Namlilia Bob Nyanga Makani

Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani!

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

TANZANIA KWANZA, UZALENDO KWANZA!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa

Huu ni (unaa) yaani unafiki wa hali ya juu. Majungu yako hayatatusababisha tuichukie CHADEMA zaidi ya hicho chama chako cha Magamba na ufisadi. KARIBU CDM chama kitakachokuongoza baada ya miaka mitatu ijayo.
 
R.I.P Bob Makani! Lakini naomba kuuliza kulikoni muasisi wa Chama Chetu Cha Chadema hakuuzuria msiba wa muasisi mwenzake kwenye msiba? Namuulizia mzee mzima Edwin Mtei!
governor.jpg
 
Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani!

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

TANZANIA KWANZA, UZALENDO KWANZA!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa

Nape, Umeandika as if Mzee Makani alikuwa anakueleza nini kilikuwa kinaendelea ndani ya chama chake (soma hapo kwenye red). Lakini bado najiuliza, haya mapenzi ya wana-ccm kwa muasisi wa CHADEMA yamechochewa na nini?
Publicity? Uzalendo?

Kimbelembele cha ccm kwenye misiba ya CHADEMA kinatia kinyaa, tuliona kwenye msiba wa Regia Mtema, sasa Mzee Makani. Lakini CCM hawa hawa walikuwa kama hawapo duniani wakati wa Msiba wa mkuu wa Majeshi na mpigania uhuru wa nchi hii Dr Kyaruzi! Nape alipata hata wasaa wa kucheza gofu wakati watu wako makaburini wakimzika Dr Kyaruzi! Leo anaongelea siasa za chuko na uongo ndani ya CHADEMA?

Kuna chama kinachougua siasa za chuki zaidi ya CCM? Dr Mwakyembe anaumwa na nini Nape? Kwa nini ngozi ya Dr Mwakyembe inatoka mba? Nape anapata wapi moral authority ya kuhubiri siasa za vyama vingine wakati wana-ccm wenzake wanamuita gamba? Anakumbuka kauli ya Maige?
 
R.I.P Bob Makani! Lakini naomba kuuliza kulikoni muasisi wa Chama Chetu Cha Chadema hakuuzuria msiba wa muasisi mwenzake kwenye msiba? Namuulizia mzee mzima Edwin Mtei!
governor.jpg

Ndallo, kuna misiba mingine inakuwa mizito kwa watu wa karibu na marehemu kuhudhuria. It is too much for them. Tuliona msiba wa Nyerere, Mandela hakuja (it is too much for him). Pia nakumbuka msiba wa Michael Jackson, Diana Rose, na Quincy Jones walikataa kabisa kuhudhuria hafla ya kumuaga marehemu. Kila mtu ana namna yake ya kuomboleza. Hata kwenye familia zetu mara nyingi baadhi ya wazazi hukataa kabisa kushuhudia maziko ya watoto.
 
Naungana na wewe FJM! Asante.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkama - Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.

Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.

Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.

Mkama ni mmoja wa vipanga wa hekima CCM na kama sikosei ni mzee wa siku nyingi ndani ya chama. Yaani alishafanya kazi serikalini mpaka akastaafu kwa mujibu wa sheria (baada ya kutimiza miaka 60).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom