na mafunzo ya kutunga kitabu na kuuza bila gharama au kwa gharama ndogo piga simu namba 0755394701
 
Back
Top Bottom