Namba 15544 ya vodacom

Namba 15544 ya vodacom

ymollel

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
3,095
Reaction score
2,294
jamani namba hii 15544 imekuwa kero. Yaani kama simu yako haina uwezo wa ku-Block number basi utateseka sana. kuna namba nyingine pia ya Tigo nayo inasumbua kichizi. Dawa tu ni Kuweka Auto Reject / Blocked List
 
Vodacom wanakosea sana. Hii namba ukiangalia salio inaleta message kama millioni hivi.
Kiukweli wateja hawasomi usumbufu kama huu. Kwanza unakuta maneno yanayokuja yanawakwaza watu. Can you imagine linakuja swali la wimbo sijui wa bongo fleva gani wakati mi na BF mbalimbali.

Forcing a customer to read offensive advert is sure way of chasing him and business-wise its stupidity of highest order.

hope that vodacom CC account bado iko inafanya kazi. Tufikishie message Invisible
 
Last edited by a moderator:
kwa kweel nilidhani hii kero ni yangu mwenywe ila tupo wengi voda tafadhalini angalieni hili tatizo hiyo namba ina sumbua saa tena kwangu zina ingia sms mbili kila baada ya masaa manne
 
Siyo hiyo tu ipo na nyingine 25515600 wananisumbua hadi kero
 
jamani namba hii 15544 imekuwa kero. Yaani kama simu yako haina uwezo wa ku-Block number basi utateseka sana. kuna namba nyingine pia ya Tigo nayo inasumbua kichizi. Dawa tu ni Kuweka Auto Reject / Blocked List
Ha ha ha ha haaaah, mkuu naona leo hii kero umeamua kuitolea uvivu, mi mda si mrefu nitatupa line yao kwa sababu hawana dili sasa hivi baada ya kutoa vifurushi vya mtandao mingine, sasa wamebaki kutumia masms yao ya ajabu ajabu
 
Vodacom waliangalie hivi kwa kweli. tena hiyo namba inayoishia na 600 ndio inapiga kabisa , unaweza ukafikiri ni simu ya deal inaita kumbe ni maujinga yao
 
Wapumbav sana hao nataka nihame kwanza kwa ujinga wao
 
Dooh wanaboa sana. Hivi KWA kuwa no wateja wao wanaleta msg Tu hata za ujinga? Naamini kule VODACOM kuna watu wamekwenda shule. Hivi ukiletewa msg Mara 30 za aina moja ileile utazisoma kweli? Sasa walivyo ovyo wanaleta msg ileile kwa miezi hata 2. Hivi lengo lao linatimia au kwa kuwa mtandao wanao tayari, hawalipii kitu, basi wanaendeleza ukilaza wao.
Tufikirie namna ya kuipeleka TCRA au mahakamani kabisa. Hivi mteja hana haki kuhusu hili?
 
Jamani haya mambo ni kwa mitandao yote si voda,tigo wala zantel kwa airtel sijui sina experience nayo, ila kama zantel kila siku wanatuma mamessage yao ya ofa mpk basi,tigo saa nyingine wanakupigia kabisa alafu wanakwambia sijui tumeongeza mnara mpya wa simu mkoa gani.! Na message nyingine nyingi tu za kukulazimisha sijui ujiunge na huduma gani mara upate hali ya hewa,habari za ligi kuu sijui matoke alaimradi kero tu juu ya kero.
 
Mimi mpaka nimetoa mlio kwenye sms ni kero wamenifanya situmi SMS tena ukiwe air time wanakufundisha matumizi hawajamaa wanaboa baya
 
zantel ndio wamezidi wao kila baada ya nusu saa wanatuma message tena zinajirudia sio mpya na wala hakuna cha maana
 
Kama tigo vile usiombe ukatumA SMS huku salio limeisha utakoma meseji zitakuja nyingi balaa
 
Msaaada wa mwanasheria niwapeleke mahakamani hawa voda iwe fundisho kwa wengine
 
Shinda 36,000pointi zaidi:
Zika Mwaka ni Leo! Ni sehemu gani watu hukusanyika kusali na kumshukuru Mungu?
1.Kanisani
2.Sokoni
Tuma 1au2 kwenda 15544!
 
Shinda 39,000pointi zaidi:
Tetesi! Hivi karibuni kocha mkuu wa Taifa Starts anunuliwa gari ya shilingi ngapi?
1.Milioni 78
2.Laki 3
Tuma 1au2 kwenda 15544!
 
Mkuu ymollel,

Hii imekuwa kero, na zaidi ni pale ambapo hujawahi hata kushiriki kujibu maswali yao wanayoyauliza then unaambiwa unapoint kadhaa tayari(let's say 10000), jibu maswali haya upate point zaidi, kwakuwa unaona kama inakuwa haikuhusu unaachana nayo baada ya muda unaona sms nyingine, Sasa namba yako imechaguliwa kwa droo ya leo ukiwa na Point 25,000(NOTE HAPA POINT ZIMEONGEZEKA ) BILA HATA KUSHIRIKI!

Sasa unajiuliza unazidi kupata point pale unapokuwa hujibu maswali au?!
 
Last edited by a moderator:
Kuna na ile +255ngap sijui inayopiga sim kabisa!!
 
Back
Top Bottom