Namibia, Zimbabwe zakataa kulinda utu, haki za binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
New York.
Namibia jana ilikuwa miongoni mwa nchi 21 zilizopinga kuingizwa kwenye ajenda za kujadiliwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa hoja inayotaka kulazimisha nchi wanachama kuunga mkono misingi na kanuni zinazolinda utu wa binadamu.

Nchi 112 ziliunga mkono pendekezo huku 17 hazikupiga kura. Nchi nyingine zilizopinga ni Zimbabwe, China, Myanmar, Korea Kaskazini, Urusi, Iran, Pakistan, Sudan na Syria wakati Iraq, Saudi Arabia, Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu, Brazil, Denmark, Israel, Japan na Malaysia ni miongoni mwa nchi zilizounga mkono.

Rais Hage Geingob na baadhi ya mawaziri wanahudhuria mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini hapa hadi Ijumaa.

Miongoni mwa mawaziri wanaohudhuria mkutano huo ni wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Netumbo Nandi-Ndaitwa, wa mazingira Pohamba Shifeta, wa madini Obeth Kandjoze, Tom Alweendo na Sophia Shaningwa.

Australia na Ghana ziliwasilisha pendekezo lisemalo “Wajibu wa Kulinda na Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Vita, Manyanyaso ya Kikabila, na Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu” kwamba liingizwe katika ajenda za Mkutano Mkuu wa 72 wa Umoja wa Mataifa (UNGA).

Msimamo huo wa Namibia umekuja wakati nchi hiyo inaitaka Serikali ya Ujerumani kulipa dola za Namibia 400 bilioni kama kifuta machozi cha mauaji ya kimbari kati yam waka 1904 na 1908.

Tovuti ya UN inasema kwamba pendekezo hilo linataka kuchukuliwa kwa hatua namna ya kuimarisha mshikamano wa sheria za kimataifa za utu na haki za binadamu na kumaliza tabia ya kuponyoka mkono wa sheria na ukatili kwa maelfu ya watu.

Katika tovuti hiyo, pia takwimu zinaonyesha kwamba watu milioni 65 walikimbia makazi yao kutokana na migogoro, mateso na ukatili.



Mwananchi
 
OK, kawaida sana hii.

Kwanza wazungu koko ndiyo wanaoongoza kwa kukiuka haki za binadamu.

Mfano, ubaguzi wa kidini, uonevu wa wahamiaji, unyanyasaji wa races zingine nchini kwao and the likes.
 
Back
Top Bottom