Namlilia Bob Nyanga Makani

Nape my Brother!

Cheo chako ni kikubwa sana, wewe ni kioo cha ccm, lolote utakalosema ni tamko la chama, jifunze kuwa na busara kidogo. As a matter of fact just try to learn from JJ Mnyika, ni kijana mdogo sana kwako lakini mtu akiwalinganisha in every aspect of life ni kama kichuu na mlima, JJM hana papara na hata siku moja hakurupuki. Kuna mtu kashauri achana na siasa huziwezi kwani kila siku unazidi kujidhalilisa wewe binafsi hali kadhalila na chama chako.

Fikiri kwa kina kabla ya kuandika au kusema kitu especially in public.

Ni heri CCM kufa kuliko wewe kufa kifikra kwani umri wako bado ni mdogo sana!
 
Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

Kwa mila zetu huwa tunasubiri kwanza mtu alazwe kwenye nyumba yake ya milele, then ndiyo spin zinaanza. Kwa wakati huu ilitakiwa ama kukaa kimya ama kuifariji familia ya marehemu. ukiingiza siasa kwenye hili basi usijisikie vibaya pale utakapoitwa mchawi, maana kwako wewe kifo hiki kimekupatia opportunity ya kuingiza agenda yako (siasa) (Umefurahia kifo, badala ya kulia).

Actually I was pleased with your first line but get off after the highlighted. Hii ni opportunity ya Bob Nyanga Makani si opportunity yako wewe Nape. Mwanadamu ana siku muhimu kabisa mbili nyingine ni ziada tu:

1. Siku ya kuzaliwa: watu husherehekea na kusifia kuwa amepatikana 'dume' au 'mwanamke wa shoka' na kuona future iliyojaa mwangaza na nuru ya upendo. Siku hii hupita na mengi katikati hufuatia

2. Siku ya kufa: Hii ni siku ambayo mbali tu huacha majonzi bali hutumiwa ku-reflect positively yale ambayo marehemu amayaacha nyuma yake huku tukimuombea 'maghafila' - amani na utulivu huko aendako ambako nobody knows what it looks like. Ni siku ya kumuenzi marehemu na kumuombea kila jema na pia ni siku ya kuwaunganisha wale wote walioguswa moja kwa moja na kifo chake si siku ya kuwagawa.

Nape kwa thread yako hii ambayo inagawa hujaitendea mema siku ya Bob Nyanga Makani. Ume-spoil siku yake na hii inaonesha wazi kuwa hujaguswa na msiba huu maana ungeguswa ungekuwa ni miongoni mwa walioungana si kutaka kutugawa. Bon Nyanga mbali tu ya kuwa ni muasisi wa chama cha siasa lakini amewahi litumikia taifa hili katika ngazi kubwa kwa uadilifu mkubwa sana kitu ambacho watumishi wengi wa level yake leo hii wanakikosa. Huo ulitakiwa kuwa ni ujumbe wako.

RIP Bob Makani, sisi wote ni waja wa mwenyezimungu na marejeo kwake ni wajibu.

!!!!!!!!!!!!!!!!KWAHERI BOB NYANGA MAKANI!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine hua ninapata shida sana ya kujua namna Nape huwa anafikiria, i mean namashaka sana kama huyu kijana huwa anafikiri kwa kutumia Kichwa au kitu kingine au hata njia anayotumia kuona, sodhani kama huwa anaona kwa kutmia macho, i doubt, wakuu labda mnisaidie!

Kwanini huwa haoni matatizo ya kisheria kwa bwana chenge, utendaji wa mwenyekiti wake, mapenzi ya Nyerere na misimamo yake juu ya chama chake na je, angekuwepo leo huyu mwasisi wa chama chake, je angeendelea kuwepo humo? anyway, RIP kamanda Bob.
 
nape hizi taarabu zako kuna siku utajisahau utaziimba kanisani kama umweza kuziimba katika msiba.
 
Upumbavu ni kutumia msiba kama jukwaa la kisiasa. Na upumbavu zaidi ni kujifanya msemaji wa chama kingine.
 
Nape jifunze ustaarabu..........huwezi kujifanya kumsifia marehemu huku unakiponda chama chake at the same time.
This is typical immature behaviour and cant be tolerated.
Wewe ni nani uyajuaye ya ndani ya CHADEMA kuliko wenyewe wanaCHADEMA? Stop this nonsense utterances!!!

GROW UP or SHUT UP.

Upo sahihi Bigirita huyu bwana ni wa kumsamehe tu maana hajui atendalo !
 
Nape utamaduni wetu ni wa thamani sana kwenye maswala ya misiba kama watanzania huwa hatuweki mambo ya siasa . Ulikuwa wapi usiseme hayo unayoyasema humu wakati Marehemu Makani alipokuwa hai? Usiwe mnafiki na fikra zako finyu .

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Ndugu Nape, ni aibu isiyo na kipimo pale mwana-adam anapoamua kutumia msiba kupata cheap political points. Katika waraka wako hapo juu, umeanza vizuri, lakini umeharibu ulipoanza kuingiza maoni yako ya kipropaganda dhidi ya CHADEMA kwa kumtumia marehemu bob Makani. Being a politician doesn't mean you should be uncouth, even for a deep green cadre of CCM like you. SHAME ON YOU!!
 
Wewe humwelewi Nape, kwenye kauli yake hiyo si kweli kwamba kaweka siasa kando. Ni lini aliongea na Marehemu akamwambia anakerwa na hili au lile.
 
Mkama - Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.

Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.

Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.
 
Kwa mila zetu huwa tunasubiri kwanza mtu alazwe kwenye nyumba yake ya milele, then ndiyo spin zinaanza. Kwa wakati huu ilitakiwa ama kukaa kimya ama kuifariji familia ya marehemu. ukiingiza siasa kwenye hili basi usijisikie vibaya pale utakapoitwa mchawi, maana kwako wewe kifo hiki kimekupatia opportunity ya kuingiza agenda yako (siasa) (Umefurahia kifo, badala ya kulia).

Actually I was pleased with your first line but get off after the highlighted. Hii ni opportunity ya Bob Nyanga Makani si opportunity yako wewe Nape. Mwanadamu ana siku muhimu kabisa mbili nyingine ni ziada tu:

1. Siku ya kuzaliwa: watu husherehekea na kusifia kuwa amepatikana 'dume' au 'mwanamke wa shoka' na kuona future iliyojaa mwangaza na nuru ya upendo. Siku hii hupita na mengi katikati hufuatia

2. Siku ya kufa: Hii ni siku ambayo mbali tu huacha majonzi bali hutumiwa ku-reflect positively yale ambayo marehemu amayaacha nyuma yake huku tukimuombea 'maghafila' - amani na utulivu huko aendako ambako nobody knows what it looks like. Ni siku ya kumuenzi marehemu na kumuombea kila jema na pia ni siku ya kuwaunganisha wale wote walioguswa moja kwa moja na kifo chake si siku ya kuwagawa.

Nape kwa thread yako hii ambayo inagawa hujaitendea mema siku ya Bob Nyanga Makani. Ume-spoil siku yake na hii inaonesha wazi kuwa hujaguswa na msiba huu maana ungeguswa ungekuwa ni miongoni mwa walioungana si kutaka kutugawa. Bon Nyanga mbali tu ya kuwa ni muasisi wa chama cha siasa lakini amewahi litumikia taifa hili katika ngazi kubwa kwa uadilifu mkubwa sana kitu ambacho watumishi wengi wa level yake leo hii wanakikosa. Huo ulitakiwa kuwa ni ujumbe wako.

RIP Bob Makani, sisi wote ni waja wa mwenyezimungu na marejeo kwake ni wajibu.

!!!!!!!!!!!!!!!!KWAHERI BOB NYANGA MAKANI!!!!!!!!!!!!!!!!

Hofstede,
What a powerful memory has it been to listen to Dr. Remmy Ongala's song!Nilikuwa ndo nakua kua and these were the only songs from RTD. The kid that I was, when I try to look back now, most of the things that were mattering to me so much back then, do not matter any more!! Just life and these sweet memories!!!!
 
Last edited by a moderator:
599371_314311975321419_1186685600_n.jpg

Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal
pamoja na Mama Salma Kikwete leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na
viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa
waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika
nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho
 
Tatizo la viongozi na wanachama wa ccm wanafikiri tupo kwenye miaka ya sitini kwamba chochote watachosema watu watakiamini tu moja kwa moja...

Nimwambie tu Nape nakumsaidia huo wakati ushapita uelewa wa watu ni mkubwa sana kwa sana na kila kauli inayotolewa inachambuliwa kwanza kuona Mantiki iliyopo.

Hakuna Mtu yoyote mwenye akili timamu anayeweza kumuamini Nape kwamba muasisi wa Chadema(Makani)anakerwa na siasa zinazoendeshwa na Chadema kipindi hiki ambapo Chama kimepata umaarufu zaidi kutokana na uongozi wake shupavu wa sasa chini ya kamanda Mbowe. Chama kina uwakilishi mkubwa zaidi Bungeni na katika ngazi ya Halmashauri, Vijana wengi katika hii Nchi aidha ni wanachama au wafuasi wa Chadema yote haya yanatokana na Siasa zilizojaa ubunifu, umakini na uzalendo kutoka kwa viongozi wa Chadema na hapo ndipo Nape na Chama chake cha Magamba wana weweseka nakuitamani Chadema ya kusadikika.
 
Nape acha siasa uchwara za kuchanganya risala ya marehemu na siasa za CCM VS CHADEMA.
 
Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani!

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

TANZANIA KWANZA, UZALENDO KWANZA!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa

Hivi nape kweli unashindwa kuwaza hata kidogo????

Unadhani hicho ulichokipost ndicho hasa kinaweza kukiongezea sifa chama chako??

Au unadhani hicho ndicho kitakuongezea heshima??

Kweli sikio la kufa halisii dawa!!.....Kufeni bwana kwa ujinga wenu!
 
Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani!

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

TANZANIA KWANZA, UZALENDO KWANZA!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa
haki kweli wewe utakuwa mgonjwa wa akili kweli kabisa.....kwanza nilipoona jina la thread nilitegemea nitakuta tahariri yenye akili kumbe huu upupuu......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom