Namchukia mzee wangu!

Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na HERI duniani. Kwa chuki hii uliyonayo juu ya mzee wako ambaye ametimiza majukumu yote kama Baba naona wewe bado akili yako ni changa sana.

Majukumu yote ya mzee wako kama Baba naona umeyaorodhoresha kwamba aliyatimiza vema bado unampongeza kwa 5%, huu binafsi naona ni uchanga wa fikira na udumavu wa akili.

Suala la kujenga nyumba ndo lisababishe chuki kiasi hiki kwa mzee, napata hisia kama angejenga nyumba nzuri bado ungemlaumu na kumchukia kwa kutonunua GARI.

Mwaka 1988 you’re now 33yrs please try to think and act like a mature folk! Wengine tulivyopata kazi jukumu la kwanza lilikuwa kuwajengea nyumba wazee wetu kwani tulijua vema kama wasingetumia rasilimali zao kutusomesha pengine wangeishi maisha ya kifahari.

Kumtuhumu mzee wako kwamba pengine alichepuka na mwanafunzi ni ushahidi tosha kwamba akili yako ni duni kwani hata kwa usilolijua you only think negative

Mwisho, nachokiona baada ya kusoma btn the line, mzee wako angeweza kukwambia sababu ya yeye kuacha kazi ila tatizo anaona akili yako bado ni ndogo kwani kama ulivyosema akianza tu kuzungumzia suala hili kwa chuki zako za kijinga unaondoka.

Muombe msamaha mzee wako, tubu dhambi na omba shetani huyo unayembeba moyoni mwako kwa miaka mingi akuache. Mungu ni mwema atakusamehe uovu huo ataondoa moyo wako wa jiwe na atakupatia moyo wa nyama.

“La Aquila Non Capit Muscas”
 
Mkuu naomba nikuambie tu kuna watu wako hivyo, yaani yeye material things haziko sana akilini mwake... sasa bahati mbaya akapata mke aliye hivyo inakuwa balaa. Lakini mshukuru na umpende tu mzee wako. Jitahidi weka wewe mazingira mazuri ukiweza.
Angalau naweza rudisha moyo kidogo.
 
So sad yani..aliyesema asieweza kushukuru kwa dogo hata kubwa hatoweza hakukosea. Ifike mahali tu appreciate juhudi za wazazi wetu kwenye kutafuta.
Kabisaa wazazi wengi wamepambana sana ili sisi tusome na kupata mahitaji mengine
 
Labda hawezi kufanya kila kitu..na ameamua kufanya vile anavyoona vinampa furaha. Mfano kama hivyo kawasomesha na kuwapa mahitaji yenu yote.

Si mumrekebishie hapo home, au hataki?
Mtu akiamua kukuchukia anatafuta sababu ya kukuchukia. Huyo mpuuzi ameamua kuchukua tatizo la nyumba yenye nyasi. Kila mtu akianza kuonesha mikwamo ya wazazi hapa, hapatatosha. Wengine tulinyimwa karo na waliojitolea kutupatia karo zilipotea ila yote tisa, kabla hawajafariki tuliwajengea maghorofa kijijini huko Liwale kwetu
 
mambo ya kuvumilia kabisa fanya yako sisi mzee wetu amestaafu mdogo eti miaka 49 shida ili alipwe mafao akaoe maana aliachana na mother kisa ndugu miongoni mwa vitu ungemchukukia kama ungekuwa mzee wako walianza kazi huko mbeya intake moja miaka ya 78 na wenzie wanne wakaamishwa kweny mkoa x kwa pamoja wenzie wote walijenga mapema wanastaafu wamejnga nyumba mbili mbili twende sasa yeye pesa za kustaafu ndo anajenga nyumba ikiwa hapo mtot wake wa kwanza ndo yupo form four hana biashara halafu mtoto wa kike sasa then tupo watano

miongoni mwa mambo aliyofanya mzee wetu kupenda sana ndugu zake alinunua kiwanja akishirikiana na mama wakajenga msingi then akaenda kujenga kwao tena vitu ananua analeta tulipopanga then anasafirisha kijijini mabati ,cement mbao .wadogo zake wapo 9 jumla na yeye 10 kawanuunulia kila kitu baiskeli kule kijijini mi naanza form one sina baiskeli nauli shida nakanyaga wadogo zak watano kila mtu na baiskeli yake tena wakubwa wana watoto 😛😛😛
hela za kustaafu kapeleka kwao huko kijijini nyingine kaoa mke hawasemeshni mpaka leo huyo mke hataki ndugu hapo kwake maana watoto wa baba sisi hatupo wote watano tuajitegemea wamwisho yupo kwa mama anasoma

mipngo yake anajadiliana na mdogo wake wa kike ambaye ni shangazi yetu anajua kila kitu cha mzee kuliko sisi yaani hapo tushafika umri wa miaka 18 wengi 30

sasa wewe ingekuwa mzee wako si ungemtukana
 
Unadhani hayo mafanikio madogo uliyonayo ungeyapata Kama ungezaliwa kwa mzazi yeyote Tanzania hii?
Halafu sababu uliyoitoa mwisho ni ya kipumbavu, eti ulishindwa kuleta demu ndani kwasababu ya uchakavu wa nyumba yenu
 
Kweli aisee..
 
Yeah ningemtukana
 
Imeandikwa.
"Waheshimu baba na mama yako, upate miaka mingi na Heri duniani"
rejea maandiko matakatifu.
 
Shukuru Mungu Una Baba Mzazi Sisi tulitamani awepo tu tumwone wtt wake ila Mungu ana mpango wake..... Kuna kipindi utatamani awepo mchukulie ni udhaifu wake ww pambana Mambo yakikaa Sawa vizuri ndo utasahau...
 
Shukuru Mungu Una Baba Mzazi Sisi tulitamani awepo tu tumwone wtt wake ila Mungu ana mpango wake..... Kuna kipindi utatamani awepo mchukulie ni udhaifu wake ww pambana Mambo yakikaa Sawa vizuri ndo utasahau...
Ahsante
 
Nyumba inajengwa baada ya kile kidogo kilichobaki,ss kama kuhusu shule na mahitaji ya nyumbani aliweza kusimamia vizur kuhusu nyumba nyie ndio mnatakiwa mpambane au ulitaka ajenge nyumba ukose elimu ?
 
Hatukuwahi kulala njaa,
Alikuwa akitutoa out
tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.
Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa
alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule
kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara.
Huna shukurani wewe
 
Wapo watoto wanaotamani angalau wapewe hizo huduma na wazazi wao, haswa baba zao lakini wametelekezwa!

Muombe Mungu kwa imani yako akusamehe. Kama hupendezwi na hali ya nyumba ya mzee wako unaweza kuifanyia marekebisho lakini si kumsimanga na kumuonyesha chuki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…