Namhurumia mdogo wangu, lakini aliyataka mwenyewe

Namhurumia mdogo wangu, lakini aliyataka mwenyewe

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,363
Reaction score
16,092
Habari za uzima wakuu, binafsi nashukuru kwa uwepo wa huu mtandao, kwani imekuwa ni sehemu ya kufarijiana, kutiana moyo pamoja na kupeana ushauri kwenye mambo mbali mbali yanayotokea kwenye jamii yetu.

Nakumbuka niliwahi kuleta uzi humu wa "hapa kuna mapenzi kweli au napotezewa muda" wengi mlinipa ushauri mzuri na mimi nikakaa chini nikatafakari na kufanyia kazi nikaona kabisa, ningeendelea kuumia tu kwenye yale mahusiano hivyo, nilishamove on, kila mtu anaendelea na mambo yake. Napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote mlionishauri na kunifumbua macho kwenhe huo uzi tajwa hapo juu.

Naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni la uzi huu sasa.

Nina mdogo wangu, umri hatujapishana sana, ni kama 2yrs hivi nadhani, huyu mdogo wangu kipindi yupo O'level alipata mimba akiwa form three hivyo ikamlazimu aache shule akae nyumbani aelee mimba.

Akajifungua mtoto wa kike akamlea hivyo hivyo kibishi kibishi maana anaishi na mama tu, baba yake alishatangulia mbele za haki, kwahiyo mama yake na dada mkubwa ndiyo walipambana kwaajili yake na mtoto na mtoto akakua, sasa ikatokea kwenye mizunguko yake akapata mwanaume dereva wa malori ya kwenda huko nchi za watu, kumbe tangu wanaanza mahusiano hadi wakaja kufikia hatua ya kuishi pamoja mdogo wangu hakusema kama ana mtoto alikuwa anamwambia mwanaume wake yule mtoto ni wa dada.

Ikatokea kuna rafiki yake na huyu mdogo wangu akamfungukia ukweli shemeji, shemeji naye akampgia dada mkubwa kumuuliza dada akamwambia ndiyo mtoto ni wa mwanamke wako ila mimi nipo karibu naye na kanizoea sana ndiyo maana ananichukulia kama mama yake na kuniita mama. Mwanaume kusikia vile alichoka na vile yeye hana mtoto, basi ikatokea kutokuelewana na ugomvi, mdogo wangu aliomba sana misamaha ila shemeji akamlia buyu.

Ila mapenzi hayashauriki, baadaye wenyewe wakaja wakapatana na wakaanza kuishi pamoja, sasa yule aliyetoa taarifa ndo akaanza kuonekana mnafki na kibao kikamgeukia yeye pengine anamtaka shemeji 😅😅 mwisho wa siku mapenzi yamenoga, wakaamua wafunge na ndoa. Hii ndoa mie sikushiriki maana mambo yalikuwa mengi hapo kati ila inshort huyu mdogo wangu alituona sisi ndugu hatufai akawa kivyake vyake, baada ya kumpata huyu mwanaume zile pesa alizokuwa anapewa na kuachiwa na kadi ya benki akatoe pesa muda wowote akihitaji akaona maisha kashayapatia, na mie hata kwenye hiyo harusi sikualikwa na yeye nilikuja kuambiwa na mtu baki.

Sasa baada ya kuoana shemeji akamwambia mdogo wangu kuwa mtoto amlete wakaishi naye hapo kwao hawezi kuwa anatoa huduma mara mbili mbili, maana yeye ndiyo kashapenda boga inabidi alipende na ua lake basi mdogo wangu alikuwa anagoma mwanzo shemeji akawa mkali ndiyo kukubali sasa kumbe alikuwa anagoma anataka mtoto akae kwa bibi yaani mama yake na mdogo wangu ili yeye bi shosti aendelee kula bata na mashosti maana ndiyo mambo ayapendayo, kisa mwanaume anahudumia alijituliza zake nyumbani hawazi kazi wala nini ni kula bata kwa kwenda mbele tu.

Sasa shemeji alisafiri na akisafirigi anakaaga huko hata miezi mitatu nadhani, siku ya siku karudi nyumbani mtoto si akaanza kumfungukia " baba unajua mimi nina baba watatu, wewe ukiondokaga kuna baba mwingine anakujaga anatutoa mimi na mama, na mwingine tena tunaendaga naye bar yeye na mama wanakunywa pombe mimi wananinunulia pipi, juisi na biskuti" sasa mtoto wa miaka mitano anaona ni kitu cha kawaida tu hapo kaongea, shemeji alivyoambiwa hizo habari akaenda kuchukua kadi yake ya benki akaondoka zake na hata kuaga hajaaga, mdogo wangu tena ndiyo kaanza kuchanganyikiwa kumtafuta kamkuta huko Bar gani sijui na ni nje ya Dar, kamkuta yupo anakunywa vibaya mno wakati since anaoa alishaahidi kuacha,,,,,,,, kufika pale bi shosti kaanza kumuomba warudi nyumbani mwanaume akamwambia wewe niache ntarudi mwenyewe.....na inasemekana kwamba hata ndugu wa mwanaume walishamuonya shemeji kuwa huyu mwanamke hafai kafata pesa tu,,,,, ila shemeji akawa mbishi akaamua kumuoa......hizo habari mimi mwenyewe nimepewa na dada mkubwa,,,,

Tamaa zimemponza mdogo wangu hii ndoa naona kabisa akiipoteza kwa ujinga na upumbavu wake maana mpaka sasa hakuna maelewano mwanaume kamkaushia na hayupo nyumbani... wanaume mnaotaka kuoa msikurupuke kuchagua mke, na nyie wanawake mwanaume akikupenda kukujali na kukuthamini muheshimishe,,,, yangu ni hayo tu.
 
Kuna fununu hata yule mzeeee alhaji Tanganyika bin sultan NAYE alichapiwa na ALIKUA na usukani kwa HIYO apige MOYO konde NDO laifu ILA mi NIKAGUNDUA du kanisalit napga chini ALAF HUYO SIO demu ni MKE asha olewa HAO NDO wanaomba ma ex zao PESA wawanunulie wame zao futariiiii



Kwishaaa



Bro Alex on da beats yoow
 
Ukitaka kufanya uchafu kwenye ndoa usifunge ndoa kile kiapo ni lazima tu kitakuumbua hata uwe unatoka usiku wa manane ukidhani watu hawkuoni ukijiona ni mjanja ukishachwa ndipo utajiona mjinga.
Muache awe lishangazi mjini,ukishafungiwa mlango wa ndoa we fanya KAZI ya kufuga vivulana tu viwe vinafanya kazi ya kukuchungulia tu,hadi ukikua ujutie upumbavu wako.
 
Back
Top Bottom