SoC03 Namna utawala bora na uwajibikaji vilivyo muhimu katika maendeleo

Stories of Change - 2023 Competition

Ms chua

New Member
Jun 1, 2023
1
1
Ni matamanio ya kila nchi kuwa na maendeleo ya kiasi cha juu sana hata kufikia hatua ya kujitegemea. Hivyobasi,ili nchi iweze kupata maendeleo hayo inapaswa kuwa na viongozi wazuri wanaowajibika.Uongozi na uwajibikaji ni maswala mawili tofauti yanayotegemeana kwani kiongozi mzuri ni yule anaewajibika.

Utawala bora na uwajibikaji ni nguzo muhimu ya maendeleo katika nchi yo yote.Uongozi bora unahusisha uwezo wa viongozi kuongoza watu kwa busara na kuwa na hekima na uthubutu wa kufanya maamuzi kwa manufaa ya wananchi wote.Kwa upande mwingine uwajibikaji huhusisha viongozi kuwa tayari kubeba majukumu na kuyatekeleza kwa ufanisi na kwa wakati.

Kutokana na utawala bora na uwajibikaji nchi huathirika vyema na matunda yake huonekana kwa wananchi wote na kuwanufaisha wote.Zifuatazo ni athari chanya za utawala bora na uwajibikaji;

Ukuaji wa kiuchumi;kutokana na utawala bora nchi inaweza kunufaika kiuchumi kwani viongozi wana madaraka na ufikivu wa rasilimali za taifa.Hivyo,wamepewa nafasi katika ngazi ya utawala ili kuweza kutumia rasilimali hizo na madaraka yao kunufaisha nchi nzima.Viongozi wana mamlaka ya kuunda sera rafiki zinazochochea maendeleo ya kiuchumi. Nchi ya Singapore kama mfano mzuri,imenufaika kiuchumi kutokana na namna serikali yao inashirikiana na wananchi katika swala zima la ukuaji wa kiuchumi ikiwawezesha wajasiriamali na wabunifu mbalimbali na pia serikali huwataarifu wananchi mipango yao na sera zao pamoja na hatua wanazotaka kufanya katika kukuza uchumi wa nchi.Vilevile,wananchi hupewa fursa kutoa maoni yao na kuuliza maswali na mwishowe kupewa ufafanuzi na serikali ili kuelewa na kushiriki katika zoezi zima la ukuaji wa kiuchumi. Mfano huu ni mzuri na wa kuigwa nchini kwetu ili tuweze kupata maendeleo.

Maendeleo ya kijamii; nchi kadhaa zimefanikiwa kupunguza umaskini kwa kuboresha sekta mbalimbali kama vile elimu na huduma za kiafya.Maendeleo ya kijamii pia yanaweza kupatikana kiurahisi chini ya utawala bora kwani viongozi watawajibika ili kuhakikisha wananchi wanafurahia matunda kutokana na rasiliamali za taifa. Rwanda kama mfano mzuri, wameweza kukuza uchumi na kupunguza umaskini tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994. Serikali ya Rwanda imefanya uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu kama barabara,shule,vituo vya afya,umeme na maji. Rais Kagame ameonesha mfano mzuri katika swala la utawala bora na uwajibikaji kwani ameinua uchumi wa Rwanda kwenye sekta mbalimbali na amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kama nchi ya karibu.

Amani na utulivu; kutokana na utawala bora nchi huweza kuondokana na migogoro kwenye sekta mbalimbali kama vile siasa,kiuchumi na kijamii. Kiongozi mzuri ataepusha nchi yake dhidi ya migogoro na kudumisha amani kwani migogoro huathiri wananchi zaidi.Mfano mzuri ni nchi ya Liberia ambapo Ellen Johnson Sirleaf ambae ni raisi mwanamke wa kwanza nchini humo alipigania amani na demokrasia ambapo kulikiwa na vita nchini humo.Hivyo,raisi huyu kutokana na uwajibikaji wake kama kiongozi mzuri alipigania amani na kuleta amani nchini humo na mwishowe aliishia kuimarisha uchumi,kudumisha amani na demokrasia nchini mwao.Hivyo,serikali yetu inaweza ikafata mfano wa kiongozi huyu katika maswala ya kidiplomasia.

Hivyo kutokana na faida za kuwa na utawala bora na uwajibikaji pamoja na mifano ya viongozi chini ya utawala bora nchi ya Tanzania inaweza ikachukua hatua zifuatazo ili kupelekea maendeleo nchini kwetu;

Kuwekeza katika elimu;ili serikali iweze kudumisha utawala bora na uwajibikaji inapaswa iwekeze katika elimu kwani elimu ndio msingi wa kujenga utawala bora.Serikali inapaswa kuongeza bajeti katika sekta ya elimu na kuongeza rasilimali ambazo zitasaidia kukarabati miundombinu ya shule na upatikanaji wa vifaa vya elimu.Sio hivyo tuu,bali serikali itabidi iimarishe mafunzo ya walimu kwani hao ndio wanaotegemewa kuwajenga viongozi wetu wajao.Walimu wanapaswa kujengewa ujuzi na maarifa yanayohitajika katika kufundisha wanafunzi kuhusu maadili na uwajibikaji.Ni kutokana na ujuzi wataopata kutoka kwa walimu ndio utakaowaongoza katika utawala wao.

Kuimarisha mfumo wa utawala bora;nchi yet inaweza kuimarisha mfumo wa utawala bora kwa kuimarisha taasisi za kidemokrasia kama mahakama huru,bunge lenye haki na usawa,uchaguzi huru na uhuru wa vyombo vya habari na kuimarisha katiba na sheria rafiki kwa wananchi wote.Vilevile serikali inapaswa kuipa vipaumbele taasisi huru zinazopambana dhidi ya vikwazo mbalimbali dhidi ya maendeleo kama vile rushwa,umaskini na ukiukaji wa haki za binadamu.Kwani,taasisi hizi zinacheza nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya taifa na mwishowe kudumisha utawala bora.

Kukuza ushirikiano kati ya serikali na wananchi; hii ni kati ya hatua nzuri sana katika kupata maendeleo na kudumisha utawala bora nchini. Serikali inapaswa kufanya kazi Bega kwa Bega na wananchi kwani viongozi wamechaguliwa na wananchi kwa ajili ya maslahi ya wananchi.Hivyo,viongozi wanapaswa kufanyika sauti ya wananchi wanyamavu ama daraja kati ya wananchi na Rais.Ushirikiano huo unaweza kupatikana kwa kuwashirikisha wananchi katika mifumo ya maamuzi ya umma kama vile mikutano,hadhara mbalimbali na mijadala.Pia,serikali inaweza kutumia vyema muundo wa serikali za mitaa. Muundo wa serikali za mtaa imeundwa ili kuweka wananchi na serikali ya juu karibu. Imeundwa na wananchi katika ngazi ya chini,mwenyekiti wa kijiji/mtaa,diwani wa kata,meya na diwani wa halmashauri ya mkoa.Muundo huu ukitumika vyema unaweza kupelekea maendeleo mazuri nchini kwani inagusa watu wote kuanzia ngazi ya chini.Hivyobasi,malalamiko/kero na mawazo mbalimbali yanakusanywa kiurahisi na viongozi kuwajibika katika kutatua changamoto chini ya uwezo wao na zile ngumu kuziwasilisha kwa mheshimiwa rais.Kwa namna hiyo,matakwa ya wananchi yanakuwa yanatatuliwa walau kila mwezi au mwaka.

Kwa kuhitimisha,nchi yetu kama nchi ya kidemokrasia yenye sifa ya amani inaweza ikafikia matamanio yake katika maendeleo.Kwani,kama ilivyo kwetu tumepewa nafasi kutoa maoni yetu na ushauri wetu kwa serikali kwa namna inaweza ikapata maendeleo kutokana na utawala bora na uwajibikaji.Hatua hii imeonesha uhuru wa kujieleza na imeonesha utayari kusikiliza maoni mbalimbali kutoka wananchi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom