Namna CHADEMA inavyokufa

CCM ilishakufa toka 1995 ..Mrema na Maalim Seif walivyowachezesha shikorobo...Mnajivuna kwa kuwa na polisi vilaza wanaofanya kazi zisizowahusu...bila hivyo R.I.P kama KANU

mnajivuna, hapo ushaonyesha ukilza
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali humu. Nimeona mijadala mingi ikiendelea. Kusema kweli mingi inajenga.

Sasa basi kwa leo ninaomba nami niweze kuchangia. Leo ninaomba kuchangia jambo la kuhusu namna ya CHADEMA inavyokufa.

A. KUKOSEKANA KWA SERA
Uhai wa chama ni kuwa na sera. Chama cha siasa kikikosa sera kinakuwa hakijui kinatakiwa kufanya nini. Kwa bahati mbaya kabisa CHADEMA imekuwepo na kuendesha siasa zisizo na sera. Na mwisho wa siku kimekuwa kikijikita kwenye matukio ya muda na yanayopita.

B. KUKOSEKANA KWA ITIKADI
Itikadi ndiyo moyo wa chama. Yaani chama lazima kiwe na itikadi. Hii ndiyo imani ya chama. Bahati mbaya CHADEMA kimekuwa kikiongozwa na misemo tu. Mf: UKAWA, OPERATION SANGARA, UKUTA, KATAFUNUA nk. Hii inafanya chama kionekane cha kihuni. Chama kinakuwa hakina future.

C. KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO YA NDANI.
Chadema kimeshindwa kutatua matatizo yake ya ndani. Kimekuwa kikiongozwa kwa mfumo wa kidikteta. Ni mtu mmoja tu ndiye anakuwa na nguvu. Ukimkosea ubafukuzwa chama. Yeye ndiye A to Z.

D. KUSHINDWA KUBADILIKA KULINGANA NA WAKATI

Hiki chama kimedumaa hakiwezi kwenda na wakati. Kimebaki kwenye siasa za matukio, kejeli na matusi. Hii siyo afya kwa chama. Kinatakiwa kiseme seta zake kuliko kuegemea siasa dhaifu.

Mwisho kabisa kifo cha CHADEMA ni natural death. Kitapotea na hatutakikumbuka tena.
Mkuu utakufa wewe Chadema itakuwepo ni uoga kuwapakazia kesi viongozi wa chadema
 
Back
Top Bottom