Namlilia Ekwueme

Sadly nilikuwa naufahamu wimbo lakini mwimbaji sikuwahi kumfahamu mpaka umauti ulipomfika.
 
Kwa masikitiko makubwa nimekutana na habari zenye kichwa kisemacho mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Nigeria amefariki usiku wa Ijumaa akiwa katika matibabu katika Hospitali ya Abuja.

Kwa haraka sana niliukumbuka wimbo ulionitoa machozi mwaka 2017 uitwao " EKWUEME" aliouimba na Prospa Ochimana.

Bado familia ya Mama huyu haijatoa sababu zilizosababisha mauti ya mwimbaji huyu aliyegusa mioyo ya wengi.

Niliupenda wimbo huu kwa mara ya kwanza baada ya kumuona Dada yangu akiuimba huku akilia kutokana na hali aliyokuwa nayo wakati huo. Ni moja kati ya nyimbo zilizoangaliwa na watu zaidi ya milioni mbili katika mtandao wa youtube. Nakumbuka mbali sana.

Mwimbaji huyu aliwahi pia kuwa kiongozi wa uimbaji Dunamis International Gospel Centre.

Aliwahi kushiriki nyimbo nyingine kadhaa kwa mfano wimbo maarufu wa "Nara Ekele" na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis Abuja), "You no dey use me play" na Emma.
Wimbo wake wa mwisho, Ikem (God of power) ulitoka mwezi wa kumi na moja mwaka 2021.

Mwimbaji huyu alikuwa akiishi na mumewe Peter Nwachukwu na ameacha watoto wanne.

Kwao walizaliwa mapacha katika familia ya Aramachi Grace Eze, ambaye naye ni mwimbaji maarufu.
Ekwueme, Ekwueme.........
Your are the living God....Eze, no one like you.
Sio your the....ni You are the living GOD....Eze no one like you.....mimi mwenyewe wimbo huu ulinigusa sana...yaani sichoki kuusikiliza....
Halafu EKWUEME hafi ...ila aliyeimba wimbo huu ndio kafa(Osinachi)...
Kwa sasa una viewers zaidi ya 98 million.....kwa kweli ukimkuta mnigeria mwenye hofu ya Mungu huwa ana hofu haswaa
 
Asante sana
 
Back
Top Bottom