Namna CHADEMA inavyokufa

Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali humu. Nimeona mijadala mingi ikiendelea. Kusema kweli mingi inajenga.

Sasa basi kwa leo ninaomba nami niweze kuchangia. Leo ninaomba kuchangia jambo la kuhusu namna ya CHADEMA inavyokufa.

A. KUKOSEKANA KWA SERA
Uhai wa chama ni kuwa na sera. Chama cha siasa kikikosa sera kinakuwa hakijui kinatakiwa kufanya nini. Kwa bahati mbaya kabisa CHADEMA imekuwepo na kuendesha siasa zisizo na sera. Na mwisho wa siku kimekuwa kikijikita kwenye matukio ya muda na yanayopita.

B. KUKOSEKANA KWA ITIKADI
Itikadi ndiyo moyo wa chama. Yaani chama lazima kiwe na itikadi. Hii ndiyo imani ya chama. Bahati mbaya CHADEMA kimekuwa kikiongozwa na misemo tu. Mf: UKAWA, OPERATION SANGARA, UKUTA, KATAFUNUA nk. Hii inafanya chama kionekane cha kihuni. Chama kinakuwa hakina future.

C. KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO YA NDANI.
Chadema kimeshindwa kutatua matatizo yake ya ndani. Kimekuwa kikiongozwa kwa mfumo wa kidikteta. Ni mtu mmoja tu ndiye anakuwa na nguvu. Ukimkosea ubafukuzwa chama. Yeye ndiye A to Z.

D. KUSHINDWA KUBADILIKA KULINGANA NA WAKATI

Hiki chama kimedumaa hakiwezi kwenda na wakati. Kimebaki kwenye siasa za matukio, kejeli na matusi. Hii siyo afya kwa chama. Kinatakiwa kiseme seta zake kuliko kuegemea siasa dhaifu.

Mwisho kabisa kifo cha CHADEMA ni natural death. Kitapotea na hatutakikumbuka tena.
Kama chadema inakufa kwanini wanazuia mikutano ya kisiasa, viongoz wa chadema kubambikiziwa kesi, kamatakamata ya viongozi wa chadema,? Ndugu hii inaonesha dhahiri kuwa chadema ni tishio kwa watawala wa ccm.
 
Asante sana kuwa kwangu Canada hakunifanyi nisiijue nchi yangu. Chadema naijua zaidi uijuavyo.
Mimi sikuwa na wewe Kanada wala sikujua kuwa ulikuwa huko, ila kutokana na kilichofanyika Chadema hivi karibuni nilipata picha kuwa wewe ni mgeni wetu Bongo ndiyo sababu nilikushauri ufike ofisini kwao licha ya kuwa hutaki kwa sababu unaijua Chadema kuliko wenye chama! That's what you learned in Canada! Welcome home, you are great.
 
Kifo huwa kinaanza na dalili. Kwanza kudhoofika, kukosa direction hatimaye kufa.

Mtafanya hujuma sana kwa cdm lakini hamtofanikiwa. Cha muhimu mfahamu watu wakichoka wamechoka. Ccm ni chama kizee hakina mvuto na ndio maana kinatumia mabavu kubaki madarakani, na namna pekee ni kuihujumu cdm kisha kupita majukwaani kufanya propaganda eti cdm inakufa kwa kukosa sera. Heshimuni box la kura kisha msubiri muone kama watu watawachagua kwa hizo sera.
 
Hii nchi inaandaliwa kuingizwa kwenye machafuko ya lazima na CCM kwa kufikiri CHADEMA ikifa ndipo CCM itapendwa.

Kati ya watu wanaostahili kunyongwa hadharani ni wale wanaoshiriki kuua demokrasia na uhuru wa watu kwa tamaa zao za kupora mali za wananchi na kulindana wasiwajibishwe kwa madhambi yao.

Ila ni hakika siku zenu zinahesabika. Hii nchi ni nchi huru na kila raia anapaswa kuwa na haki sawa na uhuru kamili wa kushiriki fursa zote za kijamii na kisiasa zilizopo kwa mujibu wa katiba.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali humu. Nimeona mijadala mingi ikiendelea. Kusema kweli mingi inajenga.

Sasa basi kwa leo ninaomba nami niweze kuchangia. Leo ninaomba kuchangia jambo la kuhusu namna ya CHADEMA inavyokufa.

A. KUKOSEKANA KWA SERA
Uhai wa chama ni kuwa na sera. Chama cha siasa kikikosa sera kinakuwa hakijui kinatakiwa kufanya nini. Kwa bahati mbaya kabisa CHADEMA imekuwepo na kuendesha siasa zisizo na sera. Na mwisho wa siku kimekuwa kikijikita kwenye matukio ya muda na yanayopita.

B. KUKOSEKANA KWA ITIKADI
Itikadi ndiyo moyo wa chama. Yaani chama lazima kiwe na itikadi. Hii ndiyo imani ya chama. Bahati mbaya CHADEMA kimekuwa kikiongozwa na misemo tu. Mf: UKAWA, OPERATION SANGARA, UKUTA, KATAFUNUA nk. Hii inafanya chama kionekane cha kihuni. Chama kinakuwa hakina future.

C. KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO YA NDANI.
Chadema kimeshindwa kutatua matatizo yake ya ndani. Kimekuwa kikiongozwa kwa mfumo wa kidikteta. Ni mtu mmoja tu ndiye anakuwa na nguvu. Ukimkosea ubafukuzwa chama. Yeye ndiye A to Z.

D. KUSHINDWA KUBADILIKA KULINGANA NA WAKATI

Hiki chama kimedumaa hakiwezi kwenda na wakati. Kimebaki kwenye siasa za matukio, kejeli na matusi. Hii siyo afya kwa chama. Kinatakiwa kiseme seta zake kuliko kuegemea siasa dhaifu.

Mwisho kabisa kifo cha CHADEMA ni natural death. Kitapotea na hatutakikumbuka tena.

hivi kitu kikifa, huwa kinakufa tena??
 
na kifo cha CCM umeanza kusikia kuanzia lini??
CCM ilishakufa siku nyingi. Udikteta unaweza kujivika chama chochote. CCM haiongozi nchi bali dikteta John Pombe Magufuli. Kama ilivyo kwa Rwanda na Paul Kagame anavyojificha kwenye chama chake na kuitisha chaguzi feki.

Hata akina Sadam Hussein na Gadafi walikuwa na vyama walivyovitumia kujificha kutawala kidikteta.
 
Halafu kimekosa ujasiri na uthubutu... kila mtu pale ufipa ni mwoga, unakumbuka amsha amsha za dogiTA SilaHA Enzi hizo?
Mna mawazo ya kipuuzi kweli. Hivi kesi ya kina Mbowe, unaifahamu ilitokana na nini?
Yule anayetibiwa Ubelgiji alikosa nini mpaka akusudiwe kuuwawa?
 
CCM ilishakufa siku nyingi. Udikteta unaweza kujivika chama chochote. CCM haiongozi nchi bali dikteta John Pombe Magufuli. Kama ilivyo kwa Rwanda na Paul Kagame anavyojificha kwenye chama chake na kuitisha chaguzi feki.

Hata akina Sadam Hussein na Gadafi walikuwa na vyama walivyovitumia kujificha kutawala kidikteta.

Hahahaha
Jisumbue roho mbaya na umaskini utakuuwa
 
na kifo cha CCM umeanza kusikia kuanzia lini??
CCM ilishakufa toka 1995 ..Mrema na Maalim Seif walivyowachezesha shikorobo...Mnajivuna kwa kuwa na polisi vilaza wanaofanya kazi zisizowahusu...bila hivyo R.I.P kama KANU
 
Tangu 2005 nazisikia hizi habari za kifo cha CDM
Labda marehemu kafufuka na amegeuka jini sasa wanataka kumuua tena na hawawezi 😂😂😂

Yani lumumba wana nyuzi zao zakufarijiana kijinga sana. Wanajaribu ku defy uhalisia kwa porojo.

Chadema inayokufa ndio hao hao kutwa kucha wanahaha kuwafunga na kuwakataza kufanya siasa.

CHADEMA Forever.
 
Back
Top Bottom