sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,249
- 4,537
Kwanza naomba mnivumilie wale nitakaowakwaza. Nataka nizungumzie kuhusu elimu yetu ya msingi haswa kwenye hizi English medium schools ambazo tumetokea kuziamini sana.
Hizi shule zinaua elimu ya nchi kwa sababu kubwa zifuatazo.
1. Watoto wanafanyiwa mitihani ya ndani mpaka ya mwisho. Mitihani ya ndani inafanywa na walimu ili kuwaonyesha wazazi kuwa watoto wanafanya vizuri, hii inavutia biashara ya shule. Pia mitihani ya mwisho haswa ya standard 4 na 7 inafanywa chumba cha mtihani yote ni sababu matokeo mazuri yanaitangaza vizuri shule.
2. Walimu wa kigeni haswa Wakenya na Waganda, hawa ni tatizo kubwa sana kwenye elimu yetu, najua hawa watu wa huko ni wazuri sana kwenye lugha ya kingereza hivyo hata wamiliki wa shule na wazazi wanawapenda sana, mwanzoni waliingia kama walimu wa English na science kidogo, ila sasa wanafundisha mpaka somo la kiswahili. Unashangaa mwalimu wa geography kutoka Kenya hajui hata ziwa Manyara lipo wapi, hajui hata kama Tanga ni jiji.
Mwalimu wa civics hajui hata TANU wala ASP, hamjui hata Waziri kawawa. Mwalimu wa history hajui hata Amboni caves ipo wapi. Hapa unategemea nini zaidi ya mtoto asiyejua vitu.
3. Watoto wanakaririshwa kama kasuku.
Matokeo yake ni nini.
Watoto wanamaliza elimu ya msingi wanaongea na kuandika kingereza lakini hawana uelewa kiundani wa mambo mengi. Fanyeni majaribio ya kuwatahini watoto majumbani muone matokeo yake mlinganishe na wanayopata darasani.
Watoto wanapofika secondary schools wanaonekana wameshuka baada ya kuachwa mbali na wanaotoka Kayumba. Kiukweli hawajashuka ila hicho ndio walichovuna huko English medium schools baada ya kulipia mamilion ya pesa.
Mwisho, Naomba Serikali ifanye ukaguzi wa kina kwenye hizi shule japokuwa nyingi ni za wakubwa. Kuna walimu wengi sana sio walimu ila ni waongea kingereza wazuri hawa ndio wanageuka walimu wa kutumainiwa bila kujali content zao.
Hizi ni shule ni bomu ambalo wazazi wengi na Serikali litawalipukia.