Namlilia Bob Nyanga Makani

Namlilia Bob Nyanga Makani

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani!

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!

TANZANIA KWANZA, UZALENDO KWANZA!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa
 
Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako!

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa Itikadi & Uenezi Taifa

Nape,
That is what I like most about politicians...they are all the same and sometimes it is difficult to know which is which..
 
Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako!
Kwenye red sikubaliani na wewe Gamba. Nape naona mnataka kutafuta haki miliki ya huu Msiba kama wa kanumba
 
Nape, kwa hili leo tuko pamoja, tuweke mambo ya siasa kando tuangalie msiba kwanza, tuko pamoja kwa hili tu. Pumzika kwa amani Mzee Makani
 
Nape, kwa hili leo tuko pamoja, tuweke mambo ya siasa kando tuangalie msiba kwanza, tuko pamoja kwa hili tu. Pumzika kwa amani Mzee Makani

Kitu cha msingi ni kumuombea mapumziko mema yenye raha Marehemu Makani. Lakini naona katibu mwenezi amepiga siasa kidogo pale.
 
Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani! Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako!

Kwenye maandishi RED naomba ufafanuzi kidogo sijui kama ilikuwa ni lazima kuandika uliyoandika.
 
Ujinga mwingine hovyo kabisa!

Unaleta siasa taka katika msiba??

Stupidity & Idiocy@ its best!
 
Imani yangu inakataa kuwaombea marehemu kwenda mbunguni [mapumziko mema] tunaamini kama ulitenda vyema wakati wa uhai wako unastahili mapumziko mema kama ulitenda mabaya unastahili moto wa milele hata watu wakikuombea mchana na usiku haitosaidia kitu.

Kitu cha msingi ni kumuombea mapumziko mema yenye raha Marehemu Makani. Lakini naona katibu mwenezi amepiga siasa kidogo pale.
 
Nape jifunze ustaarabu..........huwezi kujifanya kumsifia marehemu huku unakiponda chama chake at the same time. This is typical immature behaviour and cant be tolerated.

Wewe ni nani uyajuaye ya ndani ya CHADEMA kuliko wenyewe wanaCHADEMA? Stop this nonsense utterances!!!

GROW UP or SHUT UP.

Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!
 
Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani! Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!
Wee, mbona haya hukuwahi kuyasema au kumsifia Bob Makani wakati akiwa hai? Hii inasaidia nini kwake au hata kwetu? Pili, hivi huoni wanasheria uchwara kwenye Chama chenu cha Majambazi?

Jaji Werema humuoni kama ni Majitaka ktk tasnia ya Sheria nchini? Huoni akina Chenge, pamoja na kusoma vyuo mashuhuri duniani alivyo? Kwa Bob umeona nini hadi unajipendekeza? Kama ni kuomboleza, wewe omboleza tu kama Mtanzania mwingine yeyote yule, kuingiza siasa kwa kuongelea vyama wakati tuko kwenye msiba ni UJUHA!

Juzi pale Jangwani hukumaliza maneno yako hadi uyalete kwenye msiba wa mwenzio? Au hukupata wasikilizaji?
 
Imani yangu inakataa kuwaombea marehemu kwenda mbunguni [mapumziko mema] tunaamini kama ulitenda vyema wakati wa uhai wako unastahili mapumziko mema kama ulitenda mabaya unastahili moto wa milele hata watu wakikuombea mchana na usiku haitosaidia kitu.

Ngongo,
Usifanye kitu kinyume na imani uliyonayo. Hata hivyo wengine imani zetu hazina shida kwenye hilo. Na kwa kuwa thread si ya upande gani uko sahihi katika unaloliamini na kulifanya, basi kwangu mimi, bado ntaendelea kuomba na kusema RIP Mzee Makani.
 
Last edited by a moderator:
Nakanusha usemi wangu, sikuwa nimesoma between lines, Nape huo ugomvi uliuona wapi? Umeharibu maana nzima ya thread yako
Nape, kwa hili leo tuko pamoja, tuweke mambo ya siasa kando tuangalie msiba kwanza, tuko pamoja kwa hili tu. Pumzika kwa amani Mzee Makani
 
Hawa ndio aina ya viongozi wa ccm ilionao hivi sasa, hata kwenye masuala yanayopaswa kuweka itikadi ya vyama pembeni na kuungana pamoja ktk kuomboleza msiba wao wanaendekeza kupiga vijembe na umbeya chadema tu. Ni aibu kwa chama chochote kuwa na kiongozi wa juu mwenye upeo mdogo wa mambo kama alivyo nape nnauye.

Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana kaka, nadhani kwenye siasa ulivamia tu, siyo mahali pako. ushauri wangu wa bure, ungefikiria aina nyingine ya kazi ya kufanya, siasa achia wenyewe mnafiki mkubwa wewe.
 
Nimeshtuka kidogo kusikia muswiba wa Mohamed Makani au wengi walivyozoea kumuita (Bob Makani). Kwa kweli ni mswiba mkubwa sana na Tz wamepoteza jabali lisiloteteleka wala kutingisika.

Binafsi nilimfahamu Mohammed Makani mwaka 1974 wakti huo akija nyumbani kwa ammi yangu marhum Eng. Abdullah Salem Al harthy, mtaa wa mazengo upanga ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi sana na walipenda sana kuongea kisukuma.

Na alinisaidia sana katika utendaji wangu wa Kazi wakti nikiwa Wizara ya fedha na hata nilipopelekwa Mwanza wakti akiwa BOT kama naibu gavana (Bara) na vile akiwa naibu wanasharia mkuu.

Ni mtu makini sana na asiyyemung'unja maneno na masema kweli daima. nakumbuka mara ya mwisho nilikutana nae siku nilipokwenda Mbazi beach kumwangalia Brig General Mwakanjuki mwezi mei 2011 nilipita mpaka kwake jioni na tuliongea sana. Nakumbuka neno lake la mwisho ni kuwa lazima Tanzania itabadilika na ukweli utawala. WaTz wameshaelimika na kuchagua ukweli kuachana na batili.

Nakukumbuka sana Mohamed Makani.

Inna Lillahi wainna illaihi rajihunna.
 
Kwenye maandishi RED naomba ufafanuzi kidogo sijui kama ilikuwa nilazima kuandika uliyoandika.
Yaani hawezi kuandika kitu ambacho kina mantiki bila ya kuharibu, hivi kati ya CCM na CDM ipi yenye siasa za chuki, ubabaishaji, uongo, uzandiki na kila aina ya ghilba?

Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini!
again...hypocrisy at its very very best......typical also of what JK does.. when attending virtually all funerals in town....
 
Poor Nape. Hukuhitaji kuikashifu CDM kwa kiwango hiki. Jaribu hekima za watu kama Membe na Mwakyembe.
 
Back
Top Bottom