Namna nzuri ya kuwa mgeni!

Radium

JF-Expert Member
Aug 5, 2022
479
849
Ni jambo la kawaida kutaka kuwa mgeni mzuri (yaani mgeni atakaye pendwa na mwenyeji). Takwa la kumfurahisha, kumridhisha au kutomkwaza hutujaa pale tunapokubali mualiko wa mlo wa usiku au kwenda weekend kwa rafiki alieko tabata au kwenda likizo kwa bibi alieko Mwanga, Kilimanjaro au hata tukihamia kwa roommate mpya baada ya kuona itapunguza gharama za maisha.

Na huwa tunajilisha msumari kwa kutaka kuziba hitajio hili kwa kufuata mfumo au utaratibu tuliojifunza tangu tumezaliwa ambao tunaamini utamridhisha mwanadamu mwingine ambaye kwa wakati huu anaitwa mwenyeji.

Nayo ni kumuiga mtu huyu, tunafuata muongozo wao, kwenye maongezi tunajadili wanachotaka kujadili, tunakula wanapotaka kula achia mbali kwamba tunakula wanachokula, tunahama mada wanapohama, tunacheka kwenye karibu kila kitu wanachoona ni chakuchekesha au wanachosema kwa lengo hilo la kuchekesha.

Inaonekana huu ndio uungwana na nia safi kimtazamo lakini kuna jambo la ajabu katika nadharia(theory) hii, mtu anayeiga (mimetic person) sio muungwana na huwa hafurahishi kiutendaji (in practice). Anaweza kuwa mwema mwenye nia nzuri na sio mkali au wakutisha lakini pia sio wa kukumbukwa, anayefurahisha au hata wakupendeka.

Katika upande mwingine kuna mgeni sasa ambaye yeye anajua jamii na kujamiiana(socialize), anaeleza mahitaji yake ya tofauti waziwazi na huku akibaki kuwa wa thamani na anaye endeka.


Imagine umeenda kumtembelea bibi yako mzaa mama aliyeko Iringa *** kisha akaambiwa kama ilivyo ada kwa mwenyeji kusema "jisikie uko nyumbani". Mgeni mzuri angeweka wazi kwamba anapendelea mboga juu ya wali kuliko kwenye bakuli ya pembeni au angetafuna mfupa wa kuku kwa sababu ni kawaida yake au kwenye meza ya chakula stori zikiendelea angeweka wazi kuwa anamuunga mkono mwanasiasa fulani ambaye kila mtu anampinga walau kwa mawazo machache.

Ninachojaribu kusema ni kwamba mgeni huyu angeishi kama nyumbani bila kujaribu kufanya vitu ambavyo ni general na invulnerable.

Wageni wazuri wanatuambia kuhusu jambo la kuaibisha lililowatokea kazini kwao mfano kutoa idea ambayo kila mmoja hakukubaliana nayo na mwisho yeye mwenyewe akajua alipokosea. Au kuhusu majuto yanayowawinda katika maisha yao ya kihisia.

Kisha wanakuja kutuambia huwa ni muda gani wanaendaga kulala, ni muda kiasi gani wanahitaji kuwa peke yao ni chaneli gani wanaipenda, kwao wana king'amuzi ambacho hawaoni haja kukilipia, inawauma jinsi tulivyo nyuma kiteknolojia na hata ni viungo gani wanapenda au hawapendi vikiekwa kwenye chai.

Halafu "wanasema samahani kwa kuwa mbinafsi na kwa kiasi fulani mabwanyenye" na kisha wanaongezea kuwa wangependela ugali wa muhogo na kisamvu kama chakula cha mchana. Watu hawa wanapoondoka huwa wanakumbukwa.

Si kama mtu anayeiga anatudhuru au kutunyima uhuru japo hili linawezekana kwani hatujui wakitakacho, ni kwamba hawatupi utulivu wa roho na uhalisia.

Lengo la kila mwanadamu (kwa kujua au kutojua) katika kila muingiliano kijamii(maongezi) ni kuona zile aibu zetu, majuto,majanga,makosa, kumbukumbu na furaha na yote ambayo tunashindwa hata kuyasema zikiakisiwa kutoka kwa mtu mwingine.

Na kile tunachokiona kila tunapokuja karibu na mgeni asiyejibana au asiyeogopa kuaibika ni sisi wenyewe.

Mtu anayefurahisha kabisa ni yule muwazi na mkarimu. Mfano hai (archetype) wa mtu huyu ni mtoto ma miaka minne na nusu.

Hiki kiumbe kitamuambia mtu ambaye bado hawahazoeana kinapodhani kuwa nzi huenda usiku, kuwa kinapenda pipi yenye ladha ipi, kuwa kinapenda ubuyu wa rangi gani, na jina la utani la babu yake mzee. Hili tunaliita la kupendeza lakini kuna jambo kubwa zaidi ndani ya hili na moja kwa moja ni kututua mzigo wa kwamba eti kila mwanadamu anatakiwa aseme yale tu yanayoonekana kuwa yatamfurahisha mtu mwingine kama kuisifia nyumba yake, makochi yake au mapishi yake.

Mtoto mdogo anatukumbusha kwamba utu wa binadamu, kwa maana kwamba wao na wetu unaweza kuonyeshwa wazi na badala ya kukera na kuboa na kutusi na kuumiza, uka ponya na kufurahisha.

Au kujaribu kuonyesha utu kwa kuiga na kuficha matakwa yetu ambao ni wa ideally guest tukaishia kuonekana wanafiki na mwenyeji kuanza kujiuliza ima nilini tutaondoka.

Mgeni mzuri anachanganya uwazi na utu wa mtoto mdogo na utu wa mtu anayejitambua kijamii. Anajua kutengeza hisia nzuri na adimu na cha thamani katika maisha ya jamii ya sasa.

Nyuma ya pazia la nyuso za watu wanaojaribu kuvutia wengine (ambao sasa wanaogopa kuwa wawazi(vulnerable)kwa kuficha aibu zao na kujaribu sana kuwasifia wakiamini ndio kuwavutia) kuna jambo la kuhuzunisha, mwisho wa siku wala hawavutii.

Wao ni zao la style ya malezi ya wazazi/walezi ambayo yaliwalazimisha kuficha uhalisia wao na kuepuka kuwa 'original'. Walitakiwa kuficha wao ni nani/ wanafanya nini kwa kuogopa kumkasirisha mama ambaye ana hasira sana hasa anapotoka kazini au akiwa na kazi zake nyumbani/ baba ambaye muda mwingi yuko na simujanja yake au anakuwa amelewa au basi tu ni baba anayeogopwa na wanae.

Hatuwezi kubadilisha yaliyopita, lakini tunaweza kusitisha na kuacha vita tunayopigana dhidi ya character(uhusika halisi) zetu kila linapokuja swala la kuongea na watu wengine katika jamii.

Uhalisia wetu unaweza kuwa kuna wakati hatuutaki kwa kuamini unatuaibisha, lakini ni kwa kupitia kuweza kuuelezea na kuuonyesha ambapo urafiki wa kweli kati ya wanadamu unaweza kurejea. Rafiki wa kweli ni yule tu anayetujua kiundani.

Kuwa mwema tumekuona kama kunatupa hadhi ya chini.

We have exaggerated how much people like to be imitated and invariably agreed with. Its easy to tolerate such people but very very hard to really like them.

Ila kuwaridhisha na kuwafurahisha tunahitaji kuwa tayari kuonyesha uajabu na walau kiasi kidogo cha aibu na uhovyo ambao sisi sote tunao kama tutajichambua kiundani.
 
Ukienda ugenini, saa ya kuondoka kama kuna watoto wadogo ni vema ukawapa hata 500 au 200 kisha unawaambia hii utanunua pipi kesho shuleni. Sawa mtoto mzuri?
 
Ukiwa mgeni, ikifika muda wa kula wewe kazana sana kuangalia TV. Jifanye kama hujui kinachoendelea
 
Nikiwa ugenini mara zote najitahidi kuendana na 'flow' ya wenyeji lakini kwa mitindo yangu binafsi.

Huwa sihofii kutofautiana nao, na mara nyingi hii huniletea uhuru flani na amani ugenini.

Pia nakuaga mwepesi kuzoeana na watoto wa hapo ugenini,hasa yule mchangamfu ndio anakua mshikaj wangu. Game over, utaskia lini utakuja jamani,flani amekumiss
 
Nikiwa ugenini mara zote najitahidi kuendana na 'flow' ya wenyeji lakini kwa mitindo yangu binafsi.

Huwa sihofii kutofautiana nao, na mara nyingi hii huniletea uhuru flani na amani ugenini.

Pia nakuaga mwepesi kuzoeana na watoto wa hapo ugenini,hasa yule mchangamfu ndio anakua mshikaj wangu. Game over, utaskia lini utakuja jamani,flani amekumiss
Kuwa tu halisi
 
Back
Top Bottom