Namesomea Animal health & production; Natafuta kazi

Abigail2011

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
519
230
Wadau heshima kwenu;
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 24,nimemaliza certificate yangu pale Livestock institute training Agent ( Lita) morogoro.Sasa nawaombeni kwa heshima na taadhima wapi/mahali naweza pata kazi angalau niweze kupigapiga hapo kazi nijibane niweze kupata hapo vijisenti maana mimi dhumuni langu ni kujiajiri pindi ntakapoweza kusimama imara.Asanteni sana,nawakilisha.
 
Anza na kuku 2 majike na Dume moja fuga kitaalam baada ya miaka 5 nitafute una kuku wangapi.
 
Fatilia tanapa wametangaza Kaz jamii ya ulichosomea

TANAPA wanataka watu waliosomea wanyamapori, kimsingi huyu amesomea mifugo (wanyama wanaofugwa nyumbani au mashambani). Nimelisoma lile tangazo la TANAPA, ushauri wako ni mzuri lakini kwa mujibu wa watu wanaotakikana na TANAPA kwa ajira zilizotangazwa, ushauri wako hauta mfaa wala kumnufaisha mleta mada.

Cheers!
 
Hapo Mkuu jitahidi kujitolea kuwapa ushauri wafugaji walio karibu na wewe na kisha utakuwa unapewa kazi ya kutibu hiyo mifugo na hela ya kwenda kununulia dawa watakupa wenyewe huo ndo naona utakuwa mwanzo wa kujulikana na kujitengenezea ajira mwenyewe
 
Interview:
Unafikiri utakuwa tayari kufanya kazi ukilipwa kama shs ngapi?
What is your expected minimum salary?
 
Back
Top Bottom