Kaka kama kunamtu Mbeya asiye na ushabiki ukiongea naye atakupa clear picha.
Sugu akusanya milioni 8 mfuko wa elimu
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi Sugu, ameendelea kuzoa mafanikio kupitia mfuko wake wa elimu.
Sugu, alianzisha Mfuko wa Elimu Mbeya (MBETF) kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wasiojiweza kwenye Jimbo la Mbeya Mjini waweze kusoma bila matatizo kuanzia sekondari mpaka vyuoni.
Kwa mujibu wa Sugu, ameweza kukusanya kiasi cha shilingi 8,350,000 kutoka kwa makampuni mbalimbali ambayo yamejitolea kuuwezesha mfuko huo kutimiza malengo yake.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Facebook, Sugu ameandika kuwa Coca Cola Mbeya, imetoa shilingi 5,000,000, Lafarge-Mbeya Cemente shilingi 2,000,000 na Kampuni ya Mbeya Tanzania (TBL) shilingi 1,000,000.
Aliyataja makampuni mengine yaliyochangia kuwa ni Benki ya CRDB-Mbeya shilingi 200,000, Mwamikomo Store shilingi 150,000 na Access Computers waliotoa kompyuta moja kwa ajili ya ofisi ya MBETF, iliyopo Kata ya Nzovwe, Mbeya.
Sugu ameandika: Mimi Joseph Mbili, Mbunge wa Mbeya Mjini na Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Mbeya (Mbeya Education Trust Fund) pamoja na bodi yetu ya wadhamini, tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa makampuni hayo kwa kuchangia mfuko wetu.
Aliongeza: Ewe mwana Mbeya na rafiki wa Mbeya popote ulipo, tafadhali changia mfuko wa elimu ili tufikie malengo ya kupeleka sekondari watoto wasio na uwezo wapatao 360 kwa mwaka huu 2013. Akaunti yetu ni 01J50421214700 CRDB BANK Mwanjelwa Branch kwa jina la Mbeya Education Trust Fund.